Napendekeza kofia ngumu ndani ya usafiri wa mabasi

Daah pole Mkuu...
 
Una wazo zuri ila halitekelezeki kama suluhisho. Ajali za mabasi na malori nyingi ni head on collisions. Serikali iweke barabara separate kwa gari za kwenda na kurudi. Magari yamekuwa mengi ajali haziepukiki kwa kuweka speed governor ya 80kph!

Nikuulize tu ushawahi ona ajali ya gari kugongana uso kwa uso katika bara bara ya Kimara mwisho hadi Kibaha toka ijengwe njia 8?
 
Nimecheka. Kwanza tunaonyoa wanataka tufikeje makazini? Natoka home nimechana nywele yangu, kidala nivae helmet inivurugie kichwa?
Imagine unatoka Dar-Kigoma na helmet kichwani.
 
Sasa waTZ hawajui umuhimu wa kufunga mikanda tu ni issue kofia zitasaidia nn?
 
We jamaa ni great thinker mzuri sana. Tatizo hatuna hata research firms za kueleweka kwa hiyo hata hizo tafiti hatujawai fanya. Nawaza tu hapa ukitengeneza kofia za namna hii ukiuza pale Magufuli terminal watu watanunua tu hakuna anayependa kufa.
Tafiti zimeshafanywa na kuonekana uwekaji na utumiaji wa mikanda kwenye viti, pamoja na mwendokasi wa km 80/h kwa mabasi vinasaidia sana kupunguza madhara kwa ajali za mabasi.
 
Hzo helmet labda ziwe zile zinazotumiwa na madereva wa Formula 1, hata hivyo Bado ni wazo la kijinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…