Napenda sana mtoto, lakini najua mtoto si wangu. Ila mdada analeta ghasia. Nifanyeje? Nipo Marekani kwa sasa. Naomba ushauri

Napenda sana mtoto, lakini najua mtoto si wangu. Ila mdada analeta ghasia. Nifanyeje? Nipo Marekani kwa sasa. Naomba ushauri

Tulipima mkojo mara ya kwanza akakutwa hana mimba. Akalalamika kwamba jamani mbona juzi tu nilikuwa na mimba nimepimwa, Basi wakarudia. Ndio ikaonekana ana mimba. Basi nikaenda laboratory ya uhakika kabisa arusha. Wakasema kabla ya damu, tufanye mkojo, ndio akawa anazingua hataki kutoa sample. Baada ya kuzingua sana nikamsachi nikakuta ameficha hicho kichupa. Na yeye kipindi hicho alikubali kwamba amedanganya na kuomba msamaha. Baada ya muda ndio akaja na hio gear nyingine. Damu ilikuwa tupime lakini baada ya kumwona ana kichupa nikaona hakuna sababu.
Inaonekana alikuwa anapigana juu chini ili ionekane ana ujauzito wako. Pole mkuu kwa hilo maana uliingia sehemu sio
 
Iko hivi:
1. kama ni wako, usikimbie damu.
2. Kama ni wa mwenzako, kitanda hakizai haramu.

Either way,ni wajibuwako kulea mtoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
Napenda watoto, na angekuwa mkweli na kama asingekuwa tapeli, ningemsaidia. Mbona ninasaidia wa wengine? Huyo mdada ni kwamba sitaki kabisa mazoea naye na sababu hatuna hata mtoto, sikutaka anizoee ni kamanibilisi kabisa. Ila yeye anatafuta tu njia za kuwa karibu na mimi. Na sasa hivi ndio hii ameamua.
 
Umekosea kumuanika huyo mtoto mtandaoni....haki ya faragha. Na hata huyo mdada sidhani kama kulikuwa na ulazima sana wa kumuweka public.

Ungeweza kuandika thread bila ku-reveal identities zao.
 
Umekosea kumuanika huyo mtoto mtandaoni....haki ya faragha. Na hata huyo mdada sidhani kama kulikuwa na ulazima sana wa kumuweka public.

Ungeweza kuandika thread bila ku-reveal identities zao.
Yeye si amenianika sana kwa ndugu zangu na kwa wafanyakazi wangu? Kwa jambo ambalo anajua ni utapeli? Na ametumia hizo videos? Na mzazi wa huyo mtoto amekubali atumike? Utakuta ndio wa yule mama aliyempatia mkojo atumie kwa kipimo. Wote ni matapeli tu na mkono wa sheria utawashukia. Nimeshachoka na abuses zao mimi. Ngoja tu.
 
Naweka beti kwamba kama ni mtoto wake, na hata kama ni wa jamaa mwingine. Kama ni mtoto wake tu yeye wa kumzaa NITAMLIPA YEYE MILIONI 5, NA FAMILIA YAKE MILIONI 5. Naweka bet hii sababu najua sio mtoto wake, na pia najua mimi na yeye hatuna mtoto.
Ili upate peace of mind, solution yake ni very simple. Nunua DNA test kit huko USA mtumie ndugu yako wa karibu achukue mouth swabs za huyo mtoto halafu akutumie. Baada ya kuzipata unachanganya na mouth swabs za kwako unatuma DNA lab.
 
Ajiri mtu Tanzania kwa kazi maalum ya kumchunguza... Unaweza uka finance hata jamaa adate naye lakini wakati huohuo ukimtafutia shoga wa kike kwa nia hiyo hiyo... Mwezi ni mkubwa utapata kila kitu
Wadau Yamenikuta. Sitaki kuandika story ndefu sana. Lakini huyu mdada nilikutana naye nilivyokuja Tanzania na alinifanyia vituko ambavyo kwa kweli siwezi kuviandika hapa. Tokea nimwache amekuwa ni ghasia kweli. Nilishapima mimba naye na nikamkuta ameficha mkojo kwenye nguo ya ndani sababu matokeo yalikuwa negative kwa mimba mara positive ndio mtu akasema nimsachi. Sasa anatuma picha kwa ndugu zangu anasema nimemtekeza mtoto. Mimi kwa sasa sipo Tz niko abroad kwa hio hata DNA siwezi fanya. Ila amekuwa ghasia sana. Kuna picha amenitumia NAOMBA KAMA KUNA ANYEJUA HUYO NI MTOTO WA NANI ANIAMBIE SABABU MIMI NAJUA HUYO mdada amechukua tu mtoto wa mtu anapiga picha naye. Muda aliosema amezaa mahesabu yanakataa. Na kama nilivyosema, nilipima mwezi mmoja baada ya kuwa naye mara ya mwisho akakutwa hana, akalalamika akaomba warudie vipimo, akakutwa ana mimba. Basi ndio nilivyomsachi, nikakuta ana hicho kichupa amekificha kilichokua na mkojo. Ni mdada mrembo, lakini urembo bila roho ni kazi bure.

