Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Rudia ulichoandika. Inawezekana ulichoandika sicho ulichomaanisha.😬
Rudia kusoma nilichoandika, naona umekuja na povu pasi kuelewa.
Amandla..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rudia ulichoandika. Inawezekana ulichoandika sicho ulichomaanisha.😬
Rudia kusoma nilichoandika, naona umekuja na povu pasi kuelewa.
Tunaweza mlaumu sana Mheshimu mkuu wa mkoa lakini kumbe anamefanya hivyo kwa kushughulikia matatizo ya wananchi. Juzi nilikuwa nasafiri toka Arusha kisha nikapanda basi nisingependa kulitaja basi hili lina stand binafsi jirani Ubungo, tulipofika Bomang'ombe akapanda abiria wakati akipanda huyo abiria ni mama pamoja na wanaye wawili alidai yeye kwamba yeye anashukia mbezi. Konda akamwambia umefika mama. Tulipofika msata gari ikafuata barabara ya Bagamoyo. Yule mama akakumbusha konda sisi tunashuka mbezi hii gari mbona inapita huku. Konda akamwambia si unataka mbezi stendi kuu utafika mama. Tulipofika kwenye stendi ya basi husika maeneo ya Shekilango yule konda alimkabidhi yule mama Tsh 2000 akimwambia chukua daladala panda utafika mbezi mama akagoma akasema yeye hawezi kuanza kuhangaika na mizigo kupanda daladala. Baadhi ya abiria wakawa waungwana kumtetea mama kwamba mama alikwisha toa taarifa tangu anapanda kwenye gari kwamba yeye anaenda mbezi na si Shekilango kwa hiyo ni swala la kumuwezesha afike alikosema anakwenda.
Bahati nzuri akajitokeza abiria mmoja aliyekuwa amepokelewa na ndugu yake usafiri binafsi akamwambia mama nitakusaidia kukufikisha Mbezi panda kwenye hiyo gari mzozo ukawa umeisha. Mimi nilikuwa nimeazimia kwamba sitoki pale mpaka mama amepata msaada naye ameridhika.
Wajinga kama hao wapo. Hata ufanye vipi watakiuka taratibu. Yule mama angepiga simu kwenye taasisi inayohusika na usafiri ili wawachukulie hatua. Namba hizi zinatakiwa kuwepo kwenye mabasi yote.Tunaweza mlaumu sana Mheshimu mkuu wa mkoa lakini kumbe anamefanya hivyo kwa kushughulikia matatizo ya wananchi. Juzi nilikuwa nasafiri toka Arusha kisha nikapanda basi nisingependa kulitaja basi hili lina stand binafsi jirani Ubungo, tulipofika Bomang'ombe akapanda abiria wakati akipanda huyo abiria ni mama pamoja na wanaye wawili alidai yeye kwamba yeye anashukia mbezi. Konda akamwambia umefika mama. Tulipofika msata gari ikafuata barabara ya Bagamoyo. Yule mama akakumbusha konda sisi tunashuka mbezi hii gari mbona inapita huku. Konda akamwambia si unataka mbezi stendi kuu utafika mama. Tulipofika kwenye stendi ya basi husika maeneo ya Shekilango yule konda alimkabidhi yule mama Tsh 2000 akimwambia chukua daladala panda utafika mbezi mama akagoma akasema yeye hawezi kuanza kuhangaika na mizigo kupanda daladala. Baadhi ya abiria wakawa waungwana kumtetea mama kwamba mama alikwisha toa taarifa tangu anapanda kwenye gari kwamba yeye anaenda mbezi na si Shekilango kwa hiyo ni swala la kumuwezesha afike alikosema anakwenda.
Bahati nzuri akajitokeza abiria mmoja aliyekuwa amepokelewa na ndugu yake usafiri binafsi akamwambia mama nitakusaidia kukufikisha Mbezi panda kwenye hiyo gari mzozo ukawa umeisha. Mimi nilikuwa nimeazimia kwamba sitoki pale mpaka mama amepata msaada naye ameridhika.
