Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

Dar es Salaam haihitaji kuwa na stendi kuu ya mabasi.Ukosefu wa uelewa wa biashara ya usafiri na akili ndogo za wapanga mji zinazopenda centralization na kuona majengo makubwa makubwa ndizo zimetufikisha katika matatizo kama haya.
Inawezekana wapanga mji walinakiri tu yanayofanyika sehemu zingine duniani bila kuhusisha mazingira ya mji wao yalivyo.
 
Mimi naona RC yupo sawa tu kwa maana halisi ya kuwa na stand ya mkoa. Haitakuwa na maana kama kila mmiliki wa mabasi awe na stand yake, hata hivyo ikumbukwe ile investment iliyowekwa pale na serikali inahitaji return japo kuwa ni huduma kwa wananchi. Sasa return itarudi vipi ikiwa lengo halifikiwi kwa sababu ya uchache wa abiria
Kwahiyo kwenye feasibility study hawakuona kuwa kutakuwa na usumbufu wa kutaka kushushia watu stand ?

Unataka kuniambia investment Kama ile ilikuwa haina epembuzi yakinifu?
 
Kwa hiyo wewe unawaambia waliokuwa wanatoka kigamboni na kupitia bagamoyo waende kwa mbezi ndio warudi,,,,,
Kwamba unawaambia waliokuwa wanaanzia Bamaga,Mwenge,tegeta,boko,Bunju,mapinga,Kerege,Zinga waakaanzie Mbezi luis.
Shame to you
Mkuu, hizi ni taratibu za miji. Miji haipangwi kiholela tu kwa matakwa ya kundi fulani.
 
Usifananishe usafiri wa anga na ardhini ni vitu viwili tofauti, utaratibu huu wa Makalla utakua ni usumbufu kwa baadhi ya abiria wanaotokea ktkt ya mji kesi za kuchelewa usafiri zitakua nyingi kutokana na foleni
Ukiangalia kwa makini, huu sio utaratibu wa Makalla. Ni lazima kuna sheria zinazosimamia mambo haya. Ni bora kujiridhisha na hizo kwanza kabla ya kulaumu.

Haya mabasi yote, liseni zao zitakuwa zinaonyesha wanafanya kazi katika vituo vipi na vipi na njia watakazotumia kufika huko wanakokwenda kwa uwazi kabisa. Hawana liseni ya kusafirisha abiria tokea Temeke kwenda standi kuu.
Wewe hili unaweza kuliona kuwa dogo, lakini ni sheria, na linahusu mambo mengi.

Wewe unayepandia Temeke, ajali ikikupata kabla hujafika stendi kuu, hao wenye basi wataeleza nini?

Unasema usafiri wa anga ni tofauti na ardhini, ndiyo, lakini katika mambo mengi vyote vinafanana..Kukiwa na uwanja wa ndege Morogoro, na pawe na ndege zinazoanzia Morogoro na safari zao, lakini hawawezi kwenda nje ya nchi bila kupitia JKNIA. Huu ni mfano ninaoweza kukufafanulia vizuri, lakini ngoja niuachie hapa ukining'inia...
 
Amos Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mfadhili wa zamani wa bendi ya FM ACADEMIA ya Kinondoni , bila kufanya utafiti wowote ule leo ametoa amri ya kulazimisha mabasi yote ya mikoani kuanzia safari zao kwenye kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Mbezi Luis , kinachoitwa kituo cha mabasi cha Magufuli na kushushia abiria wake hapohapo .

Lengo kuu la kauli yake hii ni kujaribu kukusanya watu ili kuneemesha wafanyabiashara waliojazana kwenye stendi hiyo bila mpangilio wowote , Makalla anaamini kwamba abiria wote wakishushwa ama kuanzia safari zao hapo basi watanunua bidhaa za wamachinga waliojazana hapo , hivi ndivyo akili yake ilivyomtuma , kwamba abiria wakomeshwe ili kufurahisha wafanyabiashara , Amesahau kwamba abiria ni bora kuliko wamachinga kwenye mustakabhali wa Safari , hata hivyo sikubaliani naye .

