Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Ni mada ndefu sana na sina mood ya kuanza kuelezea hilo, lkn walioweka hivyo walikuwa na sababu, ila tambua moja tu nchi nyingi Duniani pamoja na za Ulaya zina fall back position, yaani mambo yanapoharibika kuna Kiongozi au mfumo ambayo huingilia na kuokoa nchi kusambaratika, ndiyo maana unaona hata Uingereza, Mkuu wa nchi ni Ufalme chini Malkia Elizabeti na hachaguliwi na yoyote na wala hashitakiki popote pale yuko Juu ya Sheria za Uingereza, na kama mambo yakiharibika yeye ndiyo mwenye uwezo wa kuingilia, hajihusishi na Siasa za kila siku lkn Wanasiasa wakizingua ana uwezo wa kuvunja Serikali na kuunda mpya, ...
Hapo umenena vyema, hawa viongozi wetu wa kisiasa ni hatari sana kumpa madaraka makubwa.
 
Muda wa mkolomije
Screenshot_2017-03-23-07-08-27.png
 
Bashite ana nguvu kwenye hii serekali kuliko Nape Nauye. Hivi Magu na Bashite wana siri gani[emoji15] mpaka imefika kumfukuza kazi Nape.


Ndukiiiii[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Sasa ni dhahiri ukiingia anga za Bashite unaenda na maji.
Swali kubwa,kuna siri gani kati yake na 'Mufalume' hadi amlinde kwa gharama iwayo yoyote ile?
 
Tangu vita ya. ngada imeanza Nnauye alionekana yupo against na kile serikali inachosimamia mara image mara sijui nikikutwa nna mahusiano na Msaniii najiuzuru haya sasa wenzie wamemuwahi...
 
Hijacking everything and create elite club from resources that were meant for all is a sin and crime. Acha wapambane mpaka wakae sawa
 
Haya mahaba ya upinzani kwa Nnape yanathihirisha kuwa upinzani huwa wana ugonjwa wa kusahau haraka sana.

Dr Slaa pamoja na kupigania chadema kutoka wabunge wawili hadi wabunge 20, Slaa alivunjwa mkono pamoja na mke wake kuharibiwa mimba wakiwa Arusha. Mwisho wa Siku Dr Slaa alifukuzwa chadema dakika za mwisho na chama kuuziwa Chadema!! Leo hii yote hayo chadema wamesahau wako bize kumuonea huruma Nape Nauye kada wa ccm!!

Swali la kujiuliza, tangu lini chadema na upinzani kwa ujumla wakaitakia mema CCM??
Slaa aliteleza bafuni akavunjika mkono.Pili toa ushahidi wa kikao kilichomfukuza Slaa Chadeam.Slaa aliondoka mwenyewe baada ya kuhitilafiana na wenzake na isitoshe alirudi kuwakandia Chadema.
 
Ni kweli tumpe pole, ila roho wa bwana ananionyesha ufa mkubwa kule kule chumbani kwao. Ngoja tuone!
 
Hivi karibuni mara baada ya Mh. Nape Nauye aliyekuwa waziri wa habari utamaduni na michezo kukerwa na kitendo kiovu alichofanya mkuu wa mkoa wa Dar e salaam Paul Makonda kuvamia kituo cha habari cha Clouds akiwa na polisi wenye siraha za moto, Mh. Rais kwa kushangaza umma wa watanzania amemfuta kazi. Mimi kama raia wa nchi hii mwenye uhuru wa kutoa mawazo kwa mujibu wa katiba ya nchi, kitendo cha kusimamia ukweli alichokifanya Mh. Nape ni cha kizalendo kinachofaa kuigwa na viongozi wote wa kisiasa; ukweli lazima usimame hata kama kuna hatari ya kupoteza kazi na hata ikibidi maisha. Mh. Nape watanzania wote wanakuunga mkono na kumbuka kuwa maisha yapo hata nje ya uwaziri na ikibidi hata nje ya CCM. Kitendo alichokifanya Rais mimi sikushangaa kwani hiyo ndiyo tabia ya viongozi wengi wa Afrika ambao hawataki kukosolewa. Rais anapaswa kufahamu kuwa hakuna binadamu ambaye fikra zake tu ndiyo sahihi na hali hii ya kufumbia macho ukiukwaji wa sheria ikiendelea taifa hili litapoteza mwelekeo. Watanzania hapo ndipo wanapaswa kujifunza kutafakari kwa kina kabla ya kupiga kura, na hii ndiyo hatari ya chama kimoja kukaa madarakani kwa muda mrefu. Hapa naweza kusema kuwa watanzania tukomae na tuendelee kuonja madhira ya makosa tuliyofanya wakati wa kupiga kura. Mh. Nape hongera umeonesha njia hata kwa wana-ccm wengine waliopewa madaraka na Rais.
Siku zote haki huinua taifa.


