Napendekeza Katiba ya CCM irekebishwe ili Dkt. Magufuli aendelee kuwa Mwenyekiti hadi atakapoamua kung'atuka kama Nyerere

Kwani Katiba ya CCM ina zuio hilo? Kama hamna, anaweza kuendelea tu kama wanachama wenzake wataendelea kumchagua. Na kwa mfumo wetu Mwenyekiti wa chama kinachotoa Rais ana nguvu kuliko Rais.

Amandla...
 
Waz
Wazo zuri,hata yule wa cdm aliiharibu ile katiba ya 1 ya chama chake akatengeneza nyingine inayomfanya kuwa mwenyekiti wa muda wote wa cdm.
 
Mwenyekiti wa chama bila kuwa na dola mkononi ni kujitafutia matatizo tu, kwa sababu mwenye dola anaweza kukupoteza fasta ukiingia kwenye anga zake
Mwaka 2008 Putin hakugombea urais wa Uusi kwa sababu alikuwa amefikia ukomo kulingana na Katiba yao. Alimwachia mtu wake agombee ambae akamteua kuwa Waziri Mkuu. Kila mtu alijua kuwa mtawala ni Putin na sio Rais wa wakati ule. Mwaka 2012 Putin akagombea urais na ndio huyo anaendelea nao.

Kwa mfumo wetu, sio lazima Katiba ibadilishwe ili mtu aendelee kutawala kama anataka. Hamna kitakachomzuia yeye kama Mwenyekiti wa Chama chake kumteua mtu wake ili agombee urais. Hata kama hatachukua nafasi yeyote serikalini, huyo rais atajua uwepo wake kwenye cheo hicho unategemea Mwenyekiti wa chama chake. Mwenyekiti ana uwezo wa kumyang'anya uanachama na hivyo kufanya nafasi yake iwe ngumu. Au anaweza kuwashawishi wabunge wa chama chake kum impeach na kumuondoa madarakani. Miaka mitano ikipita Mwenyekiti anagombea tena urais.

Tusisahau hata Nyerere alimuachia Kawawa Uwaziri Mkuu bila madhara yeyote. Uenyekiti ndio habari yenyewe, sio Urais.

Amandla...
 
Mwenyekiti wa Chama ndio mwenye jukumu la kuhakikisha chama chake kinashika dola na sio Rais. Kwa sababu hiyo chama chochote kinataka kuwa na kiongozi bora zaidi wa kukiwezesha kufikia hapo. Ndio maana kuweka kikomo kwenye nafasi ya Uenyekiti wa chama hakuna tija. Maalim alifunzwa hivyo na Lipumba alipodhani u katibu mkuu unampa mamlala zaidi ya Mwenyekiti. Ndio maana hajarudia kosa hilo ACT-WAZALENDO.

Amandla...
 
Aisee, achana na kitu kinachoitwa Amiri jeshi mkuu.
Na uraisi huwa hauna ubia, na raisi hazoeleki.
Mtu akishakalia hiyo nafasi na akapanga safu zake vizuri, itategemea hekima zake tu la sivyo hata huyo aliyedhani kuwa kamuweka anakuwa hayuko salama kivile, anaweza akamchenjia anytime!

Ukinivua uanachana wakati mimi naamrisha majeshi na usalama wa Taifa, kwqnza hicho kikao mtakikalia wapi na saa ngapi?.

Kwa nini nisiwafungulie kesi ya "uhaini", "usaliti" au kesi yoyote ile ninayoona inafaa?

Kule Russia iliwezekana kwa sababu Putin na Medvedev walikuwa na makubaliano yao binafsi!
 
Hapa kwetu hao wote unaowataja ni wanachama wazuri wa chama tawala na wanakuwa na political ambitions zao. Na rais yeyote atakaeachia ngazi kwa nia ya kurudi tena ni lazima atakuwa na makubaliano na anaemwachia hiyo nafasi. Ila, uko sahihi, kuwa kuna risk kubwa ya jamaa kuamua kumshughulikia sponsor wake kama ilivyotokea Angola. Akifanya hivyo kwetu kwa Mwenyekiti wake patatokea constitutional crisis kwa sabau mfumo mzima umejengwa kwa imani kuwa Mwenyekiti na Rais wataelewana kama vyeo hivyo vitashikwa na watu tofauti.

