Nakujibu sasa usipoelewa na hapa basi ni wazi umetaka mabishano na sio kueleweshwa,
Mwezi/Kalenda ya kiislam ina siku 29 au 30 basi, tukija kwenye suala la mfungo, ikifika siku ya 29 hua unaangaliwa mwezi kama umeandama basi siku inayofata itakua mwezi mwingine(tarehe 1) na kama haujaandama itakamilisha siku 30 na siku inayofata haijalishi mwezi uonekane ama usionekane itakua tarehe 1,
Wamejuaje kama Jumamosi ni Eid? Sababu wao hawakuuona Mwezi jana ambayo ilikua 29, basi leo wamekamilisha siku ya 30 kwa maana hiyo jumamosi mwezi uonekane/usionekane itakua tarehe 1 kwa maana ya sikukuu,
Naimani umepata mwanga.