Napendekeza bidhaa zipigwe kodi mara moja tu, njia ni hii

Changamoto hizi zitafutiwe suluhu
 
Tupunguziane milolongo katika ulipaji wa kodi, process zimekuwa nyingi
 
Tukifanya miamala inayohisisha bidhaa tunatakiwa kulipa tena kodi, 🤷🏽‍♂️
 
 
Andiko limeshiba sana
 
Andiko limeshiba sana
Mfumo huu ukitumika, naamini utachaguza sana ukuaji na ustawi wa biashara nchini, pamoja na kuongeza mapato kwa uhaki zaidi, kodi iongezwe ila ilipwe yote infull kwa mara moja pale pale kiwandani / Bandarini.
 
Haileti mantiki kodi ya shs. 10/= itumike gharama ya shs.7/= kuikusanya, hii haiingii akili!
 
Unastahili kuwa think tank ya taifa lakn kwa sabab we sio muimba mapambio hawawez kukuteua
 
Uzuri wa sheria ya mapato iko wazi kwa wakwepa kodi, atawajibishwa kwa mujibu wa sheria zetu za kodi
 
 
Mtoa hoja nakuunga mkono mtiririko wa kodi Tanzania unasababisha bei za bidhaa zetu kuwa kubwa sana na kuongeza gharama za maisha. Sijui kama wataalam wetu wamewahi kujiuliza jinsi gani hili jambo linatuletea hasara. Tanzania tumebarikiwa kuwa na bandari, bidhaa nyingi za nchi zinazotuzunguka zinapitia kwetu lakini bidhaa hizo hizo zikifika nchi za jirani zinapokwenda bei yake huwa rahisi kuliko hapa kwetu. Yaani wafanyabiashara wa kitanzania wanalazimika kwenda Uganda kuchukua mzigo na kuleta Tanzania, hivi hatuoni kuwa tunapoteza?

Kama tungekuwa tunafikiria vizuri tulipaswa kutengeneza mazingira wafanyabiashara wa nchi zinazotuzunguka Rwanda, Burundi, Zambia, Uganda & DRC wawe wanakuja kufunga mizigo hapa kwetu. Yaani ilitakiwa mtu akipiga hesabu kwa mzigo wa kawaida kwenda China, Dubai au Tanzania apate jibu bora niende Tanzania. Lengo hili hatuwezi kulifikia kwa aina ya kodi tulizokuwa nazo. Kwanza kodi zetu zinashawishi ukwepaji, yaani mfanyabiashara anashawishika kukwepa ili apate faida. Ni ukweli uliodhahiri mfanyabishara mdogo au wa kati akifuata masharti yooote na kodi zoooote za kibongo hawezi kutoboa. Hivyo, wanalazimika kukwepa kwa kutumia mbinu za kila aina.

Huwa najiuliza mfanyabiashara hata wa mtaani akifikia aina fulani ya mauzo anatakiwa kuandikishwa katika VAT kwahiyo bidhaa zake anatakiwa kuanza kuongeza 18%, wakati huo huo jirani zake ambao bado hawajafikia kiwango cha mauzo yake wanauza bidhaa ya aina hiyo bila 18%, kwa maana hii yeye hawezi kuuza tena akiendelea kuweka hiyo kodi. Sasa mfanyabiashara huyu unafikiri atakubali? Lazima atatafuta namna ya kuikwepa hii kodi ili aendelee ku-survive. Yaani kodi inamrudisha mtu nyuma hii sio sawa. Kodi ya VAT ilipaswa kuwekwa viwandani ili wanaokwenda kununua wakutane nayo hapo au kwa wafanyabiashara wakubwa wanaoagiza mizigo kutoka nje tu, na ipigwe pale mzigo unapoingia tu. Hawa wafanyabiashara wengine wapigwe kodi ya mapato pekee yake.
 
V8 na matumizi ya hovyo ya wanasiasa yatatoka wapi wasipoendeleza mfumo wa kodi wa kiwizi na unyang'anyi?
 
Nilikua na haya mawazo toka siku nyingi mpaka nikasema uongozi unahitaji mtu ambaye ameshapitia kwenye biashara akapambana na marejesho ya benki, return n.k. Ila kama hujawahi kufanya biashara huwezi kuelewa kadhia.

Na pia anayepewa huu mzigo wa kodi ni yule mwananchi mtumiaji wa mwisho anayepokeaga khanga na kitenge wakati wa uchaguzi.
 
Hii ni moja ya comment bora nilizowahi kuziona JF toka nimejiunga 2013
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…