Napinga Daladala kuingizwa kwenye BRT

Kwa msisitizo hizo coaster ziruhsiwe chache kila ruti na zibebe level seat tu watu wanne wanne tu bila kusimamisha abiria ili zisije kuua biashara ya daladala za kawaida ambazo ni msaada mkubwa sana kwa watu wa kipato cha chini.
 
Wewe unataka ufike kazini kwako au unataka mradi WA brt!? Zingatia Zaidi Mambo Yako acha wivu
 
Ni wazo zuri hasa kwa watumiaji wa huo usafiri angalau wapate usafiri kwa wakati kuliko huu usumbufu unaoendelea, changamoto ni usalama kupanda na kushuka kwa abiria pamoja hasa kwa muundo wa vile vituo vya mwendokasi BRT na mlango wa hizo daladala
 
Hii ndio serikali ya mama na anaupiga mwingi ila **** watu wanamuhujumu mama ili 2025 aonekane kituko. Washajua wapo na uongozi dhaifu kwanini wasiwafanyie madudu
 
Wewe unataka ufike kazini kwako au unataka mradi WA brt!? Zingatia Zaidi Mambo Yako acha wivu
Mkuu hiyo kazi sina ndio maana kila jioni ikifika huwa naenda posta ya zamani kucheki view bora kabisa ya BRT. Sasa wakiweka na daladala wataharibu
 
Hii ndio serikali ya mama na anaupiga mwingi ila **** watu wanamuhujumu mama ili 2025 aonekane kituko. Washajua wapo na uongozi dhaifu kwanini wasiwafanyie madudu
Anajihujumu mwenyewe
 
Ndio maana sipendi kufuatilia siasa za tz maana zinaniumiza kichwa tu

Wanasiasa wanawategemea sana watanzania wenye kufikiri Kama wewe kuhusiana na siasa, ndio mtaji wao mkuu.


Lakini kumbuka tu ni mambo mabaya pekee ndio yanayoumiza kichwa, mazuri yanatuliza akili na kuruhusu kichwa kufanya kazi.

Na mambo hayo mabaya hayajiondoi, kadiri uhisivyo maumivu ndivyo ari ya kuyaondoa inavyopanda na njia kuzidi kufunguka.

Siasa ndio Mfumo wa binaadam wa kulinda maslahi yake hapa duniani.
 
Ule mradi wao wanaungangania kuendesha wakati wao kuendesha
Hawawezi na hawatokuja kuweza kuendesha...wampe tu mwekezaji/mtu binafsi tu
wao wanachoweza ni kuchota mijihela na kula basi

Ova


Nionyeshe Mradi mkubwa aliowahi kupewa mwekezaji hapa Tanzania na ukafanikiwa kwa asilimia angalau 95 na wananchi wakafaidi kwa 100%??

Vinginevyo unazungumzia kubinafsisha?

Watanzania tuna kasumba chafu. Watu wanahujumu miradi ya kitaifa makusudi ili wapewe wao hiyo miradi ama wapewe udalali wa kutafuta wawekezaji ili wapate uhakika wa 10% kila Mwaka wa mavuno!

Kibaya zaidi tunalindana na kuitana Miamba vichochoroni huku nchi ikizidi kurudi nyuma badala ya kusonga mbele!

Kibaya zaidi hao wawekezaji wanaoletwa kila mara nao ni wapigaji Sawa na hao madalali wao!!

Facken kabisa!
 
Mkuu hiyo kazi sina ndio maana kila jioni ikifika huwa naenda posta ya zamani kucheki view bora kabisa ya BRT. Sasa wakiweka na daladala wataharibu
Hope watatumia mixed Lane na Sio special Lane za brt
 
Halafu kuna wapumbavu wanadai tuendeshe wenyewe bandari? DP World ije tu kwasababu hata mradi wa mabasi umetushinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…