Napinga Dkt. Harrison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Tume ya kuchunguza kufeli kwa wanafunzi wengi wa Law School

Hiyo ni kawaida sana! kwa watu km sisi!!........Hata wanasheria robo tatu walio fail wale! walisoma weeee! Darasani miaka kadhaa, lkn hawakuelewa !...wewe ni nani utuelewe sisi Manabii wa Mungu??

achia wenye uelewa waelewe! wenye masikio wasike!...usitake kujua kila kitu ....sisi De chosen few ndo tulivyo kamwe hatuwezi kujikataa!...there's no way you can take it out from Us!
hongera sana
 
Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza masuala ya Law school, ikiwemo wanafunzi wengi kufeli mitihani, anapaswa kuwa mtu Muungwana, Mtulivu, Msikivu na asiye na makuu, anapaswa kuwa mkweli, Mwakyembe hana sifa hizi.

Napinga uteuzi wa Harisson Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Tume hii kwa vile Haaminiki, si mkweli na ni mpenda sifa.

Kwa mfano, alipokuwa Mwenyekiti wa Tume ya bunge kuchunguza Richmond, katika Taarifa yake aliyoisoma bungeni ALIFICHA BAADHI YA TAARIFA ILI KUOKOA SERIKALI, maana yake ni kwamba alificha taarifa za Mhusika Mkuu wa Jambo lile na kuangushia jumba bovu wasiohusika, leo huyu awezaje kuaminika na kukabidhiwa tume nyingine? JE, SAFARI HII HATOFICHA TAARIFA ILI KUIOKOA SERIKALI?

Mwakyembe akiwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Kyela kupitia CCM, aliwaahidi watu wa Jimbo lake kwamba AMEPATA SOKO LA UHAKIKA LA MCHELE WAO NCHINI MAREKANI (ikumbukwe kwamba mchele wa Kyela ndio unaoongoza kwa utamu duniani)

Lakini hadi anang'olewa kwenye ubunge hakuwahi kusaidia hata kilo 10 za mchele wa Kyela kuuzwa Marekani, Mtu kama huyu hastahili kuaminiwa kuongoza tume yoyote ile.

UNAPODANGANYA NYUMBANI KWENU HUWEZI KUAMINIKA UGENINI.

Harrison Mwakyembe ni mtu aliyejaa dharau kubwa sana , huyu hawezi kuwatendea haki watu wenye digrii moja wanaopigania haki yao ya matokeo.

ALIWAHI KUKATAA MASWALI KWAO KYELA kwa kisingizio kwamba wanaomhoji ni Darasa la 7, wakati yeye anamiliki digrii 4 na kwamba watu wasio na elimu wanachopaswa kumhoji ni kuhusu kama hawana hela mifukoni mwao na labda awasaidie. Huyu hafai kuongoza Tume ya kufuatilia haki popote duniani.

Tunamuomba Waziri wa Sheria ATENGUE HARAKA UTEUZI WAKE.

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO.
Hii cotation ya mwisho ni kauli mbiu ya CCM "NITASEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO" kwani nawe ni miongoni mwao au ndio unamsagia kunguni Mwakyembe?
 
Sasa kwa kumbukumbu zako uliwahi kuona Mwanaccm yeyote akiongea ukweli ?
 
hiyo first degree waliipataje?kama ndo hivyo basi tuchunguze na hivyo ndaki za vyuo vikuu vinavyotoa hizo degree.kingereza kwangu si ajenda kwani kuna nchi nyingi duniani haziongei hiyo lugha hasa ukizingatia karne hii yenye utandawazi mkubwa.mtu yeyote anayetaka kujifunza hiyo lugha ataijua tu kama akina diamond,harmonize na wasanii wengine wanaongea lugha hiyo walisoma wapi?ndo maana kuna mjadala wa vyuo vikuu kufundisha kwa lugha ya kiswahili.hii itawasaidia wengi kumudu masomo yao.hata nyie mnaotetea hiyo lugha ni sababu tu wazazi wenu walipata fursa serikalini wakakwapua mali za walalahoi na kuwapeleka shule za kiingereza vinginevyo na nyie hamngekuwa fluent ktk lugha hiyo.
Hata mimi, I don't give a damn about English... English as English, as Language, YES! I don't care!

