Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

Waondoe machinga na wapiga debe

Watu wanafata huduma nzuri ndo maana mabasi yanatengeneza stend zao ili abiria wakwepe usumbufu waupatao mbezi
Serikali inatumia ubabe na siyo akili, alichofanya makala ni mfano wa wazi kabisa
 
Huyu mkuu wa mkoa amecopy upuuzi wa Dodoma,
Dodoma Kuna amri basi lolote hata lifike saa 8 usiku Dodoma,lazima lishushe abiria wote stand kuu,hakuna kuwapa msaada abiria wanaoenda mjini Kati Kati,basi lishushe,harafu liende tupu mjini kupaki,
Kisa wanataka abiria wanaoenda mjini,watumie usafiri mwingine wa boda boda,teksi,lengo ilikuwa ni kulazimisha abiria wapande boda boda,teksi kwenda mjini
Dodoma daladala mwisho saa nne usiku,unafika Dodoma saa Saba usiku,uchukue boda boda mpaka mjini,ulipe Tena 15000!akili za hovyo kabisa
Hili jambo halina afya kabisa kwa wananchi wa kipato cha chini, Mama Samia anatakiwa kuingilia kati kuwanusuru watu wake, wanaotoa hayo matamko hawatumii usafiri wa public, hawaonji machungu wanayopata wwananchi wa kipato cha chini
 
Dar es Salaam haihitaji kuwa na stendi kuu ya mabasi.Ukosefu wa uelewa wa biashara ya usafiri na akili ndogo za wapanga mji zinazopenda centralization na kuona majengo makubwa makubwa ndizo zimetufikisha katika matatizo kama haya.
Mkuu una point kubwa Sana ebu tia nyama tukuelewe zaidi tafadhari
 
Nchi zilizoendelea zimeruhusu makampuni ya usafirishaji kuwa na pick points zao ili wateja wapate unafuu kusafiri,hapa kwetu ni kinyume chake, tumecentralize stand bila kuweka mifumo mizuri wezeshi ya kuwafikisha abiria hapo
 
Nchi za kijamaa hazija wahi kuwa makini ni full kukurupuka ili kuonesha serikali ipo
 
Lazima niseme, hii ni ngumu mkuu Erythro.

Pamoja na pendekezo lako la mabasi hayo lazima yapitie Stendi kuu, bado naona Makalla yumo ndani ya mstari, hata kama yeye atakuwa na msukumo wa maslahi tofauti na matakwa ya mabasi hayo kuanzia na kuishia stendi kuu.

Stendi kuwa mbali na mjini siyo hoja, kwa sababu stendi kuu ni lazima ihudumiwe na usafiri toka sehemu zote za mji, kwa hiyo hiyo ni fursa kwa wenye biashara zao za usafirishaji mjini.

Ni sawa na uwanja wa ndege, ambako ukitaka kusafiri, kama unatokea Kawe, ni lazima utafute usafiri wa kukufikisha JKNIA, na hivyo hivyo, kama unaingia, utapata usafiri toka hapo kukupeleka Kawe.

Mimi naona la msingi zaidi ni Makala kuhakikisha sehemu zote za mji wake zipo huduma za kuwafikisha wananchi Stendi kuu ya mabasi, Mbezi Luis.

Lakini pia inabidi niulize swali hapa: kuna ubaya wowote kwa mfano kuwepo kwa vituo kadhaa vya mabasi mjini Dar, kwa mfano kituo cha mabasi yanayoelekea kusini mwa nchi kikawepo Mbagala; kituo cha mabasi yaendayo Nyanda za juu yakaanzia, tuseme Gongo La Mboto, n'k.?

Vipi, mbona hujachangamkia fursa ya Hotel/Guest maeneo hayo mkuu Erythrocyt

Amos Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mfadhili wa zamani wa bendi ya FM ACADEMIA ya Kinondoni , bila kufanya utafiti wowote ule leo ametoa amri ya kulazimisha mabasi yote ya mikoani kuanzia safari zao kwenye kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Mbezi Luis , kinachoitwa kituo cha mabasi cha Magufuli na kushushia abiria wake hapohapo .