Amandla...
 
Sababu kuu ya mwalimu kusisitiza Rais ndo awe huyohuyo mkuu wa chama ni sababu hizohizo za mgongano kati ya mkuu wa chama na mshika dola.

All in all rais wa TZ kwa mujibu wa katiba hata asipokuwa mwenyekiti wa chama, ana uwezo wa kumpoteza mwenyekiti wa chama anayemzingua na asifanywe kitu chochote. Anaweza kumpa kesi tu, au hata kum "Ben Saanane", Watamfanya nini?
 
Hakuna jamii iliyokosa watu waendwazimu.

Hata Hitler kuna watu walipenda awe Rais wlsi wa Ujerumani tu bali wa Ulaya nzima. Kama unampenda sana Magu, kamkabidhi familia yako lakini wanaCCM wanalia, hawamtaki, na wanasuburia sana muda huo ufike, ili ikiwezekana chama kipate uongozi mwenye hekima.
 
Hizi ni akili za kipumbavu sana, au kwa vile mnakula meza moja na mfalme wenu?

Upumbavu mkubwa kuleta hoja za kishenzi kwenye forum ya wenye akili.
 
Itakuwa ni jambo jema,ila sasa na yule mwenyekiti mwenza wa chama pendwa muache kumuandama,Naye amewafanyia makuu watu wake.
 

Ulikuwa utashi wake tu. Sidhani kama kuna katiba ya chama chochote inasema hivyo. Inategemea msimamo wa hao watendaji wake. Kumbuka ingawa Rais anateua majaji lakini hana Mamlaka ya kuwafukuza. Na majaji atakaowakuta ni wale walioteuliwa na waliomtangulia. Ni kweli kuwa wakuu wa taasisi nyingi serve at the pleasure ya Rais. Lakini sidhani kama wote watakubali kutumika kumshughulikia mtu aliyewapa hizo nafasi. Na nadhani kuwa hata ukiondoa viongozi wakuu taasisi nyingi zinakuwa na watu wengi ambao watakuwa loyal kwa Mwenyekiti. Rais akiamua kumshughulikia nchi inaweza kuvurugika sana.

Amandla...
 
Mambo tuliyoshindwa kuyafanya marais watatu kwa miaka 30 Rais Magufuli ameyafanya kwa miaka 3 by Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.

Labda hiyo quote itakusaidia.
Mkuu hakuna jipya Linafanyika halijawai kuwepo au kufanyika,mh Mwinyi , marehem mkapa lazima waseme hivyo Nikimtoa mh kikwete,
Mh Mwinyi rais msahafu kaachiwa nchi ikiwa imara, kiviwanda, shilingi, ndege, n.k yeye ndo chanzo mpaka ana mkabidhi nchi Mkapa ambaye pia aliendeleza ubinfsishaji usio na tija na kupeleka nchi kwenye shimo , na madhara yake ndo mpaka mda huu yanaendelea,
Wangine wanaongezea, na kurekebisha ila sio kwamba Kuna kipya hakijawai tokea tz, na KWA taifa Kama letu KWA umri wake hakuna kiongozi anaweza sema yeye ndo kalijenga zaidi kuliko mwingine, TAIFA, ni Kama mtoto, hupitia hatua mbalimbali mpaka kufanikiwa
Tatizo linalotukabili ni kukosa dila mahalum ya taifa kwamba kila kiongozi hawapo pale juu ajikite kwenye dila husika ,sio kila ajae aje na mfumo wake,maono yake,na utashi wake nini afanye ,hii Kama taifa hatuwezi songa mbele,kiongozi huyu atengeneza hili, akija mwingine anaacha anafanya hivi ,na ndo maana tuko hapa kwamba mwalim aliliacha taifa pazuri, waliofuata wakavuruga hasa awam mbili zilizofuata, so JK ,JPM ,wanacheza mziki ambao sio dhambi zao bali za awam zilizotangulia,
Hata hivyo sio kibali kwamba jpm aongezewe mda,maana pia yapo mengine kajitahidi na mengine hamna ,so lazima kupata vichwa vipya,
 
subiria mitusi ya LUMUMBA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…