FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 38,920
- 44,970
Wiki hii kumeanza tena ule usumbufu wa kijinga na wa kila mwaka wa kusimamisha watu barabarani ili kuwakagua sticker za wiki ya nenda kwa usalama barabarani.
Sasa kama ilivyo kawaida yetu hapa jukwaani, pakitokea kero basi tunatoa mawazo walau ya kuondoa au kupunguza kero hiyo. Sasa basi, kwakuwa bima ya chombo cha moto hulipiwa kila mwaka, na kwa kuwa ni vyema gari likakaguliwa roadworthy yake kabla halijawa insured, napendekeza vitu hivi viwili viende sambamba na hivyo sticker hiyo ambayo ni shs. 3,000/= tu, ilipiwe moja kwa moja wakati wa kulipia bima.
Hivyo basi, kama mtu ameshalipa bima, basi automatically gari litakuwa limeshakaguliwa na kulipiwa hiyo shs.3,000/= ya sticker, maana sticker zenyewe tunalipa cash mkononi kwa wauzaji ambao hata hivyo wanachaji shs.10,000/= na kusababisha upotevu mkubwa wa mapato, hivyo malipo haya yakifanyika kieletroniki kwa kutumia mifumo ya ulipaji bima ambayo ipo tayari itasababisha kuokoa pesa nyingi zitokanazo na mauzo ya sticker feki ambazo pia zinauzwa kwa bei kubwa.
Na kwakuwa bima siku hizi hatubandiki sticker, tutakuwa tumeondoa ule usumbufu wa kujaza masticker kwenye vioo, mtu akitaka kukagua anaingiza tu namba za gari kwenye kimashine na majibu yanakuja papo japo.
Nakaribisha maoni