Lengo kuu la kauli yake hii ni kujaribu kukusanya watu ili kuneemesha wafanyabiashara waliojazana kwenye stendi hiyo bila mpangilio wowote , Makalla anaamini kwamba abiria wote wakishushwa ama kuanzia safari zao hapo basi watanunua bidhaa za wamachinga waliojazana hapo , hivi ndivyo akili yake ilivyomtuma , kwamba abiria wakomeshwe ili kufurahisha wafanyabiashara , Amesahau kwamba abiria ni bora kuliko wamachinga kwenye mustakabhali wa Safari , hata hivyo sikubaliani naye .

Mbezi Luis eneo ilikojengwa Stendi ya Mabasi ya Mikoani ni nje kabisa ya jiji la DSM , kulazimisha Mabasi yaliyokuwa yanaanzia safari zake Mbagala , Tandika au Kigamboni kuacha kazi hiyo na kulazimisha sasa lazima yote yaanzie Nje ya jiji ni sawa na unyama , kwamba sasa aliyekuwa anapandia basi Mbagala akodi teksi kwa zaidi ya gharama ya tsh elfu 30 ili kulifuata basi Mbezi Luis , kwa vile tu Amos Makalla kajisikia hivyo haikubaliki na ni lazima ipingwe kwa nguvu zote .

Alichotakiwa kufanya Mh RC ni kuhakikisha kwamba basi lolote kutoka kwenye yard yoyote ile binafsi linakoanzia safari lisiondoke DSM bila ya kupita Stendi kuu ama lishushe litakako ila ni lazima lije stendi kuu , Vinginevyo Mh Makalla atamke hadharami Maslahi yake binafsi atakayopata kwa kuwatesa abiria wa Kigamboni , Vikindu , Chamanzi , Mbagala , Tandika na kwingineko waliokuwa wanapata ahueni ya kuanzia safari kwenye maeneo yao ya karibu .

Naomba kuwasilisha .

Mheshimiwa mkuu wa mkoa, hoja yake hapa, ingelikuwa ni mapato ya stand na unafuu kwa abiria ambazo angeziondoa kwa kusema kila basi linapoingia na kutoka lipitie Mbezi Louis ili kutoa mchango wa standi na kushusha na kupakia abilia wanaohitaji kupandia na kushukia pale.

Suala la kusafirisha waharifu, pale pale mbezi kama kuna mfumo wa kukagua wanaposhuka, ufanyike pale pale mbezi, wawakamate hao waharifu, kisha gari liendelee na ratiba zingine.

Na kwa taarifa, waharifu wanawaza kupanda na kushukia popote pale njiani ki mkakati. Siyo rahisi wafike Mbezi kwa kupanda na kushuka na ndiyo sabbu tunalilia serikali iimarishe sana checkpoints ziizomo njiani, idhibiti vichochoro vya mipakani, na pia wajumuishe vyombo vingine vya usafiri kama malori na magari binafsi.

Hawa mama lishe kama hawapati wateja wa kutosha maana yake soko ni dogo, watafute kwingine na si kulazimisha migogoro kwa watu ili wakachanegie mapato ya mama lishe.
 
Jamani Makala unajua magari yanayotoka Mwanza yanaingia Dar saa sita adi saba usiku? Yaani mtu ameshuka stendi ya Mbezi saa sita alafu atembee zaidi ya 1km nje ya stendi za mizigo anatafuta usafiri ya daladala za kuja mjini.

Kuanzia saa sita usiku daladala mbovumbovu ndo unazikuta pale nje umbali wa 1km za kwenda Buguruni. Ufike Buguruni uanze tena kutafuta usafiri wa bajaji na boda kukupeleka kwako.Ukiulizia Tax pale Stendi Mbezi adi Tazara huo usiku saa sita ni sawa na nauli ya Dar Mwanza.

Basi wakisema watu washushwe na daladala na mwendokasi zisogezwe eneo hilo na waboreshe mazingira; waachane na upuzi kabisa.

Kuna siku nipo na Allys Bus tumefik pale stend, traffic anamwambia amna driva kuondoka na abiria kwenye gari kuelekea mjini wakati gari inaelekea Urafiki. Nikamuuliza traffic umepewa order au umeamua tu kujisemea? yeye akasema amepewa order ..then nikamuuliza kwa akili yako unaona ni sawa gari kwenda bila abiria wanaoelekea huko? ili tu tuwaunge wamachinga wa hapa? akasema siyo sawa..then nikamuuliza wewe hiyo order hukuichallage kidogo? akasema ndugu we acha tu....shukeni.