 
Kwa maoni yangu kikubwa kinachomsumbua Nape Nnauye ni kutokuubali ukweli kwamba muda wake ndani ya CCM umekwisha au niseme kwamba ulikwisha siku ambayo Mwenyekiti mpya wa CCM alipochukuwa kutoka kwa Jakaya Kikwete, sasa kwa hali ya kawaida ilipaswa Kikwete na Timu yake wote waende na watoe nafasi kwa Mwenyekiti mpya kuunda Timu yake, Kikwete alifanya hivyo alipochukuwa ktk kwa Mkapa na Mkapa alifanya hivyo hivyo alipochukuwa ktk kwa Mwinyi!

Sasa kinachomsumbua Nape na timu yake ni kukubali hilo kwamba, kuna wakati unafika inabidi ukubali na kulet go!

Kwa nini nimetumia mfano ya maisha ya Binadamu? Hapa Duniani kila baada ya miaka 100 kizazi kipya huja, na kile kilichopo hupotea na haijalishi kama wewe ni drug dealer, hardcore criminal au Binadamu mzuri unayestahili kupewa Utakatifu lkn wote baada ya miaka 100 huenda kama vile Maji ya bahari yaoshapo mchanga ufukweni ndiyo maana Kijana aliyezaliwa mwaka 2000 don't give a shit abaout Nyerere atakwambia Nyerere ndo nini? Lkn waliozaliwa nyuma ya hapo wanamjali na mnaweza kukosana ukimuongelea vibaya Nyerere, vivyo hivyo CCM imejiwekea huo utaratibu kwamba kila baada ya miaka 10 Timu mpya huingia, na iliyopo hukabidhi na kupotea kabisa, sasa huu ni ukweli ambao Bw.Nape nafikiri unampa shida kuukubali jana alikuwa kama Mfalme akienda mahali ni kama Raisi kaingia, ukitaka Cheo Kikubwa CCM na Serikalini ni lazima umlambe miguu, ukigombana naye ndiyo mwisho wako na ajira yako itaota majani, hiyo ni power kubwa sana na leo hii ni no body sasa ni ngumu adjust kwenye maisha mapya nionavyo mimi na ndiyo maana anatoa maneno kama sijui nimepigania chama tangu Baba yangu sijui blah blah hakuna aliyepigania Chama kama Nyerere, Kawawa, Kingunge, Msuya, &Co. kama ni kuwa mtoto wa mkubwa hata Watoto wa Kawawa, Nyerere, Kingune au hata Mwinyi na Mkapa pia wanaweza kusema hivyo hivyo so no big deal, lkn wanajua kwamba muda wao umepita na wame let go!

Hivyo Nape kubali kwamba CCM iko hivyo, watakupump, watakushawishi na kukusifia lkn ukweli ni kwamba sasa hivi uwezo wako uko limited maadamu hauna mtu aliye nyuma yako ambaye anaongoza Dola, hivyo wanakudanganya tu kama siyo kukutumia!

Magufuli ataunda Timu kama vile Kikwete alivyounda yake wewe ukiwemo na siku itafika Magufuli itabidi yeye na Timu yake wakabidhi pia, na cycle kujirudia upya kama na wao wakitaka kuingilia Timu mpya yatawakuta yaliyokukuta ...

Kila La Heri Nape!

1b7e2c453b2fd5029adc694f0577caf1.jpg
6b0b3d26ec39df0186313a0432009cb6.jpg
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Nimecheka sana kwenye clip ya pili jinsi harmorapa alivokuja kwa mbwembwe af baada ya kuona bastola akala kubwa fastaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom