Niulize haya maswali.
1. Mara ya Kwanza alivyopimwa na kukuta Hana, huyo tabibu alipima maji au mkojo wa huyo mwanamke?
2. Kama Ni mkojo ulipimwa je, hii kupima Mara ya pili mlipima mkojo wake au mkojo wa Nani na Kama Ni wake Ni ya Nini kumsachi wakati tayari mlishapima mkojo wake Mara ya Kwanza?
Ilikuwa hivi mkuu. Nilivyotaka kumwacha baada ya usaliti wake wakati bado niko nje ya nchi (ndio nilikuwa nimeondoka tu Tz hata wiki 2 hazijaisha), alidai ana mimba yangu akijua hiyo itafanya nisimwache. Wakati bado niko nje, nikamwambia akapime. Ila akasindikizwa na mtu wangu wa karibu. Huyo mtu wa karibu nikamwambia achukue namba ya doctor. Basi msichana huyo ex wangu akasema anayo. Doctor akasema hana nilivyopiga simu.
Nikarudi Tz sababu alisababisha matatizo mengine ilibidi nirudi kusawazisha. Nilivyorudi ndio tukaenda kupima sasa.
Mara ya kwanza kupima mimi na yeye, kipimo kikaja hana mimba. Alitumia mkojo. Akawalalamikia hao watu kwamba sio kweli anaomba arudie tena. Wakamruhusu. Kipimo cha kurudia wakasems anayo. Mimi nikasema amekula njama na hao watu. Inakuwaje vipimo viwili tofauti lab hio hio?
Basi tukaenda lab nyingine kali zaidi nikamweleza doctor vipimo vilivyokuja tofauti. Akasema sasa msimamie akikojoa.
Demu akakataa nisiingine chooni naye. Nikashsngaa sababu hakuna nisichokijua kwake. Akasema hajisikii kufanya mkojo. Nikamnunulia maji ya kilimanjaro 2. Chupa kubwa na ndogo ili ajisikie ila akawa bado eti hajisikii kukojoa. Nikala naye bumper to bumper sababu kuna muda alikuwa anataka kwenda kichakani unaona kabisa huyu amebanwa. Ila ndio hivyo hakutaka kukojoa mbele yangu sababu akikojoa, nitataka hio sample tukaipime, na yeye kumbe alikuwa ana mipango mingine na hiyo sample ya uongo.
Baada ya masaa mawili ya kuzingua na kutotaka kutoa mkojo wa sample wa kusimamiwa, ndio nikahisi kitu. Nikasema huyu itakuwa labda ana mkojo ameficha. Hisia zilinituma hapo baada ya uzinguzi wake masaa mawili, vipimo tofauti, hataki niingie naye chooni, maji amekunywa mengi, bado eti hajisikii, na unaona anajibana miguu amebanwa, basi nikasema wewe nakusachi. Nilivyomsachi kwa nguvu, ndio nikakuta hicho kichupa amekificha chenye mkojo. Yani hasira zangu hapo acha tu.
Hii ndio ilikuwa hivyo ila sikutaka kuandika mambo marefu sana kwenye post original