Makala atambue kua kusafiri isiwe adhabu kwa wasafiri kisa tu wamachinga; kwani wamachinga wa kigamboni wao wanafanyaje biashara?
 
Lazima niseme, hii ni ngumu mkuu Erythro.

Pamoja na pendekezo lako la mabasi hayo lazima yapitie Stendi kuu, bado naona Makalla yumo ndani ya mstari, hata kama yeye atakuwa na msukumo wa maslahi tofauti na matakwa ya mabasi hayo kuanzia na kuishia stendi kuu.

Stendi kuwa mbali na mjini siyo hoja, kwa sababu stendi kuu ni lazima ihudumiwe na usafiri toka sehemu zote za mji, kwa hiyo hiyo ni fursa kwa wenye biashara zao za usafirishaji mjini.

Ni sawa na uwanja wa ndege, ambako ukitaka kusafiri, kama unatokea Kawe, ni lazima utafute usafiri wa kukufikisha JKNIA, na hivyo hivyo, kama unaingia, utapata usafiri toka hapo kukupeleka Kawe.

Mimi naona la msingi zaidi ni Makala kuhakikisha sehemu zote za mji wake zipo huduma za kuwafikisha wananchi Stendi kuu ya mabasi, Mbezi Luis.

Lakini pia inabidi niulize swali hapa: kuna ubaya wowote kwa mfano kuwepo kwa vituo kadhaa vya mabasi mjini Dar, kwa mfano kituo cha mabasi yanayoelekea kusini mwa nchi kikawepo Mbagala; kituo cha mabasi yaendayo Nyanda za juu yakaanzia, tuseme Gongo La Mboto, n'k.?

Vipi, mbona hujachangamkia fursa ya Hotel/Guest maeneo hayo mkuu Erythrocyte!
Good Point.

Cha msingi zingejengwa Terminal nyingine 3 hadi 4.
 
Vipi kuhusu mimi ninayeishi Sinza nikitaka kwenda Mtwara?

Nilipe Teksi 30,000 kwenda Temeke?

Wa Bunju je?

Cha msingi zijengwe Stand kubwa kila Wilaya.
Amos Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mfadhili wa zamani wa bendi ya FM ACADEMIA ya Kinondoni , bila kufanya utafiti wowote ule leo ametoa amri ya kulazimisha mabasi yote ya mikoani kuanzia safari zao kwenye kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Mbezi Luis , kinachoitwa kituo cha mabasi cha Magufuli na kushushia abiria wake hapohapo .

Lengo kuu la kauli yake hii ni kujaribu kukusanya watu ili kuneemesha wafanyabiashara waliojazana kwenye stendi hiyo bila mpangilio wowote , Makalla anaamini kwamba abiria wote wakishushwa ama kuanzia safari zao hapo basi watanunua bidhaa za wamachinga waliojazana hapo , hivi ndivyo akili yake ilivyomtuma , kwamba abiria wakomeshwe ili kufurahisha wafanyabiashara , Amesahau kwamba abiria ni bora kuliko wamachinga kwenye mustakabhali wa Safari , hata hivyo sikubaliani naye .

Mbezi Luis eneo ilikojengwa Stendi ya Mabasi ya Mikoani ni nje kabisa ya jiji la DSM , kulazimisha Mabasi yaliyokuwa yanaanzia safari zake Mbagala , Tandika au Kigamboni kuacha kazi hiyo na kulazimisha sasa lazima yote yaanzie Nje ya jiji ni sawa na unyama , kwamba sasa aliyekuwa anapandia basi Mbagala akodi teksi kwa zaidi ya gharama ya tsh elfu 30 ili kulifuata basi Mbezi Luis , kwa vile tu Amos Makalla kajisikia hivyo haikubaliki na ni lazima ipingwe kwa nguvu zote .

