Mfumo huu utawezesha kuwa na real time data feed ya nguzo zote za Tanesco kwa kujua mahali zilipo na kama zinaumeme.
Mtendaji wa Tanesco akiingia kwenye hii Geomap, nguzo zote zitaonekana kwa rangi nyekundu kama sensor zinasoma moto, na rangi ya kijivu kama sensor hazisomi moto. Hivyo moja kwa moja itajichora ramani ya mfumo mzima wa nguzo, na jinsi umeme ulivyo upatikanaji wake kwa wakati husika.
Taarifa za kukatika umeme zitakuwa zinajituma zenyewe automatically kwenye data feed ya mfumo, ni kiasi cha kufungia alerts kama unavyofungua notifications kwenye simu, na meneja wa mkoa husika wa Tamesco ataweza kuwa na live feed ya hali ya upatikanaji umeme.
Hii itarahisisha utoaji taarifa za kuanguka kwa nguzo, nk, ambapo mtoa taarifa atataja code number ya nguzo, na moja kwa moja Geomap itaonyesha nguzo ilipo na itashugulikiwa haraka sana. Hata kuomba umeme itakuwa rahi kwenye masuala ya Geolocation ya muombaji.
Ni hayo tu..
Mkuu
Nguzo kama nguzo haina uhusiano wowote na umeme,ni mechanical pivot ya ku-support wires.
Wires ndio zinabeba umeme,na since kuna electrical continuity tayari kuna system ya kuona kila kitu kupitia huo mwanya wa continuity kwa technology inaitwa scada
Infact scada ya kuona network nzima ni economically feasible kwa network ya nguzo za kuanzia 400kV to walao 33kV.
Kwenye nguzo za 33kV mtaani kuna fiber optic cable imepita juu katika across the whole network kukusanya ujinga wote
Wire ukikatika kokote kwenye nguzo yeyote mtaani popote kwenye mfumo wa 400kV mpaka 33kV inaonekana vizuri tu
Nguzo za mitaani sio asset za maana kiivyo kuweka huo mfumo wa mabilioni ya pesa kiasi hicho
Vitu ambavyo ni worthy assets ni labda transformer kubwa hata za chini,meter ya kupima umeme majumbani,substations,etc...sio nguzo
Nguzo sio asset ya msingi kiivyo.....kwanza network nzima inaonekana physically kwenye computer za scada centre
Nadhani bado sijaelewa unataka nini hasa chenye kuleta economic sense na kinarudisha hiyo investment.
Nguzo?Ambazo ni just mechanical pivots?Nah
I just recalled my undergrad electrical class here