Shukulove Hongera sana kwa wazo zuri. Iringa ni pazuri sana hususani Iringa mjini, kamji kadogo lakini kenye utulivu sana. Ni kweli mji hauna supermarket, cinema house, nk ni fursa nzuri kuwekeza.
Suala la biashara kulipa au kutolipa ni mpaka utakapoifanya, mchawi ni bei. Watanzania wengi tunapenda bei kitonga ndio maana watu kama kina VUNJA BEI wanazidi kutoboa, vitu bei nzuri bila kujali quality ipoje. Jenga hiyo supermarket ila uza bidhaa kwa bei poa, wengi watakuja hapo. Weka na cinema house watakuja.
Jina, weka yale yaliyokua maarufu zamani ila hayakusajiliwa popote, mfano MFALANYAKI - Kilikuwa ni kilabu maarufu cha pombe, kilikufa na jina halijatumika tena, ukiita Mfalanyaki Supermarkert au mfalanyaki store, utaibua hisia na kumbukumbu za wanairinga watamiminika na jina litazoeleka kwa kasi sana, usijali kuhusu urefu wa jina.