Ungeweka na option ya genge la Mafia. Sababu kupitia CCM, Tanzania ipo kwa ajili ya familia chache, kadhaa ikiongozwa na Don, underboss,capos, soldiers, associates chini kabisa wapo machawa wanatoa sifa na kudaka makombo, favour za hapana pale.
Mfumo huu upo kwa ajili ya watu wachache kule juu na familia zao, washikaji, ndugu, marafiki. Wengine wote huku chini wanafanya kazi, biashara kukusanya na kulipa kodi kwa ajili na kwa niaba ya familia chache zilizopo juu.
Mafia ni mfumo wa kibabe, usio wa kidemokrasia. Hautegemea wala kuamini katika demokrasia, uhuru, haki au uwazi kupata viongozi wa ndani na taifa. Bali unategemea maneno ya mtu mmoja mungu-mtu, Don, nguvu, vitisho, utekaji, utesaji mauaji, wizi, ujambazi, rushwa, visasi, magereza ili kuendeleza utawala wao. Ingawa hadharani wanahubiri, haki, demokrasia, uhuru, uwazi kiutendaji hawaamini katika ukweli na haki.