Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

"The patience of the bricklayer is assumed by the architect". Makala ndiyo architect hapa. Mipango yake haichukulii abiria watatesekaje. Kwani watamfanya nini? Ilitakiwa viongozi wa kisiasa wa mkoa wachaguliwe kwa kura za wananchi!

All these are consequences of a fundamental flaw. Katiba mbovu. Kwa katiba nzuri amri kama hii inakuwa ni kitu kinatokana na majadiliano ya madiwani na kupigiwa kura. Ikipita ndiyo inatangazwa. Kwa sasa ni Ayatollah Makala anasema apendacho na kinakuwa amri.
 
Amos Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mfadhili wa zamani wa bendi ya FM ACADEMIA ya Kinondoni , bila kufanya utafiti wowote ule leo ametoa amri ya kulazimisha mabasi yote ya mikoani kuanzia safari zao kwenye kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Mbezi Luis , kinachoitwa kituo cha mabasi cha Magufuli na kushushia abiria wake hapohapo .

Lengo kuu la kauli yake hii ni kujaribu kukusanya watu ili kuneemesha wafanyabiashara waliojazana kwenye stendi hiyo bila mpangilio wowote , Makalla anaamini kwamba abiria wote wakishushwa ama kuanzia safari zao hapo basi watanunua bidhaa za wamachinga waliojazana hapo , hivi ndivyo akili yake ilivyomtuma , kwamba abiria wakomeshwe ili kufurahisha wafanyabiashara , Amesahau kwamba abiria ni bora kuliko wamachinga kwenye mustakabhali wa Safari , hata hivyo sikubaliani naye .

Mbezi Luis eneo ilikojengwa Stendi ya Mabasi ya Mikoani ni nje kabisa ya jiji la DSM , kulazimisha Mabasi yaliyokuwa yanaanzia safari zake Mbagala , Tandika au Kigamboni kuacha kazi hiyo na kulazimisha sasa lazima yote yaanzie Nje ya jiji ni sawa na unyama , kwamba sasa aliyekuwa anapandia basi Mbagala akodi teksi kwa zaidi ya gharama ya tsh elfu 30 ili kulifuata basi Mbezi Luis , kwa vile tu Amos Makalla kajisikia hivyo haikubaliki na ni lazima ipingwe kwa nguvu zote .

Alichotakiwa kufanya Mh RC ni kuhakikisha kwamba basi lolote kutoka kwenye yard yoyote ile binafsi linakoanzia safari lisiondoke DSM bila ya kupita Stendi kuu ama lishushe litakako ila ni lazima lije stendi kuu , Vinginevyo Mh Makalla atamke hadharami Maslahi yake binafsi atakayopata kwa kuwatesa abiria wa Kigamboni , Vikindu , Chamanzi , Mbagala , Tandika na kwingineko waliokuwa wanapata ahueni ya kuanzia safari kwenye maeneo yao ya karibu .

Naomba kuwasilisha .
Samia bado anazungukwa na genge [SUKUMA GANG] , hawa watamtesa sana mpaka atakapo wa-phase out.
Huyu Makala siku moja atoke kwake kimanzichana kwa Daladala , aende Stendi mbezi kuwahi basi la saa 12 asubuhi, ndio ataelewa adha wapatazo wananchi.
Ukitoka kimanzichana saa nane usiku unafika saa 11 alfajiri mbezi, hapohujakata tiketi then uanze safari.
Hii nchi ina watu wa mihemko kuliko.
 
Hii nchi wanasikilizwa machinga na bodaboda tu,kundi hili Lina nguvu kubwa Sana ya ushawishi Kwa wanasiasa.
Hii yote imetokana na mwendazake kuwaona machinga, bodaboda na mama lishe ndiyo vipaumbele.

Sikuhizi ukipita mitaa ya Kariakoo na posta utakutana na mama lishe wanapika pembezoni mwa barabara yaani ni mwendo wa Moshi wa kuni city centre
 
Hata stendi ya mabasi ya Mwanza kipindi inatolewa city center kupelekwa Nyegezi kulikuwepo hoja hizi hizi.

Leo hii Nyegezi siyo nje ya mji tena na uanzishwaji wa utitiri wa routes za daladala zimeifanya stand iwe kama IPO city center tu.