Hata hivyo, usichanganye kati ya "sisi" na hizo nchi nyingi duniani wasioongea English kwa sababu wao tayari wameshachagua kinadharia kutoongea English na kivitendo kutotumia English wakati sisi tumechagua kinadharia kuongea English na kivitendo kutumia English"... sijui nimeeleweka!!

Na kwavile tumeshachagua kivitendo kutumia English pasi na sababu za msingi, basi linapokuja suala la law, hapo huwezi kuipuuza English, na naweza kusema law ni miongoni mwa fields chache ambazo ndo zinahitaji hasa uelewa mkubwa wa English pengine kuliko hata yule anayesoma Bachelor of Arts in English yenyewe!!

Ukitaka kujua ujinga wa English na Sheria, maneno kama "may" na "shall" tu yameshawahi kuleta mijadala mikubwa sana ya kisheria hata huko kwa native English speakers wenyewe!!

That's Law!

Nikirudi kwenye hoja ya Erythrocyte, nakubaliana nae yote aliyoongea kuhusu Mwakyembe...

Mwakyembe ni mwongo, mjivuni, ana kiburi, ana dharau... in short ana sifa zote zinazom-disqualify sio tu kuongoza tume kama hiyo bali hata kuwemo kwenye tume yenyewe!

Hili la matokeo ya LST sijalifuatilia manake nalisikia tu juu juu! Hata hivyo, sitaki kuwa mnafiki bhana!! Pale LST wakiamua kuwa "fair" wallah nakuambia wengi lazima watafeli...

Ni bahati mbaya sana hivi sasa Law watu wanaichukulia poa sana lakini law isn't for everybody... sio tu Tanzania bali duniani kote!! People love law but law has no affection to anybody!!

Sio kwamba eti Sheria ni ngumu ile mbaya... hell no but REAL Law is more than having your LLB transcript typed with First Class hata kama ni First Class halali kabisa ingawaje hizi za siku hizi, ah... acha tu nikae kimya!!

Wapenzi wa legal drama wanamfahamu vizuri sana Mike Ross wa Suits ambae sifa yake kuu ni uwezo wa kukariri... yaani ana photographic memory!

Uwezo wa kukariri ni muhimu sana kwenye law, YES... ni muhimu but when it comes to a REAL LAW, hii ni zaidi ya uwezo wako wa kukariri bali kuwa na uelewa wa kivitendo na jinsi ya kukitumia kwenye real world kile ulichokariri... yaani a practical understanding and application in the real world!!

By REAL LAW above ndo namaanisha hayo mambo mawili.... uwezo mkubwa wa kukariri na practical understaning and application ya kile ulichokariri!!

Na kwa jinsi ninavyofahamu, lengo kuu la LST ni kutengeneza combination ya mambo hayo makuu mawili coz' Kwenye mifumo yetu ya elimu, uwezo wako mkubwa wa kukariri unaweza kukupa First Class ya LLB lakini ukifika LST unaweza kukwama kama huna practical understanding ya yale unayokariri.

Ni kutokana na ukweli huo mchungu ndo maana watu kama akina Tundu Lissu wanapatikana kwa uchache sana kwenye ulimwengu wa kisheria!

Amini amini nawaambia, sometimes watu wanaamua tu kwamba "ah, wapeni tu bhana hao watoto" lakini na dunia yetu hii inayokuwezesha ku-bet hata ukiwa kitandani, huku upande mwingine ukisubiria kuwa bilionea kupitia Kalynda, nyie... LST wakiamua kukaza basi misiba kama hii itakuwa jambo la kawaida tu....
 
Na kupitia LST kuna kina Tundu Lissu wengi tu wanapotea/wanapotezwa, yaani Sheria inakosa utamu na utaalamu wa wakina Tundu Lissu sababu ya siasa inayozungumzwa hapa, ubanaji. Kwa jinsi TAL au Kibatala walivyo mahiri kwenye sheria lingekuwa ni jambo linalotegemewa na kila mtu, wanasheria hao kufika LST kufundisha wanafunzi kwenye hizo ziitwazo semina ili kuwapa uzoefu wa uhalisia wa sheria katika matumizi (practice), lakini HAWAJAWAHI kuitwa kufundisha (sijui kwa sababu ni wana-CHADEMA) na wanaokuja na kufundisha ni watoto wa maprof wa UDSM na wengine wasio na rekodi yoyote ya kuigwa kwenye sheria (kina Chuwa) zaidi ya kuwa na sifa ya kufelisha wanafunzi.

