Umeshaambiwa ...Sheria inawawaruhusu ...Consider use of experts na inafanyika!CAG ametoa riport nzuri na kuibua matumizi mabovu na yasiyo na tija katika taasis za Serikali , ambapo wa kulaumiwa ni watu wa chini Sana wa hayati Rais Magufuli, hata leo unaweza kukuta watu wamefanya matumizi mabovu ya serikali na sitegemei Rais Samia kuwa na macho 10000 kumulika kila level na kuona kila Baya huku chini, mifumo ni mibovu Sana.
Tuende kwenye mada yangu, Mradi wa umeme wa maji ni mradi ambao unaweza kupunguza Bei ya umeme na uwekezaji wake unatumia pesa nyingi kwa Mara ya kwanza lakini baada ya hapo ngarama za uendeshaji ni ndogo Sana pamoja na matengenezo, mfano kila Mwezi mitambo ya gesi ya kinyerezi unatumia takriban bil 4 za matengenezo/maintenance ambapo ukilinganisha na mtambo wa kidatu wa maji hata milioni 100 haifiki.
Point yangu ni kuwa CAG nataka kujua ametumia wataalamu gani wa HEP kuweza kujua kuwa upembuzi wa mwaka 1970 haufai, ofisi yake Haina wataalamu hao, na TANESCO walishathibitisha kuwa upembuzi ule bado ungeweza kufanya kazi Hadi leo, kwanza niwaambie, katika mito yote nchini Tanzania hakuna mto wenye maji mengi kushinda ama kukaribia RUFIJI river inapojengwa stiglers , Sasa mtasemaje kwamba hauwezi kuzalisha umeme wa kutosha.
Mi ningeomba wataalamu wa Rufiji basin, tanesco Na wengine wake waongelee Hilo suala sio kila kitu kupinga. Huu mradi una manufaa Tanzania mto ule ndo una maji mengi kuliko yote mlitaka tujenge bwawa wapi?
Hapa CAG Kama unataka tuende kwenye Gesi ambayo ni yetu lakini tunauziwa sawa, TPDC anauziwa Gesi na makampuni ya nje yanayochimba Gesi kwetu halafu wao wanawauzia tanesco kuzalisha umeme, kwa bei kubwa mno, Stiglers tu ndo inaweza kuikomboa tanesco Na watanzania, haya magesi ya muhongo hayafai.
Kuhusu Mto Rufiji...ndugu acha ushabiki.Hivi unajua mabadilliko ya tabia nchi yalitikea bonde la mto Rufiji miaka ya hivi karibuni!
Unafahamu ni mito mingapi inayotiririsha maji bobde la Mto Rufiji kwa Sasa ukilnganisha na miaka ya 1970s
Kama ni kweli walitumia Upembuzi wa mwaka 1970 ,Basi ttusubiri kuwekwa kwenye kumbukumbu za Dunia za maamuzi ya kipumbavu!