Miji "hupanuliwa" wa staili hiyo.

Labda hoja Ingekuwa uwepo wa miundombinu ya ku-accomodate watu wote watakaotumia be stendi hiyo
Unafananisha Mwanza na Dar? Mtu wa Mbagala kwenda Mbezi Mwisho inabidi aamke saa 8 usiku ndipo atawahi basi
 
Mimi naona RC yupo sawa tu kwa maana halisi ya kuwa na stand ya mkoa. Haitakuwa na maana kama kila mmiliki wa mabasi awe na stand yake, hata hivyo ikumbukwe ile investment iliyowekwa pale na serikali inahitaji return japo kuwa ni huduma kwa wananchi. Sasa return itarudi vipi ikiwa lengo halifikiwi kwa sababu ya uchache wa abiria
unajua kua pale stendi ya magufuli hakuna kampuni inaruhusiwa kupaki magari matano kwa wakati mmoja,na ilihimizwa wale wenye mabasi mengi kua na private places kuhifadhi mabasi.kunatofuati ya kupitia stendi kuu na kushusha abiria,pia hizi private stations nazo ni za kulipia sio bure.
 
Kinachotakiwa ni kampuni za usafirishaji kuanzisha shuttle bus kwaajili ya kukusanya abiria wake maeneo husika kama vile shekilango lakini mabasi yanatakiwa kuanzia na kumalizia safari kwenye stendi kuu “Terminal” hivi ndivyo hata majiji yaliyoendelea yalivyopangwa.
Hata Malaori kuingia mpaka ndani ya mji au bandarini ni udhaifu wa watu wa mipango miji.Reli ilitakiwa itumike kutoa mizigo bandarini mpaka kwenye ICD zilizopo nje ya mji.
Wewe umeongea point at least. Umetufungua akili zaidi
 
Hii kero pia iende kwa mikoa mingine mfano Iringa na Dodoma. Pale iringa stend kuu iko karibu kilometer 20 kutoka iringa mjini na mabasi yanalazimishwa kushusha abiria wote stend kisha yanaenda mjini yakiwa tupu na abiria wanalazimika kupanda dala dala kwenda mjini huko huko ambako mabasi yanaenda.
Nchi hi tuna viongoz ambao problem creators na sio solvers
 
Hata stendi ya mabasi ya Mwanza kipindi inatolewa city center kupelekwa Nyegezi kulikuwepo hoja hizi hizi.

Leo hii Nyegezi siyo nje ya mji tena na uanzishwaji wa utitiri wa routes za daladala zimeifanya stand iwe kama IPO city center tu.

Miji "hupanuliwa" wa staili hiyo.

Labda hoja Ingekuwa uwepo wa miundombinu ya ku-accomodate watu wote watakaotumia be stendi hiyo
usichanganye mada hakuna aliyepinga stendi kwenda mbezi kinachozungumzwa na suala la kulazimisha abiria kushushwa na kupakiwa ndani ya stendi ya mbezi.
 
huyu MAKALA atakuwa mkuu wa mkoa alietumikia muda mfupi sana Dar es Salaam.

yaani naishi Tabata kuna option ya kushushiwa Ubungo unanilazimisha nishushiwe huko porini Mbezi ili iweje?
Miaka 15 hapo mbezi patakua city,,ile stand imejengwa kwa kufocus miaka 20 mbele,,sio leo
 
Katika makosa makubwa Mama amefanya ni kumleta Makala Dar, alishindwa Mbeya akahamishiwa mkoa mdogo huko Rukwa/Katavi akashindwa, ataiwezaje Dar?

Badala ya kuja kutatua kero amekuja kuongeza kero, he is not for citizens
Mimi naona ni vizuri kila upande zinapoingia Barabara kuu kuwa na stendi kwa mfano kwa DSM upande wa kila road kuwe na stendi kubwa,barabara ya Nyerere(zamani Pugu road) na bagamoyo road hata katika miji mwingine tunaona Dodoma japo nao hawako vizuri sana halafu katikati kuwe na shuttle ya daladala
 
Jamani Makala unajua magari yanayotoka Mwanza yanaingia Dar saa sita adi saba usiku? Yaani mtu ameshuka stendi ya Mbezi saa sita alafu atembee zaidi ya 1km nje ya stendi za mizigo anatafuta usafiri ya daladala za kuja mjini.