Ni kweli sheria sio ni ya kila mtu, ila mwamuzi inapaswa iwe no sheria yenyewe na sio mtu mwingine tu (mwalimu na usahishaji wake). Transparency inapaswa kuwepo kwenye kila kitu hapo LST
 
Na kwa jinsi ninavyofahamu, lengo kuu la LST ni kutengeneza combination ya mambo hayo makuu mawili coz' Kwenye mifumo yetu ya elimu, uwezo wako mkubwa wa kukariri unaweza kukupa First Class ya LLB lakini ukifika LST unaweza kukwama kama huna practical understanding ya yale unayokariri.
Hili linaleta ukakasi kidogo, maana kama LLB unafundishwa theory na kukariri na kufaulu, unashindwaje kukariri hizo theory ziitwazo practice pale LST na kuziandika vivyo hivyo na kufaulu?? Ingekuwa mtu akitoka LLB anafika LST na kupewa mitihani pasipo kufundishwa (kama ilivyo CPA nk) walau ingeweza kuwa ni hoja kuwa alichofundishwa LLB ni chepesi au amekuja empyt, lakini kwa kuwa LST wanafundisha kwanza kabla ya mitihani, na mitihani wanatunga kutoka walichokifundisha, huwezi kusema kuwa watu watashindwa kukariri au useme kuwa shida ni LLB!
 
Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza masuala ya Law school, ikiwemo wanafunzi wengi kufeli mitihani, anapaswa kuwa mtu Muungwana, Mtulivu, Msikivu na asiye na makuu, anapaswa kuwa mkweli, Mwakyembe hana sifa hizi.

Napinga uteuzi wa Harisson Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Tume hii kwa vile Haaminiki, si mkweli na ni mpenda sifa.

Kwa mfano, alipokuwa Mwenyekiti wa Tume ya bunge kuchunguza Richmond, katika Taarifa yake aliyoisoma bungeni ALIFICHA BAADHI YA TAARIFA ILI KUOKOA SERIKALI, maana yake ni kwamba alificha taarifa za Mhusika Mkuu wa Jambo lile na kuangushia jumba bovu wasiohusika, leo huyu awezaje kuaminika na kukabidhiwa tume nyingine? JE, SAFARI HII HATOFICHA TAARIFA ILI KUIOKOA SERIKALI?

Mwakyembe akiwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Kyela kupitia CCM, aliwaahidi watu wa Jimbo lake kwamba AMEPATA SOKO LA UHAKIKA LA MCHELE WAO NCHINI MAREKANI (ikumbukwe kwamba mchele wa Kyela ndio unaoongoza kwa utamu duniani)

Lakini hadi anang'olewa kwenye ubunge hakuwahi kusaidia hata kilo 10 za mchele wa Kyela kuuzwa Marekani, Mtu kama huyu hastahili kuaminiwa kuongoza tume yoyote ile.

UNAPODANGANYA NYUMBANI KWENU HUWEZI KUAMINIKA UGENINI.

Harrison Mwakyembe ni mtu aliyejaa dharau kubwa sana , huyu hawezi kuwatendea haki watu wenye digrii moja wanaopigania haki yao ya matokeo.

ALIWAHI KUKATAA MASWALI KWAO KYELA kwa kisingizio kwamba wanaomhoji ni Darasa la 7, wakati yeye anamiliki digrii 4 na kwamba watu wasio na elimu wanachopaswa kumhoji ni kuhusu kama hawana hela mifukoni mwao na labda awasaidie. Huyu hafai kuongoza Tume ya kufuatilia haki popote duniani.

Tunamuomba Waziri wa Sheria ATENGUE HARAKA UTEUZI WAKE.

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO.
Ukweli mchungu ni kwamba hatotenguliwa na hiyo ndo CCM
 
Sas

Sasa wajameini kumfichia aibu Boss wako kuna Ubaya gani??....kwa sababu alimpenda Boss wake kwanini amgalagaze hovyo?? kwani yeye hana akili??........ni sawa na Baba yako akijamba sebureni eti unacheka...ni laana hiyo!!

