Napendekeza dunia iwe na nchi moja tu ya ‘United states of Earth’ (USE). Raia wa kigeni ni yule wa kutoka sayari nyingine tu

Mnataka kuchafua jamii za watu zilizostaarabika.
 
Ustake ncheke kwa kejeli !! Wenzako walishaliseti siku nyingi, muda si mrefu utasikia serikali moja ya dunia, dini moja, uchumi mmoja sarafu moja, rais mmoja, na mabara yatagawanywa mfano wa majimbo.
Na mafisadi ya CCM sasa itakuwaje? yataporaje mali za umma?
 
Kwa nini unataka iwe hivyo?
 
Kama hujavuta bangi basi usije ukavuta. Manake hujavuta tu upo hivi ukivuta je?
 
Wewe kama nani unapendekeza? Watu wajinga kama Makolo uwaruhusu kwenda nchi yoyote bure bure si itakuwa shida sana, au wavaa kobazi.
 
FRANCIS DA DON na Bob Manson huwa mnawaza vitu vikubwa mnauliza maswali magumu magumu

Mimi nadhani hilo jambo linawezekana huko mbele sana tukishaendelea kwa viwango vikubwa na tukawa tunaishi kwenye sayari nyingi

Tutakuwa kama waingereza walivyokuwa na ile British Colonial Empire

Lakini kwa sasa bado sana, tuna mambo kama ukabila, mifumo mibovu kama uchumi na dunia ina rasilimali chache, watu lazima wagombanie

Kumbuka tumekaa hapa duniani kwa miaka kama laki moja tu, tuna nafasi ya kufanya mambo makubwa bado
 
Daydreamer
Ni jambo gumu kwa hilo jambo.
Tuassume Western world au kwa Sasa ni global North watataka kupitia their muscles in finance, military au ideology ya aina yoyote.

Hawawezi kutoboa kwa sababu moja tu, watawezaje kuzishawishi Urusi na China kukubali hiyo proposal !?

Kinachowezekana ni kuwa na zone of Control tu ambayo ilishawahi kutokewa.
1.Urusi
Watawale Eastern Europe, Central Asia na Pacific area.

2.China
Hawa wavimba macho waachiwe Indochina yote, na visiwa vyote ule upande.

Jumlisha na baadhi ya visiwa kule kwenye bara la Australia.

3.USA
Tuwaachie bara lote la Amerika iwe ya kusini au ya kaskazini, ataamua mwenyewe awafanyeje.

4.Middle East tuwaachie Turkiye, Iran na Saudia.
Hapa kitawaka ila dominance wataamua wenyewe.

5.Western Europe wataamua wenye we watataka wawe World player au kuwa dominated na German/France au UK?

6.Afrika
Kuna regional player kama South Africa, Egypt, Nigeria na Tz/Kenya.

Tudadavuane mpaka tutakapo establish our own powers.

Ila ukweli haiwezekani, Geopolitics sio rahisi kama tunavyofikiri.
 
Ao raia w kigeni ndo wanaendeaha this world Kwa kushirikiana na devil
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…