Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

Napendekeza iundwe Tume Huru ya kuchunguza kifo cha Hayati Magufuli

Kwaio ukikutwa na ela zimejaa chumban kwako bas moja kwa moja wew ni mwizi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sheria inakataza kuwa na zaidi ya mil.10 ndani..

Unaiba Pesa👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220719-125637.png
    Screenshot_20220719-125637.png
    175.3 KB · Views: 5
  • Screenshot_20220719-125655.png
    Screenshot_20220719-125655.png
    49.3 KB · Views: 4
Habar watanzania lengo langu la kuanzisha huu uzi si kwa Nia Mbaya ila nikutaka tu Kumaliza Maswali ya Watanzania wengi wanao shuku kua Hayat kafanyiwa hujuma.

Baada ya kuona mambo mengi Yanayo endelea kwenye mitandao ya kijamii na mitaani. ni wazi kabisa Baadh ya watanzania walio wengi Wana shuku kifo cha Hayat Magufuli na kudhan kua kifo chake kina Hujuma.

Serikal iheshimu mawazo ya watanzania tunao tilia shaka kifo cha Rais wetu na izingatie kwa kuunda Tume huru ya uchunguzi.

Mimi Binafsi nikikumbuka Tukio la ule Moshi uliomfata Hayat Magufuli Mtwara alipokua kwenye Gari bila kujulikana wapi umetokea na kuzua Taharuki nazid kua na mashaka kua Huenda zile zilikua baadhi ya mbinu za kutaka kujaribu na zilishindwa Lakini waliojaribu hawakuacha.

Pia wasiwas wetu unakua mwingi baada ya Habari kua nyingi za magufuli kafarik kabla hata ya serikal kutangaza huku picha za Gar la mait ambalo lilibeba mwili kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii

Kwanini Kina Tundulisu na kigogo walikua wanapata taarifa na walikua na uhakika kabisa kua mzee lazima afe na asipo na wengine kusema kabisa mzee kafa

Kwanini kifo chake walikitangaza Adui zake uku wakisherekea ushind

Kwanini kabla Magufuli yupo Hai viongoz walianguka kama kuku Tena wa karibu yake ila baada ya yeye kufa Hamna kiongoz hata mmoja alie kufa?

Huwezi kusema ule ulikua uchawi sababu hakuna uchawi na wala siamini uchawi kama upo.

Sasa ili kujiridhisha Basi serikal ifanye uchunguzi na uchunguzi uwe wa wazi ili kufuta hii shauku ya Baadhi ya watu kwani ikiendelea ivi na serikal kukaa kimia huwezi jua Baadaye itakua na madhara gani pia huto jua maadui baadae wanaweza kuutumia huu uvumi kama silaha so nibora serikal ilimalize kwanza ili swala kwani kila siku mambo yanazid kupamba moto.

Video ya tukio la moshi hio apo chini.


heshima kitu cha bure, acha
 
Kwa kadri mambo yanavyoenda nashauri uwepo uchunguzi huru. Inawezekana tukawa tunamchukia Magufuli lakini tukiacha wawepo watu ambao wanaweza muondoa Rais madarakani kwa njia hiyo.

Basi tufahamu hatupo salama na hatutakuwa salama. Leo hii tunaweza furahi au kasirika lakini tuangalie siku zijazo. Nadhani ili watu wawe na amani inapaswa kuwepo Tume Huru ya mchanganyiko, watu ithibitishe kilichomuua Dr. Magufuli ni nini, kisha maisha yaendelee.

Lakini tuangalie sana ikiwa kunaweza kukawa na jamii fulani inataka watu wake tu ndiyo watawale, basi tusijedhani tutakuja kuwa salama au kuendelea nchini. Haijalishi dini na kabila zetu, haijalishi vyama vyetu.
uanze wa kitendo kumuua Lissu alafu ndio uje uo wako sasa, sawa sawa? nakuuliza tena sawasawa?
 
