Napinga hoja ya RC Makalla ya kulazimisha Mabasi yote ya Mikoani kupakia na kushusha abiria Stendi ya Magufuli pekee

Mkuu, hatutofautiani, ila nadhani ni kutoelewa tu.

Mimi sijasema popote toka mwanzo kuwa Makalla yupo sahihi, bali ninachosema ni kwamba sababu alizoshirikisha ni za kisiasa tu. Sababu muhimu zipo kwa nini hayo mabasi yanatakiwa kupakia na kushusha abiria Stendi Kuu, na nimekwishazitaja katika maandiko yangu humu.

Sijaandika sehemu yoyote kupinga kuwepo kwa usafiri mwingine wanaoweza kuumudu wasiokuwa na uwezo wa