Pamoja na kwamba haya uliyoandika hapa ni kweli, inabidi kufahamu pia kwamba kama msafiri anatiketi ya shirika la ndege linaloanzia safari zake Arusha, ni lazima aende Arusha akitokea Moshi katika safari yake ya kwenda Dar es Salaam, iwapo shirika hilo halina kibali cha safari zake kuondokea au kupitia KIA. Hali ni hivyo hivyo kwa mashirika yote ya ndege duniani. Ukisafiri na Emirates, KLM au Delta ,n.k., utalazimika kwenda kwenye 'hubs'zao, kabla hujaunganisha kwenda miji mingine isiyohudumiwa na mashirika hayo moja kwa moja.Usafiri wa ndege hivyo hivyo. Ukiwa arusha unaweza kuondokea Arusha Airport au KIA. Hauambiwi kuwa kwa sababu ulipandia Arusha Airport lazima upitie KIA. Kuna ndege za KIA na ndege za Arusha. Aidha sio kweli kuwa hauwezi kwenda nje ya nchi bila kupitia JKNIA. Unaweza kuanzia safari KIA au Zanzibar bila kushuka JKNIA. Miji mikubwa kama London, New York n.k. wana viwanja vya ndege zaidi ya kimoja ambavyo mtu unaweza kuondokea.
Hapana mkuu 'Yoda', hiyo stori yake inao uhusiano muhimu sana na mada hii. Hebu itafakari vizuri, uhusiano huo utauona tu!, uko wazi kabisa.Story yako haina uhusiano wowote na huu uzi.
Ungeinzishia uzi wake tofauti.
Nasikia bodaboda, bajaji na taxi zote ni za viongozi.Huyu mkuu wa mkoa amecopy upuuzi wa Dodoma,
Dodoma Kuna amri basi lolote hata lifike saa 8 usiku Dodoma,lazima lishushe abiria wote stand kuu,hakuna kuwapa msaada abiria wanaoenda mjini Kati Kati,basi lishushe,harafu liende tupu mjini kupaki,
Kisa wanataka abiria wanaoenda mjini,watumie usafiri mwingine wa boda boda,teksi,lengo ilikuwa ni kulazimisha abiria wapande boda boda,teksi kwenda mjini
Dodoma daladala mwisho saa nne usiku,unafika Dodoma saa Saba usiku,uchukue boda boda mpaka mjini,ulipe Tena 15000!akili za hovyo kabisa
Akili zimeingia kichwani kufahamu kwamba mtu aliyejitambulisha kuwa ni wa 'wanyonge' hayupo tena; kwa hiyo hata hao wenye njaa zao sasa wanaweza kukoroma watakavyo.Naona leo mzee wangu umeamua KUMFOKEA MTU!!, tatizo la viongozi wetu huwa wanapenda huifurahisha hadhara inayomsikiliza kwa mtu huo bila kutafakari hizo kauli zao ki mantiki!!siku hizi kuna mabasi yanaanzia safari zao , kigamboni, mbagala hadi chanika, hivyo asubuhi inakuwa rahisi kwa abiria wa maeneo hayo kuanza safari, na hata ile usiku wanapotoka mikoani yanakuja kuwashushia huko huko!!, eti mama lishe,!!!
Hili jambo linatakiwa kupigiwa kura ikiwezekana utaratibu huu ulalamikiwe kila unapotumika, ni utaratibu kandamizi, wanaoteseka ni watu wa kipato cha chini, akina mama, watoto, walemavu nk. Kilio hiki kifikishwe kwa Rais.Naona leo mzee wangu umeamua KUMFOKEA MTU!!, tatizo la viongozi wetu huwa wanapenda huifurahisha hadhara inayomsikiliza kwa mtu huo bila kutafakari hizo kauli zao ki mantiki!!siku hizi kuna mabasi yanaanzia safari zao , kigamboni, mbagala hadi chanika, hivyo asubuhi inakuwa rahisi kwa abiria wa maeneo hayo kuanza safari, na hata ile usiku wanapotoka mikoani yanakuja kuwashushia huko huko!!, eti mama lishe,!!!
Ni kweli, viongozi wengi ndiyo wenye bajaji, taxi, pikipiki na daladala, utaratibu wa kuwalazimisha abiria kushuka stand kuu za miji unalenga kunufaisha biashara zao na siyo vinginevyoNasikia bodaboda, bajaji na taxi zote ni za viongozi.
