Pre GE2025 Napendekeza Tanzania iufunge Mtandao wa TikTok

Pre GE2025 Napendekeza Tanzania iufunge Mtandao wa TikTok

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Inakula MB mno majobless tunakaa nayo mbali.

Sema ndo hivyo mkuu, tiktok ni mtandao wa kipuuzi.

Ikumbukwe tiktok ilianza kama mtandao wa maudhui mafupi(sio zaidi ya dk 1), sasa haiwezekani kutengeneza maudhui ya ubora mkubwa yenye urefu wa dk 1 tu....

Video fupi zinatengenezwa kwa ajili ya kukuburudisha tu na si vinginevyo, mtumiaji wa tiktok anajua video ni fupi kwahiyo anascroll haraka, ukitaka kukamata umakini wake inabidi ufanye mambo ya ajabu ajabu.

Na pia huwezi weka taarifa nyingi kwenye video fupi kwahiyo njia nyepesi ni kutengeneza maudhui marahisi yenye mzaha mzaha ama kuchekesha.

Kwahiyo tiktok ikawa sehemu ya utani utani tu, japo wanajitahidi kuongeza urefu wa video ila ulivoanza na unavozoeleka.
 
Acheni unafki ...
Mbona hivyo mnavyovisema mbona mimi huwa sivionagi?

Sema unakua umechagua kuona nini!

Huko mpaka baba Paroko wako yupo...sembuse Mimi ni nani?

Wabongo tunapenda kujikweza Sana ..
Mbona hasira Mzee
Kwani nimekuzuia
Endelea kutumia tik tok
 
Tiktok inakupa kile akili yako inataka, so siku nyingine usizungumze mbele za watu utatia aibu kama akili yako inapenda mambo ya kichawi basi utapata, mambo ya maupinde utapata, ukusema unapenda haya mavituko watakuletea hadi ukimbie, ukitaka mahubiri aisee kuna madhehebu kule hadi uchanganyikiwe,

Kwangu mimi napenda sana mambo ya technology, mambo ya wild life , story yaani kifupi hadi dstv nimewasahau kwa sababu ya tiktok.

Kumbuka tiktok ndio inahamasisha maandamano kenya.

Kifupi baki hapo hapo na akili zako chache
 
Back
Top Bottom