Mbezi Luis eneo ilikojengwa Stendi ya Mabasi ya Mikoani ni nje kabisa ya jiji la DSM , kulazimisha Mabasi yaliyokuwa yanaanzia safari zake Mbagala , Tandika au Kigamboni kuacha kazi hiyo na kulazimisha sasa lazima yote yaanzie Nje ya jiji ni sawa na unyama , kwamba sasa aliyekuwa anapandia basi Mbagala akodi teksi kwa zaidi ya gharama ya tsh elfu 30 ili kulifuata basi Mbezi Luis , kwa vile tu Amos Makalla kajisikia hivyo haikubaliki na ni lazima ipingwe kwa nguvu zote .

Alichotakiwa kufanya Mh RC ni kuhakikisha kwamba basi lolote kutoka kwenye yard yoyote ile binafsi linakoanzia safari lisiondoke DSM bila ya kupita Stendi kuu ama lishushe litakako ila ni lazima lije stendi kuu , Vinginevyo Mh Makalla atamke hadharami Maslahi yake binafsi atakayopata kwa kuwatesa abiria wa Kigamboni , Vikindu , Chamanzi , Mbagala , Tandika na kwingineko waliokuwa wanapata ahueni ya kuanzia safari kwenye maeneo yao ya karibu .

Naomba kuwasilisha .
Hii hoja naiunga mkono. Jamani hii itawaumiza sana abiria. Sijajua mantiki iliyotumika kulazimisha watu kwenda kupandia Mbezi. Jamani jalini na sisi tulio na uwezo wa kutumia daladala.
 
kwa hiyo sasa yale mabasi ya abiria wa mikoa ya Lindi na mtwara sasa waje kushukia mbezi ili kutoa fursa kwa daladala.
Sijui mkuu, hili ni la kuuliza wahusika, lakini taratibu ni taratibu. Unapokubali kufuata taratibu, basi timiza wajibu huo.
Liseni za mabasi zitaonyesha safari zao zinaanzia stendi kuu; halafu waokoteze abiria njiani kabla ya kuanza safari yao hapo stendi kuu? Sijui kama taratibu hizo zinaruhusu hivyo.
 
Kuna uzi humu watu waliikosoa sana hiyo stendi wakati inajengwa na wakaelezea jinsi gani haitakuwa na tija yoyote kwa wasafiri wala kupunguza foleni katika jiji ila walionekana ni wapingaji tu.
Inawezekana wapanga mji walinakiri tu yanayofanyika sehemu zingine duniani bila kuhusisha mazingira ya mji wao yalivyo.
 
Mamalishe wanataka tule mikorogo yao Mbezi tuanze kutapika kabla ya kufika
Msata, kibaya zaidi 'rambo' hazipo siku hizi. Msitulazimishe kula safarini.
 
Wewe umeongea point at least. Umetufungua akili zaidi

Tatizo tumeishi kwenye mazoea hadi tunafikiri ndio utaratibu au sheria.
Utaratibu wa bus kuishia terminal station utafungua fursa nyingi kwa madereva(shuttle buses) madereva na kampuni za mizigo (yaani unashuka begi linakufuata) ,watu wa motel na lodges kwa watu wanaoishi mbali na kituo kikuu ...Hizi ni fursa chache nilizofikiria kwa haraka .
 
huyu MAKALA atakuwa mkuu wa mkoa alietumikia muda mfupi sana Dar es Salaam.

yaani naishi Tabata kuna option ya kushushiwa Ubungo unanilazimisha nishushiwe huko porini Mbezi ili iweje?
Ndugu nina mashamba mikoani nilikuwa natumiwa chakula mara kwa mara ila sasa nimewaambia kuleni tu ikiwashinda uzeni maana tabu na gharama nilizopata kutoa mzigo mbezi hadi tabata ni bora ningekwenda soko la mabibo. kutoka stendi hadi daladala ziliko buku 5. zimejaa hazitaki mzigo. nikachukua bajaji elfu 16 hadi tabata. ongezea buku 2 kuutoa mle ndani. Makala Makala...
 
