Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

Story yako haina uhusiano wowote na huu uzi.
Ungeinzishia uzi wake tofauti.
 
Wajinga kama hao wapo. Hata ufanye vipi watakiuka taratibu. Yule mama angepiga simu kwenye taasisi inayohusika na usafiri ili wawachukulie hatua. Namba hizi zinatakiwa kuwepo kwenye mabasi yote.

Amandla...
 
Pamoja na kwamba haya uliyoandika hapa ni kweli, inabidi kufahamu pia kwamba kama msafiri anatiketi ya shirika la ndege linaloanzia safari zake Arusha, ni lazima aende Arusha akitokea Moshi katika safari yake ya kwenda Dar es Salaam, iwapo shirika hilo halina kibali cha safari zake kuondokea au kupitia KIA. Hali ni hivyo hivyo kwa mashirika yote ya ndege duniani. Ukisafiri na Emirates, KLM au Delta ,n.k., utalazimika kwenda kwenye 'hubs'zao, kabla hujaunganisha kwenda miji mingine isiyohudumiwa na mashirika hayo moja kwa moja.
 
Story yako haina uhusiano wowote na huu uzi.
Ungeinzishia uzi wake tofauti.
Hapana mkuu 'Yoda', hiyo stori yake inao uhusiano muhimu sana na mada hii. Hebu itafakari vizuri, uhusiano huo utauona tu!, uko wazi kabisa.
 
Nasikia bodaboda, bajaji na taxi zote ni za viongozi.
 
Akili zimeingia kichwani kufahamu kwamba mtu aliyejitambulisha kuwa ni wa 'wanyonge' hayupo tena; kwa hiyo hata hao wenye njaa zao sasa wanaweza kukoroma watakavyo.
 
Hili jambo linatakiwa kupigiwa kura ikiwezekana utaratibu huu ulalamikiwe kila unapotumika, ni utaratibu kandamizi, wanaoteseka ni watu wa kipato cha chini, akina mama, watoto, walemavu nk. Kilio hiki kifikishwe kwa Rais.
 
Nasikia bodaboda, bajaji na taxi zote ni za viongozi.
Ni kweli, viongozi wengi ndiyo wenye bajaji, taxi, pikipiki na daladala, utaratibu wa kuwalazimisha abiria kushuka stand kuu za miji unalenga kunufaisha biashara zao na siyo vinginevyo

Wao wanatakiwa kuiachia nguvu ya soko ifanye kazi badala kuwabaka wananchi kiuchumi
 
Nasikia bodaboda, bajaji na taxi zote ni za viongozi.
Pale Iringa zilitajwa daladala kadhaa kuwa ni za DC, zingine Mkurugenzi, zingine RC na ndiyo maana suala la kushukia stand linashupaliwa sana, ili kulazimisha biashara ya daladala, bajaji na pikipiki
 
Subirini dawa iwaingie.
 
Duuh Mzee leo umejilipua!
 
Utopolo mtupu.
Fahamu Asilimia 90 ya wasafiri wanoutumia mabasi ni wanyonge ambao Kondakta akisahau kurudisha hata buku ya chenji zitawaka ndani ya gari.

Huo unyonge umejitia mwenyewe yale maneno yaliokuwa yanaandikwa kwenye mabus sasa yabebe maana halisi huwezi kusema unatoa semi luxury au luxury services halafu usiwe na shuttle buses !
Duniani hatufanani na hatutakuja kufanana kila mtu atasafiri kwa namna atakavyoweza (afford) .
Watu walisafiri na kwenda kulala kwa mjomba siku moja kabla ili kuwahi treni! Lakini pia kila maendeleo yanagharama
 
Mkuu wa Mkoa kachemka pakubwa Sana tena
 
Sure
 
Ni kweli. Lakini hapa tunasema wewe unaongea vile ilipaswa kuwa, sivyo ilivyo. Makalla angekuwa sahihi kama angefanya utafiti na kutoa suluhisho lisilowaumiza wadau. Aweke miundombinu sahihi kati ya kituo hiki kikuu na maeneo ya jiji. Kwa mfano, mimi ningefurahi kama mwendokasi ingeungwa moja kwa moja pale kituoni. Mgeni unadrop na kuingia mwendo kasi. Kwa hali ilivyo sasa, pale kituoni ni adhabu wallahi. Ile kushuka mpka upate daladala, unajuta kuja Dar!
 
Watu wa dar mnadeka sana asee, nimepita njombe utaratibu ni kushuka na kupakilia stand, Iringa hivyo hivyo, Singinda uwo uwo hata ka mji ka musoma utaratibu ni huo huo, inakuaje dar mnalalamika hivo? Stand imejengwa kwa mabilioni itumike ipasavyo
 

Maendeleo yana ghalama yake, Isipotumika hzo changamoto za usafiri zitatatuliwa vipi?Ata ubungo huko awali haikua karibu na mji kama ilivyo leo
 

Kwa nn msiwapigie kelele wamiliki wa mabus wawe na coaster za kuwasogeza abilia maeneo ya mjini wanapowashusha usiku?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…