Nape: Uchaguzi ukiisha wakubwa tunakaa na kumalizana ila wapambe ndio hutaka kutoana roho

Nape: Uchaguzi ukiisha wakubwa tunakaa na kumalizana ila wapambe ndio hutaka kutoana roho

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Aliyekuwa mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameandika katika akaunti yake ya twitter kuwa uchaguzi ukiisha wakubwa hukaa na kumalizana ila kazi inabaki kwa wapambe ambao hupiga mikelele kiasi cha kutaka kutoana roho.

Nape anasema " Kuna maisha baada ya Siasa hivyo tupende na kuchukia kwa kiasi"

Maendeleo hayana vyama
 
Si kweli. “Wakubwa” wanahamia kwenye ulimwengu wa kimafia (underworld”) kusaka na kutekeleza mikakati ya kuangamizana huku wakitabasamiana. Hakuna urafiki kwenye siasa za kusaka madaraka. Hicho kinachoitwa “kupatana” ni “keep your enemies closer”.
 
Huyo naye anajiona mkubwa?

Kwanza hana adabu alimtukana JPM kwenye simu anadhani JPM kasahau eh?
Kwamba chalii anajiona nae ni mkubwa,baada ya ile simu ya kusema Magu ni mshamba then mkewe kule bank nae akapigwa pini fasta tu akaambiwa tunafuatilia namna mkeo alivyopata ajira hapa.

Kajamaa kakaona bora nile matapishi tu,akatembezwa makusudi kuanzia kule getini kule ikulu huku camera zikim-record fresh.

Kajamaa kakamwambia Magu, Baba nisamehe baba Magu nae akajibu Nape ni kijana wangu nimemsamehe lkn kusamehe kunauma jamani,hahahah

Sasa kama alisamehewa kweli hilo suala jingine.
Screenshot_2020-08-17-08-16-34-1.jpg
 
Mkubwa gani unanyooshewa bastola hadharani?
Mjomba hizo hasira zako hazisaidii maana una hasira mpaka unapoteza muelekeo lazima itakua umekosa mengi sana kwenye huu utawala. Unakataa mpaka ukweli, kuna kitu gani hujakielewa hapa? Pamoja na kwamba nataka sana mabadiliko lakini siona kabisa nani wa kuleta mabadiliko. Na sipo tayari kuona tunajaribisha watu kwenye kuiongoza Tanzania (ref: Nyerere : Hatuweki watu kwa majaribio) Unaowapigia debe hawana uwezo wa kuongoza kama walivyo CCM hatutaki kufanya majaribio kama ya Zambia na Freddy Chiluba

CHUKUA LIKIZO KAMA RAFIKI YAKO JINGA LAO Maana kasifia mpaka kaona hakuna msaada kaamua kuka kimya
 
Anaposema Wakubwa hajamaanisha Mkubwa yeye....

Anamaanisha Wakubwa hao mnaowajua ninyi......

Hii ni message kwa kina Sabaya na wenzake!
 
Aliyekuwa mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameandika katika akaunti yake ya twitter kuwa uchaguzi ukiisha wakubwa hukaa na kumalizana ila kazi inabaki kwa wapambe ambao hupiga mikelele kiasi cha kutaka kutoana roho.

Nape anasema " Kuna maisha baada ya Siasa hivyo tupende na kuchukia kwa kiasi"

Maendeleo hayana vyama!
nasikia mwenyekiti wetu bado ana usongo wa kum fix huyu dogo kwa kumwita "mshamba". kiwango hiki cha dharau kilimuumiza sana mwenyekiti wetu kwa kweli.

akipita mchujo wa ubunge amshukuru mungu wake!
 
Back
Top Bottom