Akizungumza na Wafanyabiashara wenzake wa Kariakoo, Ndugu Mbwana ambaye anatajwa kama kiongozi wa wafanyabiashara hao amewaasa Wafanyabiashara wote wafungue maduka yao kwa vile Waziri Mkuu alielekeza hivyo na kwamba Jumatano kutakuwa na Kikao kati ya Viongozi wa wafanyabiashara na Waziri Mkuu...
TRA Tanzania
Tanzania tuna mfumo wa kodi ambao naweza kuuita ni 'Tax chain system'. Yaani ni kwamba bidhaa moja inaweza ikapigwa kodi hata mara kumi halafu wale watu walioilipia kodi mara ya 2 hadi ya 10 wanatakiwa wapeleke mahesabu TRA ili warudishiwe kodi yao;kivipi?
Mfano bidhaa imezalishwa kiwandani, mnunuzi wa kwanza atakayenunua atalipa 18% Vat, na hii tu ndio halali ya TRA kwa bidhaa hiyo, lakini kama huyu mnunuzi wa kwanza ataenda kuiuza itabidi atoe risiti ya EFD na atamlipisha tena mteja 18% Vat ambayo TRA itamdai, huyu nae akienda kuiuza itabidi atoe risiti ya EFD ambapo atamchaji tena mteja 18% VAT ambayo nayo itatakiwa kupelekwa TRA, and so on hata mara 10.
Ili kuepuka kulipa VAT mara mbili kila mfanyabiashara atapeleka mahesabu na risiti za VAT (kwa waliounganishwa na VAT) ili kujua kiwango cha ziada cha kile ambacho ameshalipa, na hicho tu ndicho atapaswa kulipa; hii process inaleta mlolongo mgumu na very complicated, yaani ni mfumo mgumu sana bila sababu, nadhani wote mnofuatilia haya masuala mtajua.
Lengo la TRA kung'ang'ania huu mfumo ni ili kupata 18% ya faida ya kila hatua ya uuzaji wa bidhaa, hata ikiuzwa mara 10 TRA hawajali, wanataka 18% ya ile faida (gross profit) ya kila mfanyabiashara katika kila chain link ya uuzaji wa bidhaa husika, hadi kwa final consumer, yule wa mwisho kabisa. (Wanakaba hadi penalti).
Hii inaweza kuonekana ni nzuri ukiitazama kwa juu juu, lakini in reality hii ni sawa na kutumia risasi kuwinda smaki baharini, unatumia 10shs. kukusanya shs.8, yeees, ukweli ndio huu. Badala ya kusababisha such an expensive practical complexity ni kwanini TRA isiwekeze instead kuhakikisha kodi yote ya kila bidhaa inalipwa palepale kiwandani bidhaa inapozalishwa au bandarini mzigo unapoingizwa, hata kama kodi ikiongezwa sio mbaya lakini ilipwe yote infull palepale kiwandani / bandarini.
Hebu fikiria tu harassment wanayopata wateja wanaposafirisha mizigo barabarani, watu husimamishwa hovyo hovyo na mapolisi 'Tigo' wale wenye silaha za kivita as if wanasimamisha jambazi, kumbe umebeba T.V tu ndio imekuwa nongwa, kwani hii T.V si imepitia bandarini??! Si mchukue kodi yenu yote huko huko muache wananchi waishi kwa amani?
Mateso kama haya walikuwa wanayapata wamiliki wa magari ambapo kila mwaka walipanga foleni TRA na office za MXMALIPO kulipia road license, tena barabarani TRA walipoteza nguvu kazi kubwa ya wasomi wenye madegree kusimamabarabarani eti kukagua sticker za road license, as if hizo gari hazitumii mafuta ambayo tayari yana kodi lukuki, binafsi nilianzisha uzi wa kupendekeza kodi hiyo nayo iunganishwe tu humo humo kwenye mafuta(Hivi ni kwanini road license isilipiwe kwenye mafuta?) watu waligoma goma ili mwishowe logic and common sense emerged victourious, serikali ikahamishia kodi hiyo kwenye mafuta na sasa hii kero imeisha
Muda mwingine umasikini tunajitafutia wenyewe kwa kukariri vitu vilivyopitwa na wakati, technolojia imekuwa, ni rahisi sana kukata kodi yote in full kwenye viwanda / bandarini, tubadilike bwana; nakaribisha maoni.
