Napendekeza jaji Samatta au Tundu Lissu kwenye nafasi ya uspika wa Bunge la katiba kwa sababu...

Napendekeza jaji Samatta au Tundu Lissu kwenye nafasi ya uspika wa Bunge la katiba kwa sababu...

Mikael Aweda

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
2,973
Reaction score
3,904
Gazeti la Rai wiki hii limekuja na majina mengi lakini kati ya hayo mimi naona mwenye sifa ya kuongozi Bunge hilo la katiba kama tutaweka itikadi za kisiasa pembeni Jaji mkuu mstaafu Barnabas Samatta au Wakili Tundu Lissu kwa sababu;

Wote ni wanasheria makini wenye uwezo mkubwa sana wa kuchambua sheria ambyo ndo jambo litakalokuwa linahitajika sana ndani ya Bunge hilo.

Pili, Jaji Samatta na Tundu Lissu ni watu wasio na kashfa yo yote. Samatta mwenyewe aliwahi kusema wakati akiwa jaji mkuu kuwa ni heri hakimu mwadilifu mwenye uwezo mdogo kisheria kuliko hakimu mwenye uwezo mkubwa lakini fisadi. Kwa hiyo, yeye mwenyewe na Tundu Lissu ni wanayo sifa zote mbili -- uadilifu usiotiliwa shaka na uwezo mkubwa wa kuchambua mambo. Akina Chenge watatuchafulia mchakato wetu, wakae mbali na nafasi hii.

Nafahamu ugumu wa ccm walio wengi kutomkubali Tundu Lissu ndani ya Bunge la katiba kwa sababu za kisisa tu.
Hata hivyo, kuungana kwa NCCR MAGEUZI, CUF NA CHADEMA ambao wana wabunge wengi kiasi, ukijumlisha na wajumbe 166 ambao tunategemea hawatateuliwa na Rais na uwepo wa wabunge wanaccm wenye msimamo tofauti na chama chao wakiwepo hawa waliopinga sheria hii inayolalamikiwa kutoka bara, bila kusahau wabunge wa ccm wa zanzibar ambao wanaunga mkono msimamo wa kambi ya upinzani kwa siri, kunampa Lissu uwezekano wa kupata fursa hiyo hata kama ni kwa tabu sana.

Ikumbukwe kuwa, jambo la msingi ni kuptakiana kwa spika bora awe Jaji mkuu mstaafu samatta, Wakili Tundu Lissu au mtu mwingine ye yote kutoka po pote. Maombi yetu ni kuwa tusiwapate akina makinda na Ndugai kwenye jambo hili nyeti sana linaloshikilia mustakabali wa nchi yetu kwa miaka zaidi ya 100 ijayo.
Siku njema.
Nawasilisha.
Aweda.
 
Gazeti la
Rai wiki hii limekuja na majina mengi lakini kati ya hayo mimi naona
mwenye sifa ya kuongozi Bunge hilo la katiba kama tutaweka itikadi za
kisiasa pembeni Jaji mkuu mstaafu Barnabas Samatta au Wakili Tundu Lissu
kwa sababu;

Wote ni wanasheria makini wenye uwezo mkubwa sana wa kuchambua sheria
ambyo ndo jambo litakalokuwa linahitajika sana ndani ya Bunge hilo.

Pili, Jaji Samatta na Tundu Lissu ni watu wasio na kashfa yo yote.
Samatta mwenyewe aliwahi kusema wakati akiwa jaji mkuu kuwa ni heri
hakimu mwadilifu mwenye uwezo mdogo kisheria kuliko hakimu mwenye uwezo
mkubwa lakini fisadi. Kwa hiyo, yeye mwenyewe na Tundu Lissu ni wanayo
sifa zote mbili -- uadilifu usiotiliwa shaka na uwezo mkubwa wa
kuchambua mambo. Akina Chenge watatuchafulia mchakato wetu, wakae mbali
na nafasi hii.

Nafahamu ugumu wa ccm walio wengi kutomkubali Tundu Lissu ndani ya Bunge
la katiba kwa sababu za kisisa tu.
Hata hivyo, kuungana kwa NCCR MAGEUZI, CUF NA CHADEMA ambao wana
wabunge wengi kiasi, ukijumlisha na wajumbe 166 ambao tunategemea
hawatateuliwa na Rais na uwepo wa wabunge wanaccm wenye msimamo tofauti
na chama chao wakiwepo hawa waliopinga sheria hii inayolalamikiwa
kutoka bara, bila kusahau wabunge wa ccm wa zanzibar ambao wanaunga
mkono msimamo wa kambi ya upinzani kwa siri, kunampa Lissu uwezekano wa
kupata fursa hiyo hata kama ni kwa tabu sana.

Ikumbukwe kuwa, jambo la msingi ni kuptakiana kwa spika bora awe Jaji
mkuu mstaafu samatta, Wakili Tundu Lissu au mtu mwingine ye yote kutoka
po pote. Maombi yetu ni kuwa tusiwapate akina makinda na Ndugai kwenye
jambo hili nyeti sana linaloshikilia mustakabali wa nchi yetu kwa miaka
zaidi ya 100 ijayo.
Siku njema.
Nawasilisha.
Aweda.