Picha zake na ya mtoto hizi hapa. Najua huyu ni mtoto wa mtu Fulani. Naomba mnisaidie sababu ghasia zake zimezidi kwa kweli na mimi mwaka jana niliacha kazi zangu USA nikanunua tiketi ya mamilioni nikaacha shughuli zangu nikarudi Tz kushughulikia ghasia zake za mimba za uongo, na sasa sitaki KUFANYA HIVYO tena. Naomba msaada wenu wadau.

PS: Napenda sana mtoto. Ila sijajaliwa bado sababu sijapata mke bado. Ndio wadada nakutana nao kama huyu ni utapeli mtupu. Ila hata sasa hivi nasomesha Watoto watatu wa marafiki tu, kwa hio sio kwamba sina uwezo wa kumsaidia. Lakini sitaki kumsaidia mtu tapeli. Na kama nilivyosema najua hata huyo mtoto sio wake. Namba hazikubali kabisa.
View attachment 1341634

VIDEO HII HAPA
View attachment 1341657




View attachment 1341631

View attachment 1341632View attachment 1341633

Jr[emoji769]
 
Wenzangu tujitahidi kutumia kondomu kwenye mapito (najua ugumu wake, lakini inawezekana). Kuna wanawake wajanja sana, ukiingia kwenye gemu nae pekua ni kama umempa "blank cheque" kiaina.
 
Kaka hapo uliingia mkenge....ukimwangalia vizuri huyo mwanamke ana vigezo vyote vya ubaharia a.k.a chama la wana....Ninachokushauri mpotezee tu,waambie na ndugu zako ukweli wampuuze tu ashakuona unatingishika ndo maana anakutingisha.

NB😛unguza hizo USA kwenye maelezo mkuu,unatuumiza moyo sisi masikini tusio na hatia.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji3] [emoji3] [emoji3]
Kwa kweli "anatuumiza masikini"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani ukimpotezea utakufa au???? Acha kujipa stress za ovyooo...!! Mwanamke analeta utapeli kama uo alafu na wewe unatapatapa????

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimempotezea sana kwa karibu miaka miwili nikijua atanisahau. Ila hajaacha kamwe kuwa msumbufu. Anataka sana turudiane na anatumia upuuzi kama huu hajui mimi ndio inafanya nimchukie zaidi. Sasa hivi anakuwa tatizo kwangu, kwa biashara tz, kwa ndugu na kila kitu.
 
Sasa c uzae nae kikweli kweli hiyo ndo itakuwa dawa ya kuacha GHASIA huku TZ na wewe utaendelea na maisha yako huko US
 
Wenzangu tujitahidi kutumia kondomu kwenye mapito (najua ugumu wake, lakini inawezekana). Kuna wanawake wajanja sana, ukiingia kwenye gemu nae pekua ni kama umempa "blank cheque" kiaina.
Tatizo alikuwa ni mchumba. Kwa hio tulikuwa na uhusiano mkubwa na hadi kwao walishanifahamu na pete ya uchumba nilimvisha. Nilimwacha nilivyosafiri hata mwezi haujaisha akanisaliti. Asante Mungu kuniokoa. Niliingia mkenge mahali sio. Japo Mungu ndio kweli alininasua. Hawa ndio wanawake ukimwoa hata anakuondoa kabisa duniani.
 
Sasa c uzae nae kikweli kweli hiyo ndo itakuwa dawa ya kuacha GHASIA huku TZ na wewe utaendelea na maisha yako huko US
Ndugu yangu huyo sitaki kuwa na mtoto naye. Ni ghasia sana. Nashukuru Mungu haikuwa hivyo.
 
Back
Top Bottom