Pre GE2025 Napendekeza Tanzania iufunge Mtandao wa TikTok

Pre GE2025 Napendekeza Tanzania iufunge Mtandao wa TikTok

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Watumiaji wengi wa TikTok hawana maadili. Badala ya kumfungia mtu mmoja mmoja, ni afadhali wakafungia mtandao, hadi pale elimu itakapotolewa kuhusu matumizi ya mtandao huo.

Binafsi sina account ya mtandao lakini kwa video zinazotumwa kwenye mitandao mingine kutoka kwa watumiaji wake; inaonesha wazi watumiaji mtandao huo wanautumia isivyo sawasawa.

Tulinde maadili yetu.

Pia soma=> Mohammed Kawaida: Naipa Serikali miezi minne iwe imefungia Mtandao wa X
Nikijiungaga nikamaliza GB 20 kwa siku moja nikaufutia mbali. Siwezi kujiunga tena ever
 
Wakati wewe unauona mtandao wa Tiktok wa hovyo, kuna watu wanajifunza neno la mungu kupitia mtandao huo huo unaouona wa hovyo.

PambanaZaidi/CottonandMore
wengine wengi ndio sehemu yao ya kupata wateja wa biashara zao, watu wengine sijui wanawaza mpaka wapi yani wanajifikiria wao tu
 
Watumiaji wengi wa TikTok hawana maadili. Badala ya kumfungia mtu mmoja mmoja, ni afadhali wakafungia mtandao, hadi pale elimu itakapotolewa kuhusu matumizi ya mtandao huo.

Binafsi sina account ya mtandao lakini kwa video zinazotumwa kwenye mitandao mingine kutoka kwa watumiaji wake; inaonesha wazi watumiaji mtandao huo wanautumia isivyo sawasawa.

Tulinde maadili yetu.

Pia soma=> Mohammed Kawaida: Naipa Serikali miezi minne iwe imefungia Mtandao wa X
Maadili ni Nini?
 
Sio wote, mie simo tiki toku.
Nilishindwa, kila siku inaibuka mitandao mipya nitakuwa na akaunti ngapi, nimeshindwa kwendana na kasi ya mitandao
UZuri unaweza ingia tick tok bila kuwa na account sema tu hutaweza kupost au kucoment

Mi huwa naingia mara moja moja ila contents zao ni za hovyooo
 
Wakati wewe unauona mtandao wa Tiktok wa hovyo, kuna watu wanajifunza neno la mungu kupitia mtandao huo huo unaouona wa hovyo.

PambanaZaidi/CottonandMore
Na kuna siku atataka visu majumbani viondolewe, maana kuna watu wameuwawa kwa kuchomwa visu..!!

CC Lanlady
 
Ukweli ni kwamba kwenye mtandao wa TikTok kuna mambo mazuri ya kujifunza na kuna uchafu usiostahili.

Uamuzi ni wako unataka kuangalia nini. Mfano, kuna vitu vya maana sana nimejifunza TikTok.
Ni vyema ukaviorodhesha baadhi ya hvyo vitu ulivyojifunza mkuu. Na sisi tuone kama kuna uwezekano wa kuwepo kwny huo mtandao.
 
Mitandao haina shida.mwenye shida niwewe na akili zako.ikiwa kila mtu akitumia kitu vibaya kinakua kinafungiwa kitabski kitu gani na tutakua ni taifa la namna gani.hizi akili ndio maana vichwa vyetu vinadumaa tunakua tegemezi kwakutegemea bunifu za mataifa ya nje.Sisi tunabaki kuwaza kutumia na kufungia.badilika.
 
Watumiaji wengi wa TikTok hawana maadili. Badala ya kumfungia mtu mmoja mmoja, ni afadhali wakafungia mtandao, hadi pale elimu itakapotolewa kuhusu matumizi ya mtandao huo.

Binafsi sina account ya mtandao lakini kwa video zinazotumwa kwenye mitandao mingine kutoka kwa watumiaji wake; inaonesha wazi watumiaji mtandao huo wanautumia isivyo sawasawa.

Tulinde maadili yetu.

Pia soma=> Mohammed Kawaida: Naipa Serikali miezi minne iwe imefungia Mtandao wa X
Halafu itakuwa chawa wewe. Ambao "hawana maadili" umewaona tiktok tu? Huko mtaani kwako hawapo? Serikalini wamejaa wangapi? Huu ufisadi na rushwa zinazoendelea huzioni? Tuna balozi ngapi nchini zenye watu ambao "hawana maadili" tuwacancel wote? Baada ya kupigania mambo ya maana kazi kung'ang'ania mambo ambayo hayana msingi.

Bure kabisa wewe.... nyie ndio mnaotaliwa mlimwe ban za maisha kwa huu undezi wa kubomoa
 
Acheni unafki ...
Mbona hivyo mnavyovisema mbona mimi huwa sivionagi?

Sema unakua umechagua kuona nini!

Huko mpaka baba Paroko wako yupo...sembuse Mimi ni nani?

Wabongo tunapenda kujikweza Sana ..
Bongo tuna ujinga mwingi sana wakati hatuna kila kitu.Huo mtandao uko vizuri sana inategemea nawewe mwenyewe unachotaka kukitazama ni nini.Sasa mbongo akikutana na clip za wasasambuaji anakariri mtandao wote clip zilizoko ni hizo.
 
Back
Top Bottom