Napenda kujua zaidi kuhusu Kilimo cha minazi (coconut tree)

..niliuliza kwasababu nataka kuibananisha eneo langu ni dogo.
Kama ni hivyo isipungue meta nane kati ya mti na mti. Ili ufanye kilimo chenye tija jitahidi uwe na walau minazi 300 hapo utaona faida yake.
 
Haya majibu mbona mnafanya kilimo kwa hovyo hivi?

Nafasi ya minazi wastani ni 7.5mx7.5 kwa aina zote yaani chotara na ya kiafrika yaani EAST AFRICAN TALL VARIETY (EATV).

Chotara ni nazi za kipemba na zimepatikana baada ya kuchanganya aina mbili ili kufanya mbadala wa F1 iliyofeli.

EATV ina Species nyingi sana kama Ng'apa nazi ya kusini nzuri kwa harufu katika tui lake,kuna Pangani nazi nzuri ya Pwani ya mashariki kaskazi,Kuna nazi ya Mafia ambayo inatambulisha ukanda wa kusini mwa jiji la Dar es salaam,kuna Mkuyuni nazi inayotambulisha mkoa wa Morogoro bila kusahau Bagamoyo. Kuna kimtang'ata nisije kuhojiwa mbele pia.

Nazi chotara ni miaka mi4 na ile ya kiafrika ni miaka 5-7.


Kwa maswali na changamoto katika zao la minazi na hata miche tuwasiliane 0714600575.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…