Napenda kujenga duka kubwa (supermarket) sasa

Yaani watu na akili zetu House gelo katuchota na kutuaminisha anauwezo kujenga na kuanzisha supermarket?
 
 
Kwenye small industry nakupa kongole, Iringa ina potential kubwa kwenye mbao lakini sioni ikitumika kikamilifu, wengi wakiwaza kuwekeza kwenye mbao basi ni kulima na kuuza mbao ghafi wakati kuna bidhaa nyingi za mbao unaweza kuzalisha na kujiingizia kipato kikubwa huku biashara yenyewe ikiwa haina ushindani mkubwa ukilinganisha na biashara nyingine

Middle class Tanzania inakua kwa speed kubwa sana, ukipata vifaa vizuri (machines/tools), mafundi wazuri wa carpentry na marketing nzuri hii ni biashara nzuri unaweza kufanya kwa mtaji mdogo sana ukachukua soko la ndani na nchi jirani!


 
Apo iite sankeykykroavask supermarket
 
Shukulove Hongera sana kwa wazo zuri. Iringa ni pazuri sana hususani Iringa mjini, kamji kadogo lakini kenye utulivu sana. Ni kweli mji hauna supermarket, cinema house, nk ni fursa nzuri kuwekeza.

Suala la biashara kulipa au kutolipa ni mpaka utakapoifanya, mchawi ni bei. Watanzania wengi tunapenda bei kitonga ndio maana watu kama kina VUNJA BEI wanazidi kutoboa, vitu bei nzuri bila kujali quality ipoje. Jenga hiyo supermarket ila uza bidhaa kwa bei poa, wengi watakuja hapo. Weka na cinema house watakuja.

Jina, weka yale yaliyokua maarufu zamani ila hayakusajiliwa popote, mfano MFALANYAKI - Kilikuwa ni kilabu maarufu cha pombe, kilikufa na jina halijatumika tena, ukiita Mfalanyaki Supermarkert au mfalanyaki store, utaibua hisia na kumbukumbu za wanairinga watamiminika na jina litazoeleka kwa kasi sana, usijali kuhusu urefu wa jina.
 
Asante
 
Yaani watu na akili zetu House gelo katuchota na kutuaminisha anauwezo kujenga na kuanzisha supermarket?
Kwanini asiweze Boss? Kuna nyumba nyingi sana nzuri zimejengwa huku bongo ukiuliza utajibiwa mwenye nayo anakaa ulaya anafanya kazi za ndani, binafsi mkoani kwangu ipo nyumba ya dada mmoja anafanya kazi za ndani CA.
 
Hapana usijenge yale mabehewa ya wapangaji wengi nyumba 1.

Jenga :mfano , nyumba moja wapangaji wawili tu, kila mpangaji ana sebula,chumba jiko na choo chake.

Kama eneo linatosha pembeni weka vyumba vya" self contained " hata viwili.

Kwenye supermarket huko jipange utafute maarifa na ujuzi wa ku dela na watu kama cashier, walinzi, uelewa kuhusu stock, marketing, customer service/care muhimu sana .. yani wewe ukiwa kama owner inabidi uwe na skills nyingi na ufahamu wa hayo mambo jinsi yanavyokwenda tofauti na hapo uatfute manager atakeye simamia (jambo ambalo sishauti sana ) labda kama mtafanya kazi nega kwa bega
 
Yaani watu na akili zetu House gelo katuchota na kutuaminisha anauwezo kujenga na kuanzisha supermarket?
Sioni kama ni jambo la ajabu sana hata lisiwezekane, nina rafiki yangu ana dada yake yupo nje kwa kazi za ndani ndio analisha familia,

Nina rafiki aliyesoma bagamoyo chuo cha sana baada ya kumalza f4 , now yupo US hata chuo hakumaliza anacheza ngoma na kuendesha bicycle "bmx rider" amejengea wazazi na yeye kashamaliza nyumba yake!
 
Hapana usijenge yale mabehewa ya wapangaji wengi nyumba 1.

Jenga :mfano , nyumba moja wapangaji wawili tu, kila mpangaji ana sebula,chumba jiko na choo chake.

Kama eneo linatosha pembeni weka vyumba vya" self contained " hata viwili.
 
Asante
Asante kwa ushauri
 
Cc Nguli Allen Kilewella mkaribishe muwekezaji
Hili jambo liko kinadharia zaidi maana uhalisia unalikataa. Wazo ni sahihi ila wakati na mahali si sahihi. Mji wetu bado uko kwenye viwango vya maduka ya kawaida. watu wetu hawajawa na uwezo wa kununua vitu kwenye "super Market" kubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…