Mtoto mdogo wa Nuhu alipo muona Babake uchi alicheka kwa raha na haki zake zoote! akalaaniwa kizazi chake choote mpaka leo bila shaka weye ni kizazi hiko!!

Kumtunzia Boss wako heshima ni Baraka kubwa sana! usijidanganye ndo maana anapeta mpaka leo!! waleee wasema hovyo km Jiwe, Msiba, Makonda wako wapi leo??

Shetani alidai haki Mbinguni na kumsema Mungu eti ana madaraka makubwa, akayatamani leo hii tunasota nae humu mbinguni hatii mguu tena!...anasubiri kupigwa kiberiti! kwani mkubwa hakosei??

wewe hapo hujawahi kukosea....sikia sasa kukosea ni ubinadamu siyo suala la kushikia kidedea! mtu mwingine! unasikia! tena amabaye hakosei ndo hatari zaidi! ya dikteta!!

Drs la saba kuambiwa hivo kuna ubaya gani kwani?? si ndivo walivyo? au!!.......kwani drs la saba ni matusi??...au weye hukupitia huko? uliruka?? basi km ni hivo rudi ukalisomee!.....

kwani kusema ana degree 4, ni tusi?? si ndo alivyo?? na ukweli wenyewe au!! ....kwani kusema nimesoma kihalali ni dhambi/kuvunja katiba?? ya wapi??...wewe ni dhaifu sana!....unataka aambiwe ana vyeti fake! ndo ufurahie au!!

kifupi wee mzee acha chuki za kimusoma musoma ndo maana nyie waruri wachawi sana! mnamsema mutu mpaka anakufa?? sasa nani msafi aende sasa??!!

nenda weye basi make weye! huna dhambi! wkt unaiba mifugo kila siku, tunawajua wote bana! mliiba mifugo ya mbunge Mathayo.... uongo???
Kwahiyo bora umfichie siri boss wako aliye na hatia kumsingizia asiye boss wako asiye na hatia?
 
Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria awa mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa shule iliyo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria - atakiwa kuja na ripoti huru.
Vichekesho
 
Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza masuala ya Law school, ikiwemo wanafunzi wengi kufeli mitihani, anapaswa kuwa mtu Muungwana, Mtulivu, Msikivu na asiye na makuu, anapaswa kuwa mkweli, Mwakyembe hana sifa hizi.

Napinga uteuzi wa Harisson Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Tume hii kwa vile Haaminiki, si mkweli na ni mpenda sifa.

Kwa mfano, alipokuwa Mwenyekiti wa Tume ya bunge kuchunguza Richmond, katika Taarifa yake aliyoisoma bungeni ALIFICHA BAADHI YA TAARIFA ILI KUOKOA SERIKALI, maana yake ni kwamba alificha taarifa za Mhusika Mkuu wa Jambo lile na kuangushia jumba bovu wasiohusika, leo huyu awezaje kuaminika na kukabidhiwa tume nyingine? JE, SAFARI HII HATOFICHA TAARIFA ILI KUIOKOA SERIKALI?

Mwakyembe akiwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Kyela kupitia CCM, aliwaahidi watu wa Jimbo lake kwamba AMEPATA SOKO LA UHAKIKA LA MCHELE WAO NCHINI MAREKANI (ikumbukwe kwamba mchele wa Kyela ndio unaoongoza kwa utamu duniani)

Lakini hadi anang'olewa kwenye ubunge hakuwahi kusaidia hata kilo 10 za mchele wa Kyela kuuzwa Marekani, Mtu kama huyu hastahili kuaminiwa kuongoza tume yoyote ile.

UNAPODANGANYA NYUMBANI KWENU HUWEZI KUAMINIKA UGENINI.

Harrison Mwakyembe ni mtu aliyejaa dharau kubwa sana , huyu hawezi kuwatendea haki watu wenye digrii moja wanaopigania haki yao ya matokeo.