Samatta anaweza lakini Lissu hafai hata kidogo. licha ya kuwa anaongozwa na uchadema lakini pia ataongoza bunge kwa misingi ya uongo, uzushi, uzandiki na husda
 
Tuachane na hawa wazee ambao wamechoka na wengine wamechanganyikiwa Kimaisha. nampendekeza Wakili Edwin Simon Igenge kuongoza jahazi hilo. huyu jamaa ana uwezo mkubwa sana na ni mzalendo
 
Kitendo cha kupendekeza makada wa chama kuongoza Bunge la katiba ni kutaka kulifanya bunge hilo lionekane la kisiasa zaidi
 
Tuachane na hawa wazee ambao wamechoka na wengine wamechanganyikiwa Kimaisha. nampendekeza Wakili Edwin Simon Igenge kuongoza jahazi hilo. huyu jamaa ana uwezo mkubwa sana na ni mzalendo
Lizabuni,
Ninahisia kuwa awaye yote anayeingia akilini mwako lazima/huenda ni Gamba damu damu.
 
Samatta anaweza lakini Lissu hafai hata kidogo. licha ya kuwa anaongozwa na uchadema lakini pia ataongoza bunge kwa misingi ya uongo, uzushi, uzandiki na husda

Hilo la Lissu kuwa mwongo, mzushi, mzandiki na husda limeshajibiwa kama ifuatavyo,
Mosi, madai ya Lissu kwamba TEC, CCT na Shivyawata hawakuwakilishwa katika Tume ya warioba yalitolewa na taasisi hizo tatu, je, umewahi kusikia taasisi hizi tatu zikipinga kauli hiyo?
Pili,madai ya Lissu kwamba Zanzibar haikushirikishwa waziri Chikawe na hata Rais mwenyewe wameshakubali kuwa ni kweli.
Madai ya Lissu kuwa wajumbe 166 watatoka kwenye taasisi gani bado yako pale pale na kwamba chadema inapendekeza utaratibu tofauti ambao bado tunausimamia mpaka sasa.

NB; Kauli ya Lissu Bungeni siyo yake, ni kauli ya kambi ya upinzani kwa hiyo, kama Mnyika alivyosema, matusi hayo yasielekezwe kwake kwa sababu ule ni msimamo wa chama na siyo msimamo wa Lissu kwa kiutaratibu na kwa mujibu wa kanunu za Bunge.
Sawa mkuu?
 
Kitendo cha kupendekeza makada wa chama kuongoza Bunge la katiba ni kutaka kulifanya bunge hilo lionekane la kisiasa zaidi

Mkuu hayo ni mapendekezo yangu, na wewe unaweza kuwapendekeza wengine kama ulivyofanya. Hapa hatugombani tunajadiliana.
 
Tupatie orodha hiyo ya majina kutoka gazeti la Rai ili tuyachambue vizuri.

Kuhusu Lissu,mimi naona ni bora aendelee kuwa mbunge wa kawaida tu katika hilo bunge ili aweze kusaidia kutoa mchango na mawazo yake na pia kuwa kinara wa kuhakikisha mambo yanakwenda sawa kama kawaida yake.Hapa ninamanisha kuomba miongozo,kutoa taarifa,utaratibu n.k.

Akiwa Spika hawezi ku-play part vizuri kama tunavyomjua.

Bunge la katiba bila Lissu kama mbunge ni sawa na chai bila sukari.
 
Tupatie orodha hiyo ya majina kutoks gazeti la rai ili tuyachambue vizuri.

Kuhusu Lissu,mimi naona ni bora mbunge wa kawaida tu katika hilo bunge ili aweze kusaidia kutoa mchango na mawazo yakena pilu kuwa kinara wa kuhakikisha mambo yanakwenda sawa kama kawaida yake.

Akiwa Spika hawezi ku-play part vizuri kama tunavyomjua.

Bunge la katiba bila Lissu kama mbunge ni sawa na chai bila sukari.

Wengine waliotajwa huko ni Samweli Sitta, Andrew Chenge, Juma Mwapachu na Pius Msekwa na Jaji Samatta mwenyewe.
 
Samatta anaweza lakini Lissu hafai hata kidogo. licha ya kuwa anaongozwa na uchadema lakini pia ataongoza bunge kwa misingi ya uongo, uzushi, uzandiki na husda

Mkuu naomba nikuombe radhi kwa kupingana na hoja yako kuhusu Lissu. Hatungekuwa hivi tulivyo kama kusingetokea mmoja akasimamia jambo kwa lengo la kutaka haki itendeke. Lugha uliyotumia ni lugha aliyotumia Mh. Rais kumpamba Lissu, kama Lissu ndivyo alivyo basi hakika Rais asingewaita Ikulu ili kuyamaliza. Kama siyo hawa wapinzania tunaowatukana leo lini ungejua kuwa kuna fedha za hawa walioko madarakani zimefichwa Uswiss? EPA ungeijuaje wewe kama siyo hao unaowatukana leo? Kuna mengi ningeweza kuyaandika hapa lakini nayaacha ili tusiwe wavivu wa kufikiri.
 