Alichotakiwa kufanya Mh RC ni kuhakikisha kwamba basi lolote kutoka kwenye yard yoyote ile binafsi linakoanzia safari lisiondoke DSM bila ya kupita Stendi kuu ama lishushe litakako ila ni lazima lije stendi kuu , Vinginevyo Mh Makalla atamke hadharami Maslahi yake binafsi atakayopata kwa kuwatesa abiria wa Kigamboni , Vikindu , Chamanzi , Mbagala , Tandika na kwingineko waliokuwa wanapata ahueni ya kuanzia safari kwenye maeneo yao ya karibu .

Naomba kuwasilisha .
 
Mimi kinachonisikitisha ni kukosa viongozi wanaoweza kuja na plan za miaka angalau 50 mbele... mbona kina Mwalimu Nyerere waliweza kuweka mipango inayoishi hadi leo? Ukiangalia kituo cha Ubungo hakina miaka mingi tayari kimebomolewa. Hata hiyo ya Magufuli usishangae baada ya miaka mitano ikabomolewa na kuhamishwa tena. Kuhusu aliyoamrisha Makala ni upuuzi kama upuuzi mwingine. Sio lazima mabasi yarundikwe sehemu moja. Labda wangejenga stendi angalau nne jijini Dsm ili kwenda sawa na uhitaji. Hao mama ntilie wangetafutiwa utaratibu mzuri wa kuongeza thamani za biashara zao ingevutia hata wasafiri wasiopenda kula njiani kununua vyakula vyao. Huwezi kunilazimisha kula kwa mama ntilie ambaye uchafu ni mojawapo ya sifa ya yeye kuwa mama ntilie.
 
Jamani Makala unajua magari yanayotoka Mwanza yanaingia Dar saa sita adi saba usiku? Yaani mtu ameshuka stendi ya Mbezi saa sita alafu atembee zaidi ya 1km nje ya stendi za mizigo anatafuta usafiri ya daladala za kuja mjini.

Kuanzia saa sita usiku daladala mbovumbovu ndo unazikuta pale nje umbali wa 1km za kwenda Buguruni. Ufike Buguruni uanze tena kutafuta usafiri wa bajaji na boda kukupeleka kwako.Ukiulizia Tax pale Stendi Mbezi adi Tazara huo usiku saa sita ni sawa na nauli ya Dar Mwanza.

Basi wakisema watu washushwe na daladala na mwendokasi zisogezwe eneo hilo na waboreshe mazingira; waachane na upuzi kabisa.

Kuna siku nipo na Allys Bus tumefik pale stend, traffic anamwambia amna driva kuondoka na abiria kwenye gari kuelekea mjini wakati gari inaelekea Urafiki. Nikamuuliza traffic umepewa order au umeamua tu kujisemea? yeye akasema amepewa order ..then nikamuuliza kwa akili yako unaona ni sawa gari kwenda bila abiria wanaoelekea huko? ili tu tuwaunge wamachinga wa hapa? akasema siyo sawa..then nikamuuliza wewe hiyo order hukuichallage kidogo? akasema ndugu we acha tu....shukeni.

Makala atambue kua kusafiri isiwe adhabu kwa wasafiri kisa tu wamachinga; kwani wamachinga wa kigamboni wao wanafanyaje biashara?
Mkuu pole sana , Uchunguzi wetu unaonyesha kwamba viongozi wa Tanzania hawajawahi kutumia usafiri huo mnaoutumia nyie , hawajui chochote kuhusu changamoto zake
 
Tatizo ni kudharau fani za wengine na wenye fani hizo kukubali kuburuzwa tu. Hauwezi kuzungumzia stendi ya mabasi nje ya mipango miji. Stendi za mabasi ili ziwe viable zinahitaji kuwa pia kivutio cha biashara za kawaida na ziwe rahisi kufikiwa na usafiri wa kawaida. Ndio maana, tofauti na sisi tunavyofikiri, Intercity Bus Terminals nyingi ziko katikati ya miji ( Port Authority New York, Stockholm,Centraal Amsterdam ZOB Berlin n.k.) na kama iko pembezoni basi inafikika kirahisi sana na usafiri wa mjini kutoka sehemu nyingine za mji ( underground, treni, mabasi ya mjini n.k.). Aidha, hamna dhambi kuwa na intercity bus terminals zaidi yamoja ili mradi nazo pia zinafikika kirahisi kwa usafiri wa kawaida wa mjini ( dala dala, uber, boda boda n.k.).