Hao mnaotaka wachunguze kifo chake unadhani hawakujua tabia zake alipokuwa kwenye hicho cheo? Au kwakuwa watu wanatunza siri, basi unadhani wana huo muda wa kuchunguza kifo chake?
Bado unazungumzia masuala binafsi, hayo ya tabia zake sio hoja yetu hapa wala hakuna aliyesema kifo chake kichunguzwe kwa sababu alikuwa mkamilifu ana tabia njema kama Lissu ambaye ndio mnaona anastahili shambulizi lake kuchunguzwa.
 
Sisi tunachojua alikuwa muuaji na kama aliuliwa basi ndiyo vile kuwa malipo ni hapa hapa duniani
Kwamba alikuwa muuwaji, si kila mtu ana huo mtazamo mkuu wabongo wanapenda kujipa hisia kunyume na uhalisia.
 
Ndio maana mnahusiwa kutenda wema bila kujali utapata nini au utakosa nini. Huyo unayemsemea mbona hakutaka kufanya uchunguzi huru kwa Azory na Saa8! Maisha ya duniani mafupi ishini kwa wema. Vyeo hupita tu.
Mkuu huo uchunguzi haumfaidishi marehemu yeye keshakufa, huo uchunguzi ni kwa ajiri tulio hai.
 
Kwani yeye aliua wangapi? Tuanze kwanza kuchunguza wanasiasa waliokufa vifo vyenye utata kipindi akiwa Rais kwanza ndio tuende kwake
Au hao wengine hawana maana sababu hawakua marais? Binadamu wote ni sawa
Muosha huoshwa, auwae kwa ncha ya upanga nae huuwawa kwa upaga.
 
Muosha huoshwa, auwae kwa ncha ya upanga nae huuwawa kwa upaga.
Na Lissu alifanya nini hadi naye kikamkuta kile kilichomkuta maana sio wote waliyokutwa na kilichomkuta Lissu? ambaye sasa keshapata ulemavu wakati alikuwa mzima?
 

Mtu aliyefiwa na mpendwa wake hupitia hatua nyingi sana katika kupona, lakini hatua ya kwanza kabisa ni kuhisia kuwa mpendwa wake hakufa kifo cha kawaida bali ameuliwa na mtu.

Uzi huu ulianzishwa kipindi watu wakilia, ni sawa.
 
Bado unazungumzia masuala binafsi, hayo ya tabia zake sio hoja yetu hapa wala hakuna aliyesema kifo chake kichunguzwe kwa sababu alikuwa mkamilifu ana tabia njema kama Lissu ambaye ndio mnaona anastahili shambulizi lake kuchunguzwa.

Kama yeye hakuwa anajali ubinafsi na yuko kitaasisi, vifo ama kupotea kwa wengine kulipaswa kuchunguzwa kitaasisi bila kumsikiliza yeye. Sasa unataka watu wafuate utaratibu wakati yeye mwenyewe alipokuwa kwenye ofisi alipindisha sheria! Au unaona urais ni cheo cha maana sana mpaka kila mmoja atetemekee kifo chake?
 
Kama yeye hakuwa anajali ubinafsi na yuko kitaasisi, vifo ama kupotea kwa wengine kulipaswa kuchunguzwa kitaasisi bila kumsikiliza yeye. Sasa unataka watu wafuate utaratibu wakati yeye mwenyewe alipokuwa kwenye ofisi alipindisha sheria! Au unaona urais ni cheo cha maana sana mpaka kila mmoja atetemekee kifo chake?
Mkuu labda hujaelewa, hakuna ambacho kitamfaidisha marehemu wala huo uchunguzi hauna masilahi kwa marehemu.

Tatizo mkuu unaleta hisia zako binafsi kwa marehemu na sisi hatuko huko, kwahiyo mnavyotaga ufanyike uchunguzi wa shambuluzi la mtakatifu Lissu ni kwa sababu Lissu ni kwa sababu ya tabia za Lissu?
 
Back
Top Bottom