Napendekeza stika za Wiki ya Nenda kwa Usalama zilipiwe kwenye bima, ukikata bima ukague na gari kabisa na vyote ulipie kwa mara moja

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Wiki hii kumeanza tena ule usumbufu wa kijinga na wa kila mwaka wa kusimamisha watu barabarani ili kuwakagua sticker za wiki ya nenda kwa usalama barabarani.

Sasa kama ilivyo kawaida yetu hapa jukwaani, pakitokea kero basi tunatoa mawazo walau ya kuondoa au kupunguza kero hiyo. Sasa basi, kwakuwa bima ya chombo cha moto hulipiwa kila mwaka, na kwa kuwa ni vyema gari likakaguliwa roadworthy yake kabla halijawa insured, napendekeza vitu hivi viwili viende sambamba na hivyo sticker hiyo ambayo ni shs. 3,000/= tu, ilipiwe moja kwa moja wakati wa kulipia bima.

Hivyo basi, kama mtu ameshalipa bima, basi automatically gari litakuwa limeshakaguliwa na kulipiwa hiyo shs.3,000/= ya sticker, maana sticker zenyewe tunalipa cash mkononi kwa wauzaji ambao hata hivyo wanachaji shs.10,000/= na kusababisha upotevu mkubwa wa mapato, hivyo malipo haya yakifanyika kieletroniki kwa kutumia mifumo ya ulipaji bima ambayo ipo tayari itasababisha kuokoa pesa nyingi zitokanazo na mauzo ya sticker feki ambazo pia zinauzwa kwa bei kubwa.

Na kwakuwa bima siku hizi hatubandiki sticker, tutakuwa tumeondoa ule usumbufu wa kujaza masticker kwenye vioo, mtu akitaka kukagua anaingiza tu namba za gari kwenye kimashine na majibu yanakuja papo japo.

Nakaribisha maoni
 
Kwanza mkuu ningependa procedure za kufuata katika kulipia hiyo sticker ya nenda kwa usalama barabarani
Unaenda kituo chochote cha Polisi ulizia Mkaguzi Wa magari ukiwa na Tsh. 5000 yako mkononi pamoja na details za Magari unayotaka kukatia.

Anakuandikia details za Magari yako kwenye kikaratasi kmf. Aina ya gari, rangi pamoja na P.No kisha akakupatia hiki kikaratasi pamoja na karatasi nyingine yenye gundi mahsusi kwa ajili ya kubandikia..

Hiko kikaratasi ndiyo wanakiita Sticker sasa.!
 
Okay mkuu well noted
 
Usumbufu usio wa lazima, ilipwe tu kwenye bima
 
Halafu kibaya sasa, hata ukaguzi wenyewe haufanyiki, yaani sticker zimebaki kama gelesha tu, sasa ya nini kuumizana vichwa na hayo masticker?
 
Mkuu Utawauwa Mapongo Wote Tanzania Kwa Njaa
 
Hatimaye ombi limesikika.
Kuanzia August sticker unalipia kwa control number ukaguzi gharama ni 18,000
 
Kero za stika ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani imeshaanza tena, hii kitu iunganishwe na bima, ikikaguliwa inapewa na bima moja kwa moja
 
shida yenu nini ? mnaleta mada ya kutaka kuwatesa wananchi, sisi tumeridhika kuinunua stica traffic kwa bei yoyote nyamazeni
 
Ni kero kubwa sana, kwa siku unasimamishwa mara 10 eti kukagua stika, stika ya 5k unauziwa 10k.., kero tupu, na hakuna ukaguzi, tukilipa bima na hiyo 5k iwekwe humo humo, unakaguliwa na kulipa bima kwa pamoja
 
Wiki hii kumeanza tena ule usumbufu wa kijinga na wa kila mwaka wa kusimamisha watu barabarani ili kuwakagua sticker za wiki ya nenda kwa usalama barabarani.

Sasa kama ilivyo kawaida yetu hapa jukwaani, pakitokea kero basi tunatoa mawazo walau ya kuondoa au kupunguza kero hiyo. Sasa basi, kwakuwa bima ya chombo cha moto hulipiwa kila mwaka, na kwa kuwa ni vyema gari likakaguliwa roadworthy yake kabla halijawa insured, napendekeza vitu hivi viwili viende sambamba na hivyo sticker hiyo ambayo ni shs. 3,000/= tu, ilipiwe moja kwa moja wakati wa kulipia bima.

Hivyo basi, kama mtu ameshalipa bima, basi automatically gari litakuwa limeshakaguliwa na kulipiwa hiyo shs.3,000/= ya sticker, maana sticker zenyewe tunalipa cash mkononi kwa wauzaji ambao hata hivyo wanachaji shs.10,000/= na kusababisha upotevu mkubwa wa mapato, hivyo malipo haya yakifanyika kieletroniki kwa kutumia mifumo ya ulipaji bima ambayo ipo tayari itasababisha kuokoa pesa nyingi zitokanazo na mauzo ya sticker feki ambazo pia zinauzwa kwa bei kubwa.

Na kwakuwa bima siku hizi hatubandiki sticker, tutakuwa tumeondoa ule usumbufu wa kujaza masticker kwenye vioo, mtu akitaka kukagua anaingiza tu namba za gari kwenye kimashine na majibu yanakuja papo japo.

Nakaribisha maoni

========================
Update: 04/07/2022

Hatimaye ombi limesikika.
Kuanzia August sticker unalipia kwa control number ukaguzi gharama ni 18,000
Una kitu, usikilizwe
 
Back
Top Bottom