Pale Iringa zilitajwa daladala kadhaa kuwa ni za DC, zingine Mkurugenzi, zingine RC na ndiyo maana suala la kushukia stand linashupaliwa sana, ili kulazimisha biashara ya daladala, bajaji na pikipikiNasikia bodaboda, bajaji na taxi zote ni za viongozi.
Subirini dawa iwaingie.Amos Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mfadhili wa zamani wa bendi ya FM ACADEMIA ya Kinondoni, bila kufanya utafiti wowote ule leo ametoa amri ya kulazimisha mabasi yote ya mikoani kuanzia safari zao kwenye kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Mbezi Luis, kinachoitwa kituo cha mabasi cha Magufuli na kushushia abiria wake hapohapo.
Lengo kuu la kauli yake hii ni kujaribu kukusanya watu ili kuneemesha wafanyabiashara waliojazana kwenye stendi hiyo bila mpangilio wowote, Makalla anaamini kwamba abiria wote wakishushwa ama kuanzia safari zao hapo basi watanunua bidhaa za wamachinga waliojazana hapo, hivi ndivyo akili yake ilivyomtuma, kwamba abiria wakomeshwe ili kufurahisha wafanyabiashara, amesahau kwamba abiria ni bora kuliko wamachinga kwenye mustakabhali wa Safari, hata hivyo sikubaliani naye.
Mbezi Luis eneo ilikojengwa Stendi ya Mabasi ya Mikoani ni nje kabisa ya jiji la DSM , kulazimisha Mabasi yaliyokuwa yanaanzia safari zake Mbagala, Tandika au Kigamboni kuacha kazi hiyo na kulazimisha sasa lazima yote yaanzie Nje ya jiji ni sawa na unyama , kwamba sasa aliyekuwa anapandia basi Mbagala akodi teksi kwa zaidi ya gharama ya tsh elfu 30 ili kulifuata basi Mbezi Luis, kwa vile tu Amos Makalla kajisikia hivyo haikubaliki na ni lazima ipingwe kwa nguvu zote.
Alichotakiwa kufanya Mh RC ni kuhakikisha kwamba basi lolote kutoka kwenye yard yoyote ile binafsi linakoanzia safari lisiondoke DSM bila ya kupita Stendi kuu ama lishushe litakako ila ni lazima lije stendi kuu, Vinginevyo Mh Makalla atamke hadharami Maslahi yake binafsi atakayopata kwa kuwatesa abiria wa Kigamboni, Vikindu , Chamanzi, Mbagala, Tandika na kwingineko waliokuwa wanapata ahueni ya kuanzia safari kwenye maeneo yao ya karibu.
Naomba kuwasilisha.
Duuh Mzee leo umejilipua!Naunga mkono hoja. Baadhi ta wenye mabasi wenye stendi zao pale Sinza Shekilango kama Kilimanjaro, Dar Lux, Marangu Coach na mengine, wenye mabasi zaidi ya moja kwa route ya Moshi Arusha, njia rahisi kwao ni route ya Bagamoyo Msata, na sio njia ya Chalinze, kuwalazimisha lazima waanzie Stendi mpya ni kuwatesa tuu bure abiria, after all, wengi wa abiria wa mabasi hayo, haswa wale abiria wa 1st Class, sio wa type ya kununua vitu kwa machinga au kula kwa Mama Ntilie! Hivyo kama nia ni kuwasaidia Machinga na mama ntilie, then, hizo ni sababu alizotoa Mkuu wa Mkoa ni sababu za kijinga sana!.
Hatuwezi kuendelea kuendesha nchi kijinga jinga hivi halafu utegemee tutapata mafanikio. Il tuendelee , la kupata maendeleo ya kweli de must stop such nonsense!.
p
Utopolo mtupu.
Fahamu Asilimia 90 ya wasafiri wanoutumia mabasi ni wanyonge ambao Kondakta akisahau kurudisha hata buku ya chenji zitawaka ndani ya gari.
Mkuu wa Mkoa kachemka pakubwa Sana tenaAmos Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mfadhili wa zamani wa bendi ya FM ACADEMIA ya Kinondoni, bila kufanya utafiti wowote ule leo ametoa amri ya kulazimisha mabasi yote ya mikoani kuanzia safari zao kwenye kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Mbezi Luis, kinachoitwa kituo cha mabasi cha Magufuli na kushushia abiria wake hapohapo...
SureHuo unyonge umejitia mwenyewe yale maneno yaliokuwa yanaandikwa kwenye mabus sasa yabebe maana halisi huwezi kusema unatoa semi luxury au luxury services halafu usiwe na shuttle buses !
Duniani hatufanani na hatutakuja kufanana kila mtu atasafiri kwa namna atakavyoweza (afford) .
Watu walisafiri na kwenda kulala kwa mjomba siku moja kabla ili kuwahi treni! Lakini pia kila maendeleo yanagharama
Ni kweli. Lakini hapa tunasema wewe unaongea vile ilipaswa kuwa, sivyo ilivyo. Makalla angekuwa sahihi kama angefanya utafiti na kutoa suluhisho lisilowaumiza wadau. Aweke miundombinu sahihi kati ya kituo hiki kikuu na maeneo ya jiji. Kwa mfano, mimi ningefurahi kama mwendokasi ingeungwa moja kwa moja pale kituoni. Mgeni unadrop na kuingia mwendo kasi. Kwa hali ilivyo sasa, pale kituoni ni adhabu wallahi. Ile kushuka mpka upate daladala, unajuta kuja Dar!Lazima niseme, hii ni ngumu mkuu Erythro.
Pamoja na pendekezo lako la mabasi hayo lazima yapitie Stendi kuu, bado naona Makalla yumo ndani ya mstari, hata kama yeye atakuwa na msukumo wa maslahi tofauti na matakwa ya mabasi hayo kuanzia na kuishia stendi kuu.
Stendi kuwa mbali na mjini siyo hoja, kwa sababu stendi kuu ni lazima ihudumiwe na usafiri toka sehemu zote za mji, kwa hiyo hiyo ni fursa kwa wenye biashara zao za usafirishaji mjini.
Ni sawa na uwanja wa ndege, ambako ukitaka kusafiri, kama unatokea Kawe, ni lazima utafute usafiri wa kukufikisha JKNIA, na hivyo hivyo, kama unaingia, utapata usafiri toka hapo kukupeleka Kawe.
Mimi naona la msingi zaidi ni Makala kuhakikisha sehemu zote za mji wake zipo huduma za kuwafikisha wananchi Stendi kuu ya mabasi, Mbezi Luis.
Lakini pia inabidi niulize swali hapa: kuna ubaya wowote kwa mfano kuwepo kwa vituo kadhaa vya mabasi mjini Dar, kwa mfano kituo cha mabasi yanayoelekea kusini mwa nchi kikawepo Mbagala; kituo cha mabasi yaendayo Nyanda za juu yakaanzia, tuseme Gongo La Mboto, n'k.?
Vipi, mbona hujachangamkia fursa ya Hotel/Guest maeneo hayo mkuu Erythrocyte!
Huwezi kufanya return kwa kuwaumiza wananchi tena kwa kuwabaka, think outside the box, na ndiyo tafsiri ya kiongozi, waondolee watu kero ili kuwaongezea ufanisi na siyo kuwajengea mazingira magumu ili waumie nawe unufaike kupitia maumivu yao, kiongozi ni problem solver siyo problem creator
Huyu mkuu wa mkoa amecopy upuuzi wa Dodoma,
Dodoma Kuna amri basi lolote hata lifike saa 8 usiku Dodoma,lazima lishushe abiria wote stand kuu,hakuna kuwapa msaada abiria wanaoenda mjini Kati Kati,basi lishushe,harafu liende tupu mjini kupaki,
Kisa wanataka abiria wanaoenda mjini,watumie usafiri mwingine wa boda boda,teksi,lengo ilikuwa ni kulazimisha abiria wapande boda boda,teksi kwenda mjini
Dodoma daladala mwisho saa nne usiku,unafika Dodoma saa Saba usiku,uchukue boda boda mpaka mjini,ulipe Tena 15000!akili za hovyo kabisa