ALIWAHI KUKATAA MASWALI KWAO KYELA kwa kisingizio kwamba wanaomhoji ni Darasa la 7, wakati yeye anamiliki digrii 4 na kwamba watu wasio na elimu wanachopaswa kumhoji ni kuhusu kama hawana hela mifukoni mwao na labda awasaidie. Huyu hafai kuongoza Tume ya kufuatilia haki popote duniani.

Tunamuomba Waziri wa Sheria ATENGUE HARAKA UTEUZI WAKE.

NITASEMA KWELI DAIMA FITNA KWANGU MWIKO.

Ana upeo mdogo, anapaparika, he has never been objektive, anaongozwa na mihemuko yake kufanya maamuzi.
 
Hili linaleta ukakasi kidogo, maana kama LLB unafundishwa theory na kukariri na kufaulu, unashindwaje kukariri hizo theory ziitwazo practice pale LST na kuziandika vivyo hivyo na kufaulu?? Ingekuwa mtu akitoka LLB anafika LST na kupewa mitihani pasipo kufundishwa (kama ilivyo CPA nk) walau ingeweza kuwa ni hoja kuwa alichofundishwa LLB ni chepesi au amekuja empyt, lakini kwa kuwa LST wanafundisha kwanza kabla ya mitihani, na mitihani wanatunga kutoka walichokifundisha, huwezi kusema kuwa watu watashindwa kukariri au useme kuwa shida ni LLB!
You got me wrong....

SIO wanafundishwa kukariri bali unatakiwa kuwa na uwezo wa kukariri kwa sababu sheria ina mambo mengi mno! Sheria inakuwa na reference nyingi mno!

Sasa kukariri hayo mambo ni jambo moja na kujua ku-apply ulichokariri ni jambo lingine.

Chukulia Wakili kwa mfano.

Wakili anapokuwa mahakamani pale anakumbana na legal battle vs watalaamu wenzake!

Kwahiyo hata kama kipawa cha kukariri unacho, unaweza kupigwa KO ukiwa field kwa sababu pale is more than what you've bali unavyoweza kukitumia ulichokariri kwa kujenga hoja za kisheria katika ku-attack na ku-counter attack hoja za upande upili.
 
Na kupitia LST kuna kina Tundu Lissu wengi tu wanapotea/wanapotezwa, yaani Sheria inakosa utamu na utaalamu wa wakina Tundu Lissu sababu ya siasa inayozungumzwa hapa, ubanaji.
Hayo ya kubana siwezi kuyazungumzia... inawezekana ni kweli kuna siasa za kukomoana au hisia zetu. Hata hivyo, mie nazungumzia malengo ya LST ambayo ni kuwapata akina Tundu Lissu wenye uwezo wa kujenga hoja za kisheria.

Sehemu kama zile wanajikita kwenye PRACTICAL Legal Training.
Kwa jinsi TAL au Kibatala walivyo mahiri kwenye sheria lingekuwa ni jambo linalotegemewa na kila mtu, wanasheria hao kufika LST kufundisha wanafunzi kwenye hizo ziitwazo semina ili kuwapa uzoefu wa uhalisia wa sheria katika matumizi (practice), lakini HAWAJAWAHI kuitwa kufundisha (sijui kwa sababu ni wana-CHADEMA) na wanaokuja na kufundisha ni watoto wa maprof wa UDSM na wengine wasio na rekodi yoyote ya kuigwa kwenye sheria (kina Chuwa) zaidi ya kuwa na sifa ya kufelisha wanafunzi.
Hilo nakubaliana na wewe lakini kubwa zaidi, sehemu kama zile sio tu kuwa na Ma-Professor kama akina Kabudi bali watu wenye field experience.

Sasa kama wamejaza ma-Academician watupu wasio na field experience, basi hilo ni tatizo lakini siwezi kulisemea sana kwa sababu sina uhakika.
Ni kweli sheria sio ni ya kila mtu, ila mwamuzi inapaswa iwe no sheria yenyewe na sio mtu mwingine tu (mwalimu na usahishaji wake). Transparency inapaswa kuwepo kwenye kila kitu hapo LST
Hapa sina cha kusema kwa sababu sifahamu ukweli wa kinachoendelea huko!!

Najiepusha kutumia mihemuko kwa sababu Wanafunzi wanaolalamika wanaweza kuwa sahihi au LST wanaweza kuwa sahihi!
 
