FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
Nilikuwa napendekeza hawa walimu ambao tayari wameshaajiriwa kazi yao isiwe kufundisha, kazi yao ibaki kuchukua attendance na kusahihisha mitihani tu.
kwanza hawajui kufundisha, halafu hata hicho wanachokifundisha hawakijui.
Yaani mwalimu kabisa wa hesabu wa shule ya msingi unamuuliza akueleze chochote kuhusu ‘Trigonometric ratios’ , ana baki anatoa macho tu.., hamna kitu., unamuuliza akueleze kanuni ya kutafuta ‘Surface Area’ ya Cylinder , anabaki kucheka cheka tu.
Sasa basi, napendekeza serikali iandae vipindi vya masomo mbali mbali ambapo vitarekodiwa kwenye video, pia video ziambatane na ‘Illustrative video animations’ ; ambapo mashuleni watakuwa wanapelekewa ‘Flash disk’ yenye vipindi vya masomo yote vya mwaka mzima, na viwe kwa kiswahili kama vile ambavyo wamekuwa wakifundishwa.
Ikifika mida wa kipindi husika, kiranja wa darasa anaweka flash, anachagua somo husika la kipindi husika kwa siku husika, na hapo wataanza kusikiliza somo , na wakimaliza wataweka slides na kuchukua notes hapo hapo na kukopy exercise za kufanya. Wakimaliza wanakusanya, mwalimu yeye kazi yake kusahihisha tu! Itumike Projector na tablet moja tu inatosha.
Hawa waliopo wanatosha sana kwa kuchukua attendance na kuchapa wale wasiofika shuleni, maana ndio wanachojua, lakini kitaaluma wapo empty, nina ndugu namjua personally, hadi nasemaga, hivi serikali ndio inamlipa huyu mshahara, hajui kitu kabisa!
Projector na Tablet havizidi laki 5, hapo na solar panel unapata, ila mwalimu unamlipa mamilioni kwa mwaka wakati anaingia darasani mara moja kwa mwezi.
Najua nimeeleeweka.
==========================
Kwa kuboresha, mfumo ufungiwe AKILI MNEMBA (AI) ili kuweza kujibu maswali ya wanafunzi kwa urahisi na ufanisi.
==========================
Update: 08/02/2024
Wazo limefanyiwa kazi vizuri kabisa.
==========================
Update: 10/02/2024