Napendekeza serikali ifunge projector madarasa yote shule za msingi badala ya kuajiri walimu, hii itasaidia kuokoa takriban trillion 3 Kwa mwaka

K
Kwenda shule kupata elimu na kuwa na uwezo wa kutumia elimu hiyo kufanya uchambuzi wa kina ni tatizo kubwa miongoni mwa wasomi vijana wa Kitanzania.
 
Ni sahihi kabisa. Kuna udhaifu wa kupingukiwa maarifa kwa BAADHI ya walimu hususani kwa masomo ya hesabu,sayansi na ung’eng’e.Na ukifuatilia unaweza kukuta kuna sababu za msingi ama zisizo za msingi za hao BAADHI ya walimu kuwa hivyo.
Kuhusu njia uliyopendekeza kutumika kufundishia ni nzuri isipokuwa kwa taaluma ya ualimu na kwa level ya msingi, the best method ya kumpa maarifa mtoto inaitwa student-centered method. Yaani mwanafunzi ndio awe kiini cha yeye kupokea maarifa. Kwa level ya primary tulishatoka kabisa kwenye teacher-centered method na inatumika kwa kiasi kidogo Hivyo kutumia projector ni kama kumnyima mtoto fursa ya yeye kuwa chanzo cha maarifa anayopaswa.
 
Unamuhukumu mwalim bila kufuatilia mchakato uliomtengeneza huyo mwalimu, ,, nafikili Kuna vitu vingi vinatakiwa kulekebishwa, ikiwemo elimu ya mleta maada, contents za reasoning kwenye taaluma yake zilikuwa haba ingawa alikuwa na akili ya kuelewa , ila hakupata contents za kumsaidia kujaribu kuelewa Kila jambo,

NB, walimu wa msingi wanafundisha masomo mengi ambayo hawakusomea, ila waliyofaulu kidato Cha nne angalau kwa alama D, ili ufauru hesabu kwa alama D unatakiwa angalau ujue topics nne ambazo ni composory , kama ilivo Geography kwa Map. Statics ,photo na survey, unapata D
 
 
Tatizo mnarahisisha mambo, nchi hii tukiulizana wanaopata (waliopata) angalau D ya hesabu kidato cha nne ni wangapi?, Pia shule ya msingi hakuna specialization yaani mwalimu anafundisha masomo yote, sasa hapo unataka mwalimu ajue vingi visivyomhusu kwa faida na maslahi ya nani?.

Mwalimu analipwa kiasi gani hadi ajitese kujua mengi wakati muda huo angetengeneza visheti ili awauzie wanafunzi?.

Unataka mwalimu wa sekondari ajue triple integral sijui topology au furiour series ili iweje?.

Kikubwa ambacho watu hawajui wanataka kile anachojua basi na kila mtu akijue wakati hatuko hivyo.

Binafsi ninawapongeza sana walimu wana mambo mengi sana wametuwezesha hadi tumeweza ku-type nyuma ya keyboard, malezi n.k.

Kuna mtu kukaa na watoto wake watatu tu kipindi cha mwezi mmoja wakati wa likizo anaona kero mno hadi anatamani shule zifunguliwe siku inayofuata, sasa je mwalimu anayehangaika na watoto 600 bado hauoni mchango wake hadi kudhani shule ni kukokotoa tu?

Kwenye masuala yahusuyo shule inawezekana jukumu la mwalimu kufundisha likawa na 30%, halafu 70% ikawa inahusisha mambo mengine ambayo "AI, slides na video clips za masomo yaliyoandaliwa visiweze kuyatatua.


Kwa mantiki hiyo bado serikali inapaswa kuajiri walimu wengi zaidi.
Angalia mfano vyo bora duniani kama MIT au Havard University pamoja na technology kubwa waliyo nayo bado utakuta wameajiri walimu wengi mno kwa wastani wa kila wanachuo 8 mnakuwa na Mentor wenu kwa pale MIT, sasa je kwetu sisi dunia ya 3 tena shule ya msingi ndo unataka walimu wapunguzwe?.

Kwa sasa ukitaka kupata walimu ambapo wako vizuri zaidi kichwani basi serikali ibadili muundo wa udahili wa walimu angalau wale waliopata div one O-level na A-level ndio wawe walimu pekee ngazi ya sekondari na wenye angalau diploma ya Elimu ndio wawe walimu wa msingi, vinginevyo hayo unayoyatamani yawe yatabaki nadharia.


Sanjari na hilo hoja zako zingejikita zaidi kutumia hiyo njia uliyoshauri kama nyongeza ya njia mbadala ya kufundishia na Serikali kuboresha maslahi ya walimu kama kuwapa motisha, kuwaongezea mishahara, kuwalipa Overtime et al ili watuzalishie wanafunzi bora.
 
Ngoja tuone kwanza, maana tukiajiri walimu inatia hasara sana taifa ukizingatia mwalimu anaingia mara moja kwa mwezi. Subiri nifikirie, ngoja tushauriane kwanza
 
Dah, kwahiyo issue na mahusiano na interaction ktk jamaa watafundishwa na projector pia? Hebu anza wewe kuwalea watoto wako kwa mfumo wa tablet na projector kwanza nyumbani halafu ndo tuhamishie shule.
 
Aisee! Ni shule gani ya msingi inayofundisha Trig ratios mkuu?
Nimenukuu hapo "mwalimu kabisa wa hesabu wa shule ya msingi unamuuliza akueleze chochote kuhusu ā€˜Trigonometric ratios’ , ana baki anatoa macho tu.., hamna kitu., unamuuliza akueleze kanuni ya kutafuta ā€˜Surface Area’ ya Cylinder , anabaki kucheka cheka tu."
Kama ww ni mwalimu wa S/M nahofia utakuwa unawa Overdose watoto.
Kama ww ni msomi halafu ukaenda kumwuliza mwalimu wa shule ya msingi maswali hayo uliyotaja ya Hesabu alikushangaa.
 
Ngoja tuone kwanza, maana tukiajiri walimu inatia hasara sana taifa ukizingatia mwalimu anaingia mara moja kwa mwezi. Subiri nifikirie, ngoja tushauriane kwanza
Naam; kaeni muyajadili halafu wewe ulete mrejesho hapa.
 
Utakuwa unaishi ulaya.
Hata Ulaya hawafanyi hivyo. Lazima kutofautisha Somo (Subject) na zana za kufundishia(Teaching aids) namna ya kufundisha na lengo au matarajio.
Otherwise utakuwa unaonesha watoto video.
 
Yote uliyosuauri ni mema ila kwa akili za Kiafrika haiwezekani .
Ni heri tuendelee na ujima wetu huu huu
Mkuu, mbona unajihafifisha hivyo? Huna habari kwamba wapo Waafrika wengi sana wanatoa huduma bora na za kiwango cha juu huko ambako sio kwa Waafrika? Jitukuze ww kwanza - Charity begins at home.
 
Daah hela zikiwa nyingi na Taarifa ya CAG inakua nzuri pia kwenye upigaji bora watu waajiriwe walipwe..
 
Hoja yako ni nzuri, ila rejelea upya bei ya projector inayofaa kutumiwa darasani (1.5mil na kuendelea) solar inahitaji mfumo kamili, sola panel 400watts (laki 5 na kuendelea) charge controller 30amps (around laki moja), inverter watts 1000 around laki moja, battery angalau 100aH kuanzia laki 3, jumla una hela ngapi apo jomba? Rejelea upya makadirio yako afu baadhi ya vifaa ni vya kubadili kila mwaka 1 au 2, ajiri na teknishian sasašŸ™†šŸ¾ā€ā™€ļø
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…