Napendekeza taa za mwanga barabarani na nyaya za simu zifungwe kwenye nguzo za umeme

Napendekeza taa za mwanga barabarani na nyaya za simu zifungwe kwenye nguzo za umeme

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Yaani badala ya kununua milingoti ya chuma na wire kwa ajili ya kufunga zile taa za mwanga barabarani, napendekeza taa ziwe zinafungwa kwenye mistimu ya umeme iliyopo kando kando ya barabara na ziungwe kwenye umeme moja kwa moja, hii itakoa fedha nyingi mno.

Pia badala ya kusimika mistimu ya nyaya za simu napendekeza hizo nyaya za simu zifunge tu kwenye mistimu ya umeme ambayo ipo tayari hivyo kuokoa gharama kubwa sana katika usambazaji wa mawasiliano.

Mamlaka husika ziwasiliane na Tanesco ambao ndio wamiliki wa nguzo hizo ili kuona utekelezaji wake.

images.jpeg.jpg


==================================
Update: 08/09/2021

Hatimaye, Nyaya za mawasialiano ya simu za mkongo (Fiber network) kufungwa kwenye nguzo za umeme


==================================
Update: 12/09/2021

===========================
Update: 15/06/2022

==========================


View: https://www.instagram.com/p/C91u30piZpR/?igsh=MTRwZ2ZveGpuZDF3bw==
 
Hivi ufunge taa za barabarani kwenye nguzo ya umeme! Tujuavyo ni kuwa nguzo za umeme zinakaa mita kadha kutoka barabarani, sasa hizo taa zitakazofungwa kwenye nguzo zitakuwa na kazi ya kuangazia madudu kwenye mitaro ya barabara au?

Dunia inaenda kasi hata hizo nguzo za umeme zitaanza kuonekana uchafu muda si mrefu.

Dah!
 
Teknolojia imepanuka sana Tanzania tuna majira ya joto na jua lipo sana utumiaji wa solar uwe endelevu na upigiwe debe sana hasa kwenye taa za barabarani na vijijini ili kupunguza gharama za uendeshaji na kutunza mazingira
 
Aiba,
Iwe solar au otherwise, bado pendekezo langu lipo kama lilivyo.
 
Santino,
Ile taa inafungwa kwenye cantilever ndefu inayoweza ku-span hata mita 2 kutoka ilipo nguzo.
 
Masikini! Yaani unataka miji yetu iwe na uchafu huo kisa kubana matumizi? Ujenge barabara ya gharama kubwa kisha uning'inize taa kwenye hizi nguzo za Tanesco zenye polio.
Mpango mkakati wa Tanesco ni kuongeza matumizi ya nguzo za zege zenye mvuto, na wameshaanza kuzitumia Kariakoo, upanga, kinondoni na kwingineko.
 
Brother hata ukiweka watu wa kuzishikilia hizo taa badala ya nguzo bado ni uchafu mjini.
Kwahiyo tukiweka nguzo nyingine separate za taa halafu tukaziacha hizo za Tanesco kama zilivyo, uchafu unapungua au unaongezeka?
power3.jpg
 
Miji mikubwa sasa hivi haipaswi kuwa na hiyo minguzo iliyopinda miguu.

Umeme upitishwe chini.
Kwa nchi kama yetu inayotumia nguzo za umeme, tukifunga taa kwenye separate pole na tukaacha zilizopo kama zilivyo, uchafu unaongezeka auunapungua?
 
Mitaa mingi yetu haijakaa kwenye mpangilio kwahiyo tutarajie vurugu kwenye hili pendekezo lako
 
Barabara ninayokaa nguzo ziko mita 10 hadi 20 kutoka barabarani unataka wafunge taa kwenye nguzo ili uwe unawanga gizani?
Vipi kwa barabara na mitaa ambayo nguzo za umeme zipo kando tu ya barabara, je, tukiweka separate poles za taa na kuacha za umeme kama zilivyo, uchafu unaongezeka au unapungua?
 
Mitaa mingi yetu haijakaa kwenye mpangilio kwahiyo tutarajie vurugu kwenye hili pendekezo lako
Kwenye hiyo mitaa isiyo na mpangilio, tukiweka taa kwenye nguzo separate na tukaziacha hizo za umeme kama zilivyo, vurugu inaongezeka au inapungua?
 
Vipi kwa barabara na mitaa ambayo nguzo za umeme zipo kando tu ya barabara, je, tukiweka separate poles za taa na kuacha za umeme kama zilivyo, uchafu unaongezeka au unapungua?
Unadhani nguo za umeme zimeongozana kama siafu? Unajua umbali wa kutoka nguzo moja hadi nyingine?

Unataka ili mradi ionekane kuna taa za barabarani au unataka kuona nini wewe?
 
Back
Top Bottom