Napendekeza Katiba ya CCM irekebishwe ili Dkt. Magufuli aendelee kuwa Mwenyekiti hadi atakapoamua kung'atuka kama Nyerere

Napendekeza Katiba ya CCM irekebishwe ili Dkt. Magufuli aendelee kuwa Mwenyekiti hadi atakapoamua kung'atuka kama Nyerere

Nami nakuunga mkono kuliko kuongeza muhula mwingine wa urais bora awe Mwenyekiti wa maisha wa CCM
 
Yeye hajaongelea Katiba ya Nchi ameongelea Katiba ya Chama chao.
Hapo sawa. CCM waendelee na umilele wa chama chao lakini wasilazimishe KATIBA YA NCHI na umilele wao. Latina ya nchi inatambua uwepo wavyama vinginakila chama kina sera zake, ziheshimiwe.
 
CCM ni chama dola.

CCM ni chama tawala wala hilo halina ubishi.

CCM ni chama mbeba maono wa taifa hili la Tanzania.

Dr Magufuli ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM na Rais wa nchi yetu ameonyesha uwezo mkubwa sana katika kusimamia misingi ya chama na uzalendo kwa ujumla.

Kwa mageuzi makubwa anayoendelea kuyafanya ndani ya chama ambayo yameonyesha ufanisi mkubwa kwa maendeleo ya taifa, napendekeza katiba ya CCM ifanyiwe marekebisho ili nafasi ya mwenyekiti isiwe na ukomo.

Hii itatoa fursa kwa mwenyekiti Magufuli kuendelea na uongozi hadi atakapoamua kung'atuka kama alivyofanya baba wa taifa Mwalimu Nyerere.

Maendeleo hayana vyama!
Pendekeza Tanzania kuwa Nchi ya Kifalme
 
Lazima chama kikibadili katiba yake basi ,huku kungine rahis tu kama wanasukuma mlevi.na ndicho kitafata hao akina butiku wanasema tu
 
Nazungumzia katiba ya CCM!
Rais analitumikia taifa ambalo linaongozwa na katiba ya nchi, Rais kafanya mambo yenye maslahi kwa nchi yake wakiwemo wasiokijua chama chake hicho, Bora ungeshauri tufanye mageuzi ya katiba sababu ndio mgongo wa Taifa zima na maamuzi yanayofanyika kutokana na katiba yanaathiri kila kada tofauti na katiba ya CCM ambayo si katiba ya nchi.
 
Tunataka rais wetu ajaye tumpe na uenyekiti wa chama, Magufuli akapumzike chato. Hatuwezi ruhusu Rais wetu awe chini ya mtu mwingine chamani.
 
Mkuu hakuna jipya Linafanyika halijawai kuwepo au kufanyika,mh Mwinyi , marehem mkapa lazima waseme hivyo Nikimtoa mh kikwete,
Mh Mwinyi rais msahafu kaachiwa nchi ikiwa imara, kiviwanda, shilingi, ndege, n.k yeye ndo chanzo mpaka ana mkabidhi nchi Mkapa ambaye pia aliendeleza ubinfsishaji usio na tija na kupeleka nchi kwenye shimo , na madhara yake ndo mpaka mda huu yanaendelea,
Wangine wanaongezea, na kurekebisha ila sio kwamba Kuna kipya hakijawai tokea tz, na KWA taifa Kama letu KWA umri wake hakuna kiongozi anaweza sema yeye ndo kalijenga zaidi kuliko mwingine, TAIFA, ni Kama mtoto, hupitia hatua mbalimbali mpaka kufanikiwa
Tatizo linalotukabili ni kukosa dila mahalum ya taifa kwamba kila kiongozi hawapo pale juu ajikite kwenye dila husika ,sio kila ajae aje na mfumo wake,maono yake,na utashi wake nini afanye ,hii Kama taifa hatuwezi songa mbele,kiongozi huyu atengeneza hili, akija mwingine anaacha anafanya hivi ,na ndo maana tuko hapa kwamba mwalim aliliacha taifa pazuri, waliofuata wakavuruga hasa awam mbili zilizofuata, so JK ,JPM ,wanacheza mziki ambao sio dhambi zao bali za awam zilizotangulia,
Hata hivyo sio kibali kwamba jpm aongezewe mda,maana pia yapo mengine kajitahidi na mengine hamna ,so lazima kupata vichwa vipya,
Hadi hapo tutapoondoa imani kwa watu na kujenga kifumo ambayo itaheshimiwa na yeyote ataeingia madarakani. Tutaendelea na haka kamchezo ka hatua mbili mbele hatua tatu nyuma
 
CCM ni chama dola.

CCM ni chama tawala wala hilo halina ubishi.

CCM ni chama mbeba maono wa taifa hili la Tanzania.

Dkt. Magufuli ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM na Rais wa nchi yetu ameonyesha uwezo mkubwa sana katika kusimamia misingi ya chama na uzalendo kwa ujumla.

Kwa mageuzi makubwa anayoendelea kuyafanya ndani ya chama ambayo yameonyesha ufanisi mkubwa kwa maendeleo ya taifa, napendekeza katiba ya CCM ifanyiwe marekebisho ili nafasi ya mwenyekiti isiwe na ukomo.

Hii itatoa fursa kwa mwenyekiti Magufuli kuendelea na uongozi hadi atakapoamua kung'atuka kama alivyofanya baba wa taifa Mwalimu Nyerere.

Maendeleo hayana vyama!
aibu yako
 
Mzoga wako umebakia mifupa tu now.

Unamuabudu vipi mwanadamu?
 
Back
Top Bottom