=================================
Update: 04/04/2021
Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba, amesema wanaangalia namna ya kutumia mfumo mpya wa ukusanyaji kodi
Mama Samiah ana lipi la kutuambia juu ya kauli yake kwamba akipata nafasi ya kukopa atakopa tena. Tumsikilize mwamba akiwafundisha wanafunzi wake, na endapo Rais wetu anaweza kuirudia ile kauli yake juu ya mikopo? ================================ Update: 15/02/2022...
Kuna tetesi ya mgomo wa wafanyabiashara eneo la Kariakoo. Sababu za kuitisha mgomo; 1. Urasimu bandarini 2. Usajili wa stoo 3. Kamata kamata hovyo ya wateja kwa ukuguzi wa risiti Wao wapo tayari kufanya biashara kwa uhuru na kulipa kodi bila mambo ya rushwa rushwa na maonezi. Rai kwa...
Hakuna mfanyabiashara anayelipa VAT,bali hulipwa na mtumiaji wa mwisho!!Mfanya biashara yeye ana kuwa ni mkusanyaji tu wa hiyo kodi na kuiwakilisha serikalini.Na ndio maana sio kila mfanyabiashara ana sifa za kuwa mkusanyaji wa kodi hiyo.Ugomvi unaanzia kwenye bidhaa una pata faida yako,halafu hutaki kutoa risiti ya EFD,na hiyo 18% uliyokusanya kwa mlaji badala ya kuiwakilisha TRAnayo unaitaka tena!!???
Hakuna mfanyabiashara anayelipa VAT,bali hulipwa na mtumiaji wa mwisho!!Mfanya biashara yeye ana kuwa ni mkusanyaji tu wa hiyo kodi na kuiwakilisha serikalini.Na ndio maana sio kila mfanyabiashara ana sifa za kuwa mkusanyaji wa kodi hiyo.Ugomvi unaanzia kwenye bidhaa una pata faida yako,halafu hutaki kutoa risiti ya EFD,na hiyo 18% uliyokusanya kwa mlaji badala ya kuiwakilisha TRAnayo unaitaka tena!!???
Sina hakika kama umeelewa hoja yangu juu ya mfumo kuleta mlolongo mkubwa na wa gharama bila sababu. Maana hayo unayosema ndio nami nimeyasema na hakuna aliyebisha.
Mfumo ninaopendekeza utahakikisha watu hawakwepi kodi, maana hapatakuwa tena na haja ya kutegemea utoaji risiti ili kukusanya kodi za bidhaa.
Hali kadhalika biashara zitafanyika bila bughudha toka kwa vijana njaa njaa mitaani wanaokamata mizigo, kiujumla gharama za ufanyaji biashara zitashuka sana na kuchagiza ukuaji wa uchumi.
Halafu kingine, kwanini unajibu hoja nzito kwa pupa kama nguruwe kafunguliwa bandani? Tuliza akili na uchangie mada kwa mantiki huku ukizingatia hoja tajwa.
VAT YA 18% ni kubwa sana na imekaa muda mrefu. Ukiwauliza watu wa TRA wanasema hawawezi kushuhsha sababu ya walipaji ni wachache, na wachache hao wengine ni wadanganyifu. Nafikiri serikali asilimia ya ikipungua unaongeza wigo wa watu kulipa VAT, sababu wanaona ni kiasi si kikubwa. Hii 18%...
