Napendekeza TCRA wapige marufuku matangazo ya BBC nchini Tanzania. Wameitukana kumbukumbu ya Mwl. Nyerere

Napendekeza TCRA wapige marufuku matangazo ya BBC nchini Tanzania. Wameitukana kumbukumbu ya Mwl. Nyerere

Nimetoka kushuhudia ushenzi wa hali ya ya juu toka kwa hawa muda huu. Eti wameonyesha kipindi cha historia ya ukombozi wa Afrika, ambapo wametaja wapambania uhuru kama akina Kwame Nkrumah, Patrice Lumumba na Nelson Mandela, Jomo Kenyatta miongoni mwa wengi.

Lakini cha ajabu walipofika kwenye ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika wameishia kumtaja Mandela tu na kuishia hapo. Yaani Julius Kambarage Nyerere, pamoja na mchango wake mkubwa katika ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, hajatajwa hata kwa bahati mbaya, hii maana yake nini??!

Wanasema ‘A TRUTH HALF TOLD IS A LIE’, kwa kukaa kimya ni kukubali matusi ya nguoni juu ya baba wa taifa letu. Ngoja nipunguze jazba kwanza..., daah!!!
Wewe anzisha chombo chako cha habari uanze kumtangaza mwl Nyerere.
 
Habari ni sawa na chakula mezani.

Mtazamaji/mskilizaji ataamua kuikubali au kuikataa na kukipongeza au kukidharau chanzo/chombo cha hiyo habari.

Kuwafungia hakutawazuia kuendelea kututangaza vibaya endapo wamedhamiria kufanya hivyo.
Ni wapi ambapo wamewatangaza vibaya ?
 
si hilo tu huku Tanzania utakuta kuna barabara ya sam Nojuma sijui shule Mugabe sijui chuo cha Mandela sijui barabara ya Kwame Nkurumah sasa nenda huko walikosaidiwa kupata uhuru na Tanzania hata mtaa wa Kambarage hakuna [emoji1787] tatizo sisi kiherehere,kimbelembele chetu muda wa kuijenga nchi yetu eti tunawasaidia wasio na shukrani wapate uhuru na tulikuwa tunawasongea hata ugali washibe
Hujafika South Africa wewe.

Hapa sauzi kuna barabara ya Nyerere
 
Soma kwanza 1964 mutiny kisha uongee hizo pumba. Bila huyo muingereza, nyerere si angekaa madarakani miaka 3 tu na kung'olewa.
Kwani hoja inasemaje? Mbona mnakaza ubongo bila sababu?
 
Moja ya sababu ya nchi yetu kubaki masikini ni rasilimali kubwa tulizotumia kusaidia ukombozi Afrika kitendo cha BBC kutaja historia ya ukombozi Afrika bila kumtaja Nyerere na kumtaja Kenyatta ni wazi habari yao imejaa upotoshaji
 
Moja ya sababu ya nchi yetu kubaki masikini ni rasilimali kubwa tulizotumia kusaidia ukombozi Afrika kitendo cha BBC kutaja historia ya ukombozi Afrika bila kumtaja Nyerere na kumtaja Kenyatta ni wazi habari yao imejaa upotoshaji
Tende wema nenda zako usingoje shukrani.

Tunajitia kiherehere kusaidia nchi nyingine wakati nchi yetu inapumulia mipira.

Always charity begins at home.
 
Msisubiri BBC waeleze... Kuna kipindi nilishawahi ona Mkenya akiwakusanya waAfrika Kusini akieleza namna walivyoisaidia Afrika Kusini katika mapambano yao ya kupigania uhuru, Nikabaki nasikitika tu.
Wote watakuwa mazuzu nilishangaa kwenye mazishi ya Mandela walivyokuwa wanamshangilia Obama huku wakisahau Marekani ilimhesabu Mandela kama gaidi
 
Nadhani hata sisi ndiyo tunafanya Legacy ya Mwalimu ianze kusahaulika hasa hasa kipindi hiki cha Utawala huu! Mfano haya yanayoendelea kuhusiana na uchaguzi wa mwaka huu.
Wakati Mwalimu alisimamia misingi ya Usawa na Haki za binadamu,sisi ndiyo tunazikanyaga! Alipiga vita ukabila,udini,ukanda,nk lakini haya ndiyo sasa yameshamiri awamu hii,Wakati Mwalimu alichukia Udikiteta na Uonevu,hayo ndiyo habari kwa sasa!
Sasa unafikiri kama sisi hatuenzi Legacy ya Mwalimu kwa vitendo walio nje watafanyaje?
 
Historia hubadilishwa kulingana na matakwa ya wahusika, hapa ni lazima Nyerere wamtoe maana hakuwahi wachekea wazungu, mpaka anaondoka madarakani hawakuwahi gusa raslimali zetu kama madini na nk.. hivo hawawezi muheshimisha kwa lolote hata kama anastahili.
Mwadui Williamson Diamond mines haikuguswa?
 
Sifa upewe siyo ujipe. Nimegundua tulifungiwa kwenye box kwa muda mrefu na mi FISI M, tukiwa kwenye box tuliaminishwa hayo, ya Nyerere, Nyerere, Nyerere.

Sasa ukitoka nje masikioni unasikia Nyerere, Nyerere, Nyerere. Akili ikikukaa sawa sauti zile zinapotea, ukiona husikii Nyerere, jua sasa akili iko sawa. Yani yale maluweluwe hayapo tena.

Wale walijikomboa wenyewe sio kwamba Nyerere aliwakomboa.

Nchi imekuwa ya chama kimoja muda mrefu, na stori zilikuwa hizo za ma FISI M, sasa kuna masauti mengi.

Hizo habari za Nyerere zinakosa muelekeo na support.

Tusilazimishe sifa, kama zipo zetu tutapewa, lakini tusiwalazimishe kutoa sifa kwetu, pengine hatustahili.

Ukitaka sifa za Nyerere mtafute Kabudi, mtakesha akikutajia Nyerere.
mkuu una stress sana.tulia kunywa maji mengi.
 
Back
Top Bottom