Utopolo mtupu.
Fahamu Asilimia 90 ya wasafiri wanoutumia mabasi ni wanyonge ambao Kondakta akisahau kurudisha hata buku ya chenji zitawaka ndani ya gari.
Tatizo tumeishi kwenye mazoea hadi tunafikiri ndio utaratibu au sheria.
Utaratibu wa bus kuishia terminal station utafungua fursa nyingi kwa madereva(shuttle buses) madereva na kampuni za mizigo (yaani unashuka begi linakufuata) ,watu wa motel na lodges kwa watu wanaoishi mbali na kituo kikuu ...Hizi ni fursa chache nilizofikiria kwa haraka .
 
Naunga mkono hoja. Baadhi ta wenye mabasi wenye stendi zao pale Sinza Shekilango kama Kilimanjaro, Dar Lux, Marangu Coach na mengine, wenye mabasi zaidi ya moja kwa route ya Moshi Arusha, njia rahisi kwao ni route ya Bagamoyo Msata, na sio njia ya Chalinze, kuwalazimisha lazima waanzie Stendi mpya ni kuwatesa tuu bure abiria, after all, wengi wa abiria wa mabasi hayo, haswa wale abiria wa 1st Class, sio wa type ya kununua vitu kwa machinga au kula kwa Mama Ntilie! Hivyo kama nia ni kuwasaidia Machinga na mama ntilie, then, hizo ni sababu alizotoa Mkuu wa Mkoa ni sababu za kijinga sana!.

Hatuwezi kuendelea kuendesha nchi kijinga jinga hivi halafu utegemee tutapata mafanikio. Il tuendelee , la kupata maendeleo ya kweli de must stop such nonsense!.

p
Kitu kimachonikera kwa hii stand ya mbezi ni wale madalali kukukaba tangu unaingia Getini. Watakufwata mpaka gari unayotaka kupanda na ukifika kwenye gari/bus husika nauli inapanda. Mf. Nauli 16000 utaambiwa 18000.
Abiria unabaki na mshangao je ni kilometres zimeongezeka au kuna tofauti ya nauli kutoka Mkoa X kwenda dar,nakutoka dar kurudi mkoa X
 
Ukiangalia kwa makini, huu sio utaratibu wa Makalla. Ni lazima kuna sheria zinazosimamia mambo haya. Ni bora kujiridhisha na hizo kwanza kabla ya kulaumu.

Haya mabasi yote, liseni zao zitakuwa zinaonyesha wanafanya kazi katika vituo vipi na vipi na njia watakazotumia kufika huko wanakokwenda kwa uwazi kabisa. Hawana liseni ya kusafirisha abiria tokea Temeke kwenda standi kuu.
Wewe hili unaweza kuliona kuwa dogo, lakini ni sheria, na linahusu mambo mengi.

Wewe unayepandia Temeke, ajali ikikupata kabla hujafika stendi kuu, hao wenye basi wataeleza nini?

Unasema usafiri wa anga ni tofauti na ardhini, ndiyo, lakini katika mambo mengi vyote vinafanana..Kukiwa na uwanja wa ndege Morogoro, na pawe na ndege zinazoanzia Morogoro na safari zao, lakini hawawezi kwenda nje ya nchi bila kupitia JKNIA. Huu ni mfano ninaoweza kukufafanulia vizuri, lakini ngoja niuachie hapa ukining'inia...

Hapa ndipo nisipoelewa. Mabasi yanayoondokea Tandika yanaanza safari moja kwa moja kwenda Kusini na wala hayarudi Stendi Kuu. Hapo awali palikuwa na mabasi yaliyokuwa yanaanzia safari Ubungo na kupitia Tandika. Na yakirudi yanaishia Tandika. Hamna aliyekuwa anapanda basi Tandika kwenda Ubungo halafu kurudi kuelekea Kusini.