Yule Mwamba anayekubaliwa na wengi kwa kupigania Haki za Watu woote bila kujali misingi yao ya kiitikadi ametoa ushauri wake kuhusu sakata la Kariakoo na Wafanya biashara. Huyo Champion wa siasa za Bongo ameeleza pia nini kinaendelea na kusema kuwa chanzo kikubwa ni Katiba Ya Sasa ambayo imempa...
Sawa, ila kodi yote ilipwe pale pale Kiwandani au bandarini, hata akiweka Vat 50% sawa, ila ilipwe yote hapohapo kwenye source, huku mtaani wananchi tufanye biashara kwa uhuru bila bughudha, sisi sio wakimbizi!
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo, leo Mei 17, 2023. Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo wametoa malalamiko mbele ya Waziri Mkuu ambapo wameilaimu TRA kwa kutokufuata taratibu sahihi za...
Kikao cha wafanyabiashara wa Kariakoo , wawakilishi mikoani na waziri mkuu kimeibua uozo na mengine mazito na magumu wanayopotia wafanyabiashara wa Tanzania.. Kikao kimeisha salama kwa kukubalika kwa hoja karibia zote zilizoibuliwa na wafanyabiashara.. Furaha imetamalaki wazi kwenye nyuso zao...
Tatizo ni Bunge kutunga sheria mbovu za kodi. Lkn lenyewe limekaa kimya kama halihusiki. Na wadau nao wamekaa kimya hata hawajadili. Pale Naibu Speaker alipaswa kupopolewa mno lkn aaahhh wapi
Mimi ni mnunuzi bidhaa mbalimbali hapo kariakoo ukweli ni kwamba asilimia 90 ya wafanyabiara hawatoi risiti halali yani ukinunua mzigo wa mil 1 unapewa risiti ya laki 5 wafanyabiasha wa wahindi wao watakuomba wakutolee risiti ya laki 7 wanaouza bidhaa bila risiti ni asilimia 1 wanaotoa risiti...
Mgomo wa Kariakoo umeibua mengi. Lakini pamoja na kuonyesha madudu ya uncontrollable TRA na rushwa za nje nje zilizoishinda serikali kuzikabili, mgomo umeibua jambo serious la utendaji chini ya kiwango wa mawaziri wa Fedha na Mipango, pamoja na yule wa Biashara na Viwanda. Wiazara hizi lazima...
Ukiskiliza malalamiko mengi ya wafanyabiashara wanazungumzia kamatakamata ya TRA na polisi katika mizigo, faini kubwa kwa kutotoa risiti za mauzo na TRA kudai rushwa kutokana na mambo haya. Hapa kiini cha tatizo ni VAT na kodi nyingine za bandarini. Serikali anzeni kwa kufanya VAT ilipewe na...
Mamlaka za kodi ni "polisi wa mapato" inachukua halali ya serikali, na kawaida, ni jbo gumu kwenda kuchukua kwa mtu fedha yake, lazima alalamike. Wanachofanya TRA kukusanywa mapato, hata halmashauri, kinafanyika Dunia nzima, na mamlaka za kodi duniani kote, hazijawahi "kupendwa". Ukiona...
Hapa ndipo waandishi wa habari za uchunguzi wanatakiwa kuingia "chimbo". Wakawasake hao wafanyabiashara wa nchi jirani wawahoji. Lakini, kinachoonekana wafanyabiashara wa kariakoo ndio wameiua kariakoo yao. TRA hawawezi kuhangaika na aliyelipa Kodi halali, wanashughulika na wakwepa Kodi...
Nauliza tu ndugu zangu Wasomi wa Political Economy Ni kweli kabisa Uchumi wa Tanzania unategemea Soko la Kimataifa Kariakoo? Yaani wale jamaa wa Mkutano wa juzi ndio tegemeo la Taifa? Nimekaa pale nasubiri majibu Jumaa kareem!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.