Napinga ACT-Wazalendo kushiriki kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) huko Zanzibar

Zitto hajawahi kuwa mwanasiasa, ni mfanyabiashara wa siasa. Inasikitisha Wazanzibar kumuamini mtu wa aina hii.
 
2015 Zitto ndio mpinzani pekee aliyebaki bungeni wakati wapinzani wote walipotoka kupinga dhuluma ya uchaguzi wa Zanzibar , vuta kumbukumbu .
 
Hata Mimi napinga, kwasababu ya chaguzi ndogo zitakazofanyika je hao ACT wamejiandaaje? Kupata uchaguzi wenye usawa kwenye chaguzi ndogo.
 
Pole
 
2015 Zitto ndio mpinzani pekee aliyebaki bungeni wakati wapinzani wote walipotoka kupinga dhuluma ya uchaguzi wa Zanzibar , vuta kumbukumbu .
🤣🤣

Kwa Zitto ni sawa eee?!!

Ila kwa mh.Mbowe KUIBADILI GIA ANGANI...kumchukua Lowassa na kuiparanganyisha CHADEMA asili...si SAWA ee?!!

Zitto ameangalia MBALI...RUZUKU ikiwemo....

Usajili ulee..nae Mbowe aliangalia MBALI... RUZUKU ikiwemo...
 
Wewe unazo hela za kula wenzio hawataki kuganga njaa kwa ajili ya siasa
 
Unaweza kuta Zitto kazidiwa nguvu na wakina Maalim.

Amandla...
Maalim Sharif ,
Amepima upepo
Muda na umri vimemtupa mkono,
Sharif ameona bora asitaafu siasa huku akiwa makamo wa Kwanza wa Raisi,
2025 hatakuwa na nguvu Tena,na atasitafu siasa,
2025 Zitto na chama chake ataludi Tanganyika au ACT itakuwa kabisa.
 
ACT ndo washaingia SUK tayari. Ingawa wewe si mwanachama, tambua kuwa chama hiki ni "mshirika" chama chako CDM.

Lakini kwakuwa ACT wanaungana na CCM kujenga SUK, wao sasa ni CCM-B na nyie kama washika wao mnakuwa CCM-C kwa maana rafiki wa rafiki yako naye ni rafiki yako pia. Na kama hutaki iwe hivyo, basi jilaumu kuwa chama chako kilifanya utopolo kujinasibisha na ACT ya Seif kwenye harakati za uchaguzi uliopita!

Zaidi unatakiwa kutambua ukweli mchungungu kwamba Prof. Lipumba ana misimamo inayoona mbali kwenye siasa kuliko kina Mbowe hasa pale anapojitenga na wote wanaowatanguliza mbele makada wa CCM "kupiginia upinzani". Sasa kwa maamuzi haya ya ACT yanaidhalilisha CDM pia.
 
🤣🤣
 
Unajisi mtupu! Zto alitaka "kumpindua" Mbowe kwa kutaka madaraka-uenyekiti, hivyo kwa hili waliloliamua, sishangai katu!
Naamini unaanza kuelewa kuwa Mwanasiasa hayupo kwa Maslai ya Taifa au wananchi Bali wapo kwa ajili ya madaraka au Utawala tu
 
Siasa za Tanzania ukizifuatilia sana jiandae kupatwa na Cancer ya ubongo

Wanasiasa wengi ni Yuda eskarioti Wanasumbuliwa na njaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…