Gazeti la Rai wiki hii limekuja na majina mengi lakini kati ya hayo mimi naona mwenye sifa ya kuongozi Bunge hilo la katiba kama tutaweka itikadi za kisiasa pembeni Jaji mkuu mstaafu Barnabas Samatta au Wakili Tundu Lissu kwa sababu;
Wote ni wanasheria makini wenye uwezo mkubwa sana wa kuchambua sheria ambyo ndo jambo litakalokuwa linahitajika sana ndani ya Bunge hilo.
Pili, Jaji Samatta na Tundu Lissu ni watu wasio na kashfa yo yote. Samatta mwenyewe aliwahi kusema wakati akiwa jaji mkuu kuwa ni heri hakimu mwadilifu mwenye uwezo mdogo kisheria kuliko hakimu mwenye uwezo mkubwa lakini fisadi. Kwa hiyo, yeye mwenyewe na Tundu Lissu ni wanayo sifa zote mbili -- uadilifu usiotiliwa shaka na uwezo mkubwa wa kuchambua mambo. Akina Chenge watatuchafulia mchakato wetu, wakae mbali na nafasi hii.
Nafahamu ugumu wa ccm walio wengi kutomkubali Tundu Lissu ndani ya Bunge la katiba kwa sababu za kisisa tu.
Hata hivyo, kuungana kwa NCCR MAGEUZI, CUF NA CHADEMA ambao wana wabunge wengi kiasi, ukijumlisha na wajumbe 166 ambao tunategemea hawatateuliwa na Rais na uwepo wa wabunge wanaccm wenye msimamo tofauti na chama chao wakiwepo hawa waliopinga sheria hii inayolalamikiwa kutoka bara, bila kusahau wabunge wa ccm wa zanzibar ambao wanaunga mkono msimamo wa kambi ya upinzani kwa siri, kunampa Lissu uwezekano wa kupata fursa hiyo hata kama ni kwa tabu sana.
Ikumbukwe kuwa, jambo la msingi ni kuptakiana kwa spika bora awe Jaji mkuu mstaafu samatta, Wakili Tundu Lissu au mtu mwingine ye yote kutoka po pote. Maombi yetu ni kuwa tusiwapate akina makinda na Ndugai kwenye jambo hili nyeti sana linaloshikilia mustakabali wa nchi yetu kwa miaka zaidi ya 100 ijayo.
Siku njema.
Nawasilisha.
Aweda.