Badala ya kukimbilia ku consolidate shughuli zote kwenye kituo hicho, angezungumzia namna gani mwendo kasi ingeweza kuunganisha kituo hiki na vituo vya Shekilago na Tandika. Aidha, vituo hivi viunganishwe na vituo vya treni, bandari na airport. Uamuzi wa kujenga intercity bus terminal unahitaji umakini mkubwa na sio wa kuangaliwa in isolation. Tunarudia makosa yale yale tunayoyafanya katika ujenzi wa masoko mjini.

Amandla...
 
Ni rahisi sana. Jiografia ya kuingia Dar es Salaam imegawanyika katika sehemu kuu tatu.

Moja ni njia inayotoka Kusini ambayo sehemu kubwa inaisha Mtwara.

Pili ni Njia inayotokea Moro ambayo hapo Moro inagawanyika kuelekea Nyanda za juu kusini katika mikoa ya Mbeya,Ruvuma, nchi za Zambia, Malawi n.k na nyingine kuelekea Dodoma.

Tatu ni kutokea Kaskazini ambayo sasa Barabara ya Bagamoyo inatumika kwa kiasi kikubwa.

Kituo cha mabasi cha Magufuli kinawafaa zaidi watu wa njia ya pili kutokea Moro na kidogo wa njia ya tatu kutokea Kaskazini ila hakina tija kubwa kwa watu wanaotokea Kusini

Watu wanaotokea kusini walipaswa wawe na Stendi yao kubwa Mbagala, watu wa kutokea Kaskazini walipaswa wawe na stendi yao kubwa Bunju na magari yao yaishie huko.

Magari yanayotokea Kusini yanashusha robo tatu ya abiria wake Mbagala/Temeke, Magari yanayotokea Moro yanashusha robo tatu ya abiria stendi ya Magufuli magari yanayotokea Kaskazini yanashusha robo tatu ya abiria wake Kuanzia Kibaha/Kimara/Bunju/Tegeta.
Ukiwa na vituo vitatu vikubwa unaondoa hizi kelele za sasa hivi na unapunguza foleni za mrundikano wa mabasi makubwa katikati ya mji.
Mkuu una point kubwa Sana ebu tia nyama tukuelewe zaidi tafadhari
 
Lazima niseme, hii ni ngumu mkuu Erythro.

Pamoja na pendekezo lako la mabasi hayo lazima yapitie Stendi kuu, bado naona Makalla yumo ndani ya mstari, hata kama yeye atakuwa na msukumo wa maslahi tofauti na matakwa ya mabasi hayo kuanzia na kuishia stendi kuu.

Stendi kuwa mbali na mjini siyo hoja, kwa sababu stendi kuu ni lazima ihudumiwe na usafiri toka sehemu zote za mji, kwa hiyo hiyo ni fursa kwa wenye biashara zao za usafirishaji mjini.

Ni sawa na uwanja wa ndege, ambako ukitaka kusafiri, kama unatokea Kawe, ni lazima utafute usafiri wa kukufikisha JKNIA, na hivyo hivyo, kama unaingia, utapata usafiri toka hapo kukupeleka Kawe.

Mimi naona la msingi zaidi ni Makala kuhakikisha sehemu zote za mji wake zipo huduma za kuwafikisha wananchi Stendi kuu ya mabasi, Mbezi Luis.

Lakini pia inabidi niulize swali hapa: kuna ubaya wowote kwa mfano kuwepo kwa vituo kadhaa vya mabasi mjini Dar, kwa mfano kituo cha mabasi yanayoelekea kusini mwa nchi kikawepo Mbagala; kituo cha mabasi yaendayo Nyanda za juu yakaanzia, tuseme Gongo La Mboto, n'k.?

Vipi, mbona hujachangamkia fursa ya Hotel/Guest maeneo hayo mkuu Erythrocyte!
Kwa hiyo wewe unawaambia waliokuwa wanatoka kigamboni na kupitia bagamoyo waende kwa mbezi ndio warudi,,,,,
Kwamba unawaambia waliokuwa wanaanzia Bamaga,Mwenge,tegeta,boko,Bunju,mapinga,Kerege,Zinga waakaanzie Mbezi luis.
Shame to you
 
Back
Top Bottom