Tuachane na hawa wazee ambao wamechoka na wengine wamechanganyikiwa Kimaisha. nampendekeza Wakili Edwin Simon Igenge kuongoza jahazi hilo. huyu jamaa ana uwezo mkubwa sana na ni mzalendo

Nashukuru kwa mapendekezo yako, hili ni jambo zuri. Je, huyu ni nani anafanya nini wapi? Unaweza kumwelezea kwa urefu kidogo.Je, ni Mbunge wa Bunge la katiba? Maana kuwa spika lazima uwe mjumbe wa kikao kwanza au uwe mbunge wa Bunge hilo kwanza.
Watajwa wengine ukimwacha Lissu na Sitta akiwepo samatta mwenyewe wanapigiwa chapuo kwenye nafasi 166 za wajumbe wengine ambao utataratibu wa kupatikana kwao ndo umeleta Nongwa iliyopo.
 
Tuachane na hawa wazee ambao wamechoka na wengine wamechanganyikiwa Kimaisha. nampendekeza Wakili Edwin Simon Igenge kuongoza jahazi hilo. huyu jamaa ana uwezo mkubwa sana na ni mzalendo

Hivi nyinyi CCM hii tabia ya kutukana wazee mtaacha lini? Kumbe laana mnajipa wenyewe halafu mnasingizia CDM..
 
CCM ukiwatajia Lissu, ni sawa na kuweka Mbolea ya chumvi chumvi kwenye kidonda!!
 
Mkuu naomba nikuombe radhi kwa kupingana na hoja yako kuhusu Lissu. Hatungekuwa hivi tulivyo kama kusingetokea mmoja akasimamia jambo kwa lengo la kutaka haki itendeke. Lugha uliyotumia ni lugha aliyotumia Mh. Rais kumpamba Lissu, kama Lissu ndivyo alivyo basi hakika Rais asingewaita Ikulu ili kuyamaliza. Kama siyo hawa wapinzania tunaowatukana leo lini ungejua kuwa kuna fedha za hawa walioko madarakani zimefichwa Uswiss? EPA ungeijuaje wewe kama siyo hao unaowatukana leo? Kuna mengi ningeweza kuyaandika hapa lakini nayaacha ili tusiwe wavivu wa kufikiri.

Nakubaliana na wewe, Lissu ni mtu wa muhimu sana ktk nchi hii na amesaidia MENGI ndani ya Bunge. Hilo ni jambo lilio wazi sema tu wakati mwingine ushabiki wa kiitikadi inakuwa changamoto kidogo kwa baadhi yetu.
 
Tupatie orodha hiyo ya majina kutoka gazeti la Rai ili tuyachambue vizuri.

Kuhusu Lissu,mimi naona ni bora aendelee kuwa mbunge wa kawaida tu katika hilo bunge ili aweze kusaidia kutoa mchango na mawazo yake na pia kuwa kinara wa kuhakikisha mambo yanakwenda sawa kama kawaida yake.Hapa ninamanisha kuomba miongozo,kutoa taarifa,utaratibu n.k.

Akiwa Spika hawezi ku-play part vizuri kama tunavyomjua.

Bunge la katiba bila Lissu kama mbunge ni sawa na chai bila sukari.

Nakubaliana na wewe kabisa kwa 100%. Lissu ni lazima akae kwa wabunge wengine ili kuwa mwanga na taa ya kumulika kila aina ya uozo utakaokuwa unajitokeza...
 
Tupatie orodha hiyo ya majina kutoka gazeti la Rai ili tuyachambue vizuri.

Kuhusu Lissu,mimi naona ni bora aendelee kuwa mbunge wa kawaida tu katika hilo bunge ili aweze kusaidia kutoa mchango na mawazo yake na pia kuwa kinara wa kuhakikisha mambo yanakwenda sawa kama kawaida yake.Hapa ninamanisha kuomba miongozo,kutoa taarifa,utaratibu n.k.

Akiwa Spika hawezi ku-play part vizuri kama tunavyomjua.

Bunge la katiba bila Lissu kama mbunge ni sawa na chai bila sukari.

Kimsingi nakubaliana na hoja yako, lakini je, ni lazima spika asitoe maoni yake? Mimi nadhani itategemea kanuni watakazojiwekea itakavyokuwa. Ikumbukwe pale hakuna vyama au pande mbili zinazotofautiana. Watz wanaojenga mstakabali wa nchi yetu kwa faida ya vizazi vijavyo.
 
Ningependa spika asiwe aliegemea upande wowote wa chama cha siasa. Hii itaongeza impartiality katika maamuzi. Hivyo kwa maoni yangu, Samatta sawa (naamini hajaegemea chama chochote!), Lissu hapana (ni gwanda).

Hata hivyo naheshimu mchango mkubwa wa Lissu na naamini anao uwezo mkubwa tu.
 
Mh Tundu Lissu abaki kua mbunge katika bunge la katiba,napendekeza Jaji Samatta awe spika
 
Back
Top Bottom