Kuanzia saa sita usiku daladala mbovumbovu ndo unazikuta pale nje umbali wa 1km za kwenda Buguruni. Ufike Buguruni uanze tena kutafuta usafiri wa bajaji na boda kukupeleka kwako.Ukiulizia Tax pale Stendi Mbezi adi Tazara huo usiku saa sita ni sawa na nauli ya Dar Mwanza.

Basi wakisema watu washushwe na daladala na mwendokasi zisogezwe eneo hilo na waboreshe mazingira; waachane na upuzi kabisa.

Kuna siku nipo na Allys Bus tumefik pale stend, traffic anamwambia amna driva kuondoka na abiria kwenye gari kuelekea mjini wakati gari inaelekea Urafiki. Nikamuuliza traffic umepewa order au umeamua tu kujisemea? yeye akasema amepewa order ..then nikamuuliza kwa akili yako unaona ni sawa gari kwenda bila abiria wanaoelekea huko? ili tu tuwaunge wamachinga wa hapa? akasema siyo sawa..then nikamuuliza wewe hiyo order hukuichallage kidogo? akasema ndugu we acha tu....shukeni.

Makala atambue kua kusafiri isiwe adhabu kwa wasafiri kisa tu wamachinga; kwani wamachinga wa kigamboni wao wanafanyaje biashara?
Wahakikishe basi za uda zinaoperate masaa 24 kutoka hiyo stand,,hiyo ndo simple solution..
 
Hata stendi ya mabasi ya Mwanza kipindi inatolewa city center kupelekwa Nyegezi kulikuwepo hoja hizi hizi.

Leo hii Nyegezi siyo nje ya mji tena na uanzishwaji wa utitiri wa routes za daladala zimeifanya stand iwe kama IPO city center tu.

Miji "hupanuliwa" wa staili hiyo.

Labda hoja Ingekuwa uwepo wa miundombinu ya ku-accomodate watu wote watakaotumia be stendi hiyo
Ila kuna miji imedumaa,,mfano shinyanga,,stand iko porini,na ukiachwa hapo usiku,unaweza hata kuliwa fisi..😂😂
 
Mimi naona ni vizuri kila upande zinapoingia Barabara kuu kuwa na stendi kwa mfano kwa DSM upande wa kila road kuwe na stendi kubwa,barabara ya Nyerere(zamani Pugu road) na bagamoyo road hata katika miji mwingine tunaona Dodoma japo nao hawako vizuri sana halafu katikati kuwe na shuttle ya daladala
Ni wazo zuri sana, hata hizo stand zingeungwa kwa mtandao wa trams za uhakika ingekuwa jambo la kipekee sana
 
Hii nchi wanasikilizwa machinga na bodaboda tu,kundi hili Lina nguvu kubwa Sana ya ushawishi Kwa wanasiasa.
Hii yote imetokana na mwendazake kuwaona machinga, bodaboda na mama lishe ndiyo vipaumbele.

Sikuhizi ukipita mitaa ya Kariakoo na posta utakutana na mama lishe wanapika pembezoni mwa barabara yaani ni mwendo wa Moshi wa kuni city centre
Nilikutaga mamantilie anasukuma chapati kwenye veranda ya Mwanza Hotel,,ndo nikajua kumbe tuko choo cha kike..
 
Sasa hakutakuwa na maana ya stand watu wazoee tu hivyo hivyo daladal,bajaji,boda machinga wenye maduka yanayozunguka stand hiyo watakosa wateja
Mtu baada ya kununua maji ya kunywa stand anaenda kushushiwa huko shekilango mwisho stand inakuwa sio ishu watu watashindwa hata kufungua migahawa kwa kuhofia watakosa wateja
 
Kazi kubwa ya stendi ni mabasi kushusha na kupakiza abiria karibia na mahali wanapoenda au kuishi sio huo ugoro mwingine wa ziada unaouzungumizia wewe.

Back
Top Bottom