Usafiri wa ndege hivyo hivyo. Ukiwa arusha unaweza kuondokea Arusha Airport au KIA. Hauambiwi kuwa kwa sababu ulipandia Arusha Airport lazima upitie KIA. Kuna ndege za KIA na ndege za Arusha. Aidha sio kweli kuwa hauwezi kwenda nje ya nchi bila kupitia JKNIA. Unaweza kuanzia safari KIA au Zanzibar bila kushuka JKNIA. Miji mikubwa kama London, New York n.k. wana viwanja vya ndege zaidi ya kimoja ambavyo mtu unaweza kuondokea.

Huu uamuzi ulitakiwa ufanyike baada ya tathmini ya wataalam kuhusu athari zake kwa watumiaji na mji. Kwa mfano, kulazimisha mabasi yote yanayotoka kusini kupita mjini kwenda Mbezi ni kuongeza msongamano wa magari, uchafuzi wa hali ya hewa, kuongeza kelele, kuongeza uwezekano wa ajali n.k. Na hata yakianzia Mbezi yataendelea kupakia abiria Tandika na Mbagala. Labda serikali izuie na hilo.

Amandla...
 
Wewe ndio Kilaza mkubwa. Unafikiri kila kitu kinachofaa Mwanza, Arusha au Mbeya kitafaa Dar es Salaam. Dar es salaam ni Dar es Salaam na hayo majiji mengine ni hayo. Binadamu mwenye akili njema anajifunza kwa wenzake kisha anaongezea na ubunifu wake kulingana na mahitaji ya mazingira yake.
Wewe ambaye si kalaza hebu tupe mfano wa mji mkubwa wenye kariba ya kutumia akili zako, tujifunze!.
 
😬
Naona kama unatudanganya sasa. Tutajie kifungu cha hiyo 'Transportation Contract Regulations' inayo specify exactly wapi basi lako litaanzia na kuishia safari zake. Unataka kutuambia mabasi yote yaliyokuwa yakianzia safari zao Tandika na Shekilango walikuwa wanakiuka taratibu na serikali ilikuwa inawaangalia tu?

Hamna mtu aliyesema kuwa kila mmiliki awe na terminal yake, kama ilivyokuwa kwa Scandindavia ( ambae alitumia terminal ya Kamata) na hao wa sasa waliowekeza Shekilango. Kama sheria kama hiyo ipo basi Manispaa husika zilikosea kuwapa vibali vya ujenzi katika maeneo hayo.

Kutokujua basi lako linapotokea mjini Nairobi ni uzembe wako na sio wa wenye mabasi. Hasa huu wakati wa simu janja ambapo unaweza ku google basi litatokea wapi na kujipanga ipasavyo. Aidha, ukienda katika stendi yeyote utaelekezwa mabasi unayo hitaji yanaanzia wapi. Hapo zamani ilikuwa ukienda Ubungo wakati unataka kwenda Lindi utaambiwa uende Tandika. Ukikazania kwenda Kariakoo kulitafuta basi itakuwa ni uzembe wako.

Sisi ambao unatuona kama vile hamnazo tunahoji ulazima wa kuwa na kituo kimoja cha mabasi yeyote katika mazingira yafuatayo:
1. Kituo kinachopendekezwa hakiwezi kutoa huduma hiyo kwa miaka michache ijayo.
2. Miundo mbinu ya kuwafanya watu waweze kufika na kutoka hapo kwa urahisi haitoshelezi. Mnazi Mmoja inayozungumziwa na wengine ilikuwa inafikika kirahisi kutokana na ukaribu wake na Kariakoo, hivyo hivyo kwa Kisutu.
3. Upatikanaji wa huduma za watu kuweza kulala stendi wakisubiri usafiri.

Ukweli ni kuwa kituo kimejengwa bila tathmini ya kutosha ya mahitaji ya watu wanaotumia usafiri wa mabasi ya kawaida. Ni kama vile kujenga soko kwa mfano wa Mlimani City, hayatalipa.

