Wanabodi,
Miaka mitano ya Rais John Pombe Magufuli si mingi. Itaisha muda si mrefu.
Ninajua 2015 vijana wengi wa CCM walijitokeza kuutaka Urais wakiwemo January Makamba, Mwigulu Nchemba hata Hamisi Kigwangala lakini wote waliangukia pua baada ya kuachwa kwenye mchujo.
Kwa mwaka 2025 kwa mtazamo na maoni yangu twende na kijana Ridhiwan Kikwete. Kijana huyu ni mnyenyekevu, hodari, mchapakazi, msomi, muumini wa haki za binadamu na haiba ya kiuongozi.
Riz amezaliwa na kukulia familia ya utawala na hivyo kuwa na uzoefu na si wa kuokota dodo chini ya mwembe. Anatufaa maana hana tamaa ya madaraka.
#RK2025