Na kweli usitumie mihemko, tumia akili yako. Wanafunzi wanalalamika kufelishwa, LST wanasema hawamfelishi mtu bali wanafunzi wana uwezo duni kiakili. Wanafunzi wanasema basi turudishiwe booklet zetu tuone hayo madudu tuliyoandika na pia tuone usahishaji ulivyofanyika, LST wanasema uliwahi kuona wapi (chuo gani) mwanafunzi anarudishiwa booklet? Wanafunzi, kwa mujibu wa sheria za LST, ukataji wa rufaa ni kwa sababu yeyote inayohusisha USAHISHAJI MBAYA WA MTIHANI au UJUMLISHAJI MBAYA WA MAKSI, sasa chochote katika hivyo huwezi kuvijua bila kuona booklet, na sheria ndogo ya LST inaruhusu mwanafunzi kuhakiki maksi zake, tunaomba booklet tujihakikishie kufeli kwetu, LST - Hapana, booklet haziwezi kurejeshwa..

Sasa hapo LST wanakuwaje sahihi kusema kuwa wanafunzi wana uwezo duni? Wanafunzi wanasema mchawi usahishaji, leta booklet imalize fitna, LST hawataki
 
Hayo ya kubana siwezi kuyazungumzia... inawezekana ni kweli kuna siasa za kukomoana au hisia zetu. Hata hivyo, mie nazungumzia malengo ya LST ambayo ni kuwapata akina Tundu Lissu wenye uwezo wa kujenga hoja za kisheria.
Hoja za kisheria ndio kama hizo, mitihani ya LST inatoka bila mwanafunzi kufundishwa?? Kama jibu ni ndiyo iweje ashindwe kukariri ilhali aliweza kwenye LLB?

Hoja nyingine, je, booklet zinaruhusiwa kuhakikiwa au la? Kama jibu ni Ndiyo, je LST wanatekeleza takwa hilo? Wanawapa wanafunzi booklet wazihakiki?

Hoja ya tatu, unaweza kukata rufaa kwa kusema maksi zako hazijajumlishwa au kusema mtihani wako umesahishwa vibaya ilhali hujaona booklet? Hauoni ni kama utakuwa unaagua kiganga?

Hizi zinapaswa kuwa HADIDU ZA REJEA kwa hiyo Kamati HURU ya uchunguzi
 
Wakili anapokuwa mahakamani pale anakumbana na legal battle vs watalaamu wenzake!
Legal battle ya mahakamani haitokei kama jambo la kushtukiza, ni mambo ya maandalizi kabisa, hayo ndiyo yanayofanya mmoja awe wakili mzuri kuliko mwingine, ni namna ulivyojiandaa kukabiliana na jambo ambalo lipo mezani tayari linajulikama. Ni tofauti na mitihani, ambayo yenyewe maswali yanakuja kwa kushtukiza, hapo ndipo mwanafunzi hutumia kumbukumbu zake alizokariri na kuelewa kuziweka katika majibu ya maswali. Mahakamani kinachofanyika ni umahiri wa wakili kutafsiri sheria tofauti na mpinzani wake, sheria ni hiyohiyo ila tafsiri zimekuwa tofauti, sasa mnaomba mahakama itoe tafsiri sahihi.

Kwa hiyo kwenye uhalisia, mahakamani ni kurahisi sana kuliko shuleni kwa kuwa muda wa maandalizi huwa ni mkubwa, na jambo ni la wazi. Huwezi kumnyima ufaulu mwanafunzi kwa makusudi kwa hofu yako kuwa hatakuwa wakili mzuri baada ya kufaulu, mtu apewe kilicho halali, afaulu ama afeli kwa uhalali
 
Wakati wewe unajiandaa na wenzako pia wanajiandaa.

Hayo mambo ya kwamba wameonewa au hapana, narudia... siwezi kuyaongelea, lakini kwavile wewe unaamini wameonewa; je unaweza kutuambia unatumia vigezo gani ku-conclude kwamba wameonewa?

Je, umepitia papers za hao wote walioonewa?! Na wameonewa kwa sababu zipi?

Kwavile ulizungumzia suala la siasa, je unataka kutuambia hao wote ni wafuasi wa upinzani au unamaanisha nini hasa?!
 
Back
Top Bottom