Watawala wangeachia utaratibu uliopo uendelee wakati wakiboresha miundo mbinu ya kuwafikisha na kuwatoa abiria kwenye kituo hicho na vingine vilivyopo. Ni mawazo potofu kuvunja masoko yaliyo jirani na makazi ya watu na kuyahamisha kusiko na watu kwa kutegemea watu watapanda dala dala kwenda kununua tungule. Watarudi tu kufuata wateja.

Amandla...
Rudia kusoma nilichoandika, naona umekuja na povu pasi kuelewa.
 
Naunga mkono hoja. Baadhi ta wenye mabasi wenye stendi zao pale Sinza Shekilango kama Kilimanjaro, Dar Lux, Marangu Coach na mengine, wenye mabasi zaidi ya moja kwa route ya Moshi Arusha, njia rahisi kwao ni route ya Bagamoyo Msata, na sio njia ya Chalinze, kuwalazimisha lazima waanzie Stendi mpya ni kuwatesa tuu bure abiria, after all, wengi wa abiria wa mabasi hayo, haswa wale abiria wa 1st Class, sio wa type ya kununua vitu kwa machinga au kula kwa Mama Ntilie! Hivyo kama nia ni kuwasaidia Machinga na mama ntilie, then, hizo ni sababu alizotoa Mkuu wa Mkoa ni sababu za kijinga sana!.

Hatuwezi kuendelea kuendesha nchi kijinga jinga hivi halafu utegemee tutapata mafanikio. Il tuendelee , la kupata maendeleo ya kweli de must stop such nonsense!.

p
Naona leo mzee wangu umeamua KUMFOKEA MTU!!, tatizo la viongozi wetu huwa wanapenda huifurahisha hadhara inayomsikiliza kwa mtu huo bila kutafakari hizo kauli zao ki mantiki!!siku hizi kuna mabasi yanaanzia safari zao , kigamboni, mbagala hadi chanika, hivyo asubuhi inakuwa rahisi kwa abiria wa maeneo hayo kuanza safari, na hata ile usiku wanapotoka mikoani yanakuja kuwashushia huko huko!!, eti mama lishe,!!!
 
Tunaweza mlaumu sana Mheshimu mkuu wa mkoa lakini kumbe anamefanya hivyo kwa kushughulikia matatizo ya wananchi. Juzi nilikuwa nasafiri toka Arusha kisha nikapanda basi nisingependa kulitaja basi hili lina stand binafsi jirani Ubungo, tulipofika Bomang'ombe akapanda abiria wakati akipanda huyo abiria ni mama pamoja na wanaye wawili alidai yeye kwamba yeye anashukia mbezi. Konda akamwambia umefika mama. Tulipofika msata gari ikafuata barabara ya Bagamoyo. Yule mama akakumbusha konda sisi tunashuka mbezi hii gari mbona inapita huku. Konda akamwambia si unataka mbezi stendi kuu utafika mama. Tulipofika kwenye stendi ya basi husika maeneo ya Shekilango yule konda alimkabidhi yule mama Tsh 2000 akimwambia chukua daladala panda utafika mbezi mama akagoma akasema yeye hawezi kuanza kuhangaika na mizigo kupanda daladala. Baadhi ya abiria wakawa waungwana kumtetea mama kwamba mama alikwisha toa taarifa tangu anapanda kwenye gari kwamba yeye anaenda mbezi na si Shekilango kwa hiyo ni swala la kumuwezesha afike alikosema anakwenda.
Bahati nzuri akajitokeza abiria mmoja aliyekuwa amepokelewa na ndugu yake usafiri binafsi akamwambia mama nitakusaidia kukufikisha Mbezi panda kwenye hiyo gari mzozo ukawa umeisha. Mimi nilikuwa nimeazimia kwamba sitoki pale mpaka mama amepata msaada naye ameridhika.
 
Back
Top Bottom