Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Hivi hii hiyo hoteli ya Protea mmiliki wake ni nani?
 
Wamemwaga ugali Nape akamwaga mboga......Nape toboa sufuria sasa.
thubutu yake hapo hana jipya zaidi ya blablaa akitoa chochote alichokijua kupitia uwaziri wake ambacho ni siri ya serikali amerahisisha kifungo chake tena miaka kibao...isiyozidi wala kupungua 20
 
Nape kawahiwa, laiti angeweza kujiuzulu kabla ya Rais kumtumbua angechukua point mingi sana, pengine aliweka matumaini bila kujua Bond iliyopo katikati ya Mkuu na mteule wake imekaaje!
Mkuu hapa Nape ndo kacheza kama Pelle, hichi ndo sahihi katika mantiki ya kwamba Yeye kama waziri mwenye dhamana alitenda yale yaliyopasa kutendwa, na Mkuu wake wa kazi kamfuta kazi kwa kile ambacho ni sahihi...

Angejiuzulu sana angekua kakurupuka sana
 
Pamoja na kwamba Nape katolewa kwenye uwaziri,lakini tusisahau kuwa bado ni mwanachama wa ccm.
Hawezi kupingana hadharani na mwenyekiti wake wa chama. Zaidi zaidi atawashukuru tu wanahabari kwa kufanya nao kazi. Wanaubuyu a.k.a wazee wa shilawadu naona mnasubiria kwa hamu ubuyu wa nape. HAKUNA JIPYA, NENDENI MKAOGE
 
Huyo nape anapata mashabiki wengi sababu ya kuwatetea wauza na wala ngada.
 
hii movie ya Nape ilianzia dodoma mkuu baada tu yakumaliza mkutano wa bunge, Nape akapewa kazi kwa sababu yupo ndani nyuma wapo kina Bashe na Msukuma sasa kaanzwa mmoja hao wengine wanakuja
 
Mkuu hata mtu muoga kwa miaka 10 anaejulikana hivyo, Leo ukitokea moto ghorofani akajitosa kuokoa maisha ya mtoto atageuka kuwa shujaa. Ushujaa ni kile kitendo cha mwisho unachofanya na kuondoa historia yako ya nyuma iliyokuwa mbovu
Mkuu ni mekuelewa
 
Tulia Nape Nauye maji yapowe! Hasira haijengi hata siku moja!
Hakika!! Haya mashindano ya nani ana uwezo zaidi wa matendo/maneno hayafai kabisa. Can somebody please put a stop to this CIRCUS?? 😡
 
Ninawasiwasi na maeneo anapoenda Nape kuongelea, lakini naimani bado ataendelea kuwa mwana ccm mtiifu katika chama chake. Huku nje hatapaweza, kuna kula virungu + kulala lupango, unaweza ukachanganywa na wauza ng'ada. Kiufupi vita ya huku kitaa ni ngumu, huku pia magoli ya mkono hakuna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…