Napendekeza Serikali ya Tanzania ichapishe Noti za Shilingi Elfu (50,000) na Laki moja (100,000)

Ni vitu vingapi kwa maisha ya kila siku unanunua ambavyo ni 50 K

Au unataka watu waanze kusumbuana na chenji mtu anaingia kwenye daladala anatoa 50 K au anakunywa bia moja anatoa 50 K...

Pili kuwa na noti yenye denominator kubwa inaonyesha uchumi wenu ni mbovu yaani mtu hata kununua gari inabidi aende na trela la noti hivyo kupunguza hayo wanaweka denominator kubwa... (Kwahio since ninajua haupo serious nashangaa kwanini huu uzi haujaamia kwenye Chit - Chat)
 
Hizi akili zingine bhn ningependeza tuchapishiwe not 200 zile na 100
 
Haya ni mawazo mgando kabisa. Tungekuwa na uchumi mkubwa hatungehitaji hata kuwa na noti ya 10k. Jiulize kwanini US dollar yao hawana noti kubwa zaidi ya $100. Ni wazi pesa yetu Ina thamani ndogo mno, ndio maana, eg, ukienda sokoni kununua mbogaunahitaji kuwa na, mathalani 50k. Ingekuwa na thamani ungebeba elfu tano na ukaweza kununua mahitaji yaleyale. Kama hela yako Haina thamani utasemaje uchumi ni mkubwa?
 
Mm nafikiri au kutokana na elimu ya uchumi niliyonayo ,ni kwamba nchi inalazimika kuchapisha pesa zake baada ya uchumi wake kudorora nauzalishaji pia kudorora.Mfano Zaire ya Mabutu ,uchumi ulidorora na kufikia total collapse of monetary system.The same to Zimbabwe.Yaan Bei ya vitu inapanda in a matter of hr.Unaenda sokoni na kikapu cha pesa ,kwa kuwa vitu vipo juu.Mfano nyanya zinauzwa shs 50,000.Au soda inauzwa laki tatu.This happened in Zaire those big days of Mobout Seseko.Nauli kutoka ya daladala inakuwa shs lak sita.Hapo ndio tunakwenda kuchapisha note ili kupunguza mzigo wa kuzibeba.Yaan hauwezi kuweka pesa mfukoni ili uende baa.Kwan pia ni laki nane.
 
Us noti kubwa si ni dola 100,kwa hiyo hiyo hela haina hadhi?,hebu jibu kwanza hili
 
Duuh mtoa mada sijui uliwaza nini asee, ilitakiwa tupambane noti kubwa iwe walau Sh 1000 na hiyo noti iwe na thamani ya kuweza kununua midrange smartphone ya aina yoyote, kadiri unavyozidi kuchapisha noti kubwa ndivyo thamani ya pesa yako inavyozidi kushuka na hiyo ni dalili mbaya kiuchumi
 
Note elf 50 na laki. Ukija nayo dukani haununui kitu.sina chenji, I elf kumi tu chenji tupata tabu alafu we .ivi wew uliwahi fanya biashara. Au unataka kuua biashara ndogo x2
 
Aliyekwambia Uchumi Imara unakuzwa kwa kuwa na Noti zenye namba nyingi ni nani...!?

Zambia hapo walikua na Noti zenye namba nyingi kama zetu, mwisho wakatengeneza Noti mpya, wakatoa sifuri mbili, leo wana Noti ya Kwacha 1, 2, 5, 10, 50 na 100 ..... !

1 Kwacha = 100 t'sh
 
SAS unajengaje uchumi imara bila viwanda manager ?

Kweli Kbsa ya dhani noti ikiwa za elf 50 na laki ndio Hali ya uchumi itastawi
 
Kuchapisha notes, ni indicator ya Ku collapse kwa uchumi wa nchi. Yaan, bei za vitu zimepanda sana na zinapanda kwa haraka within a month, week tunashindwa kubeba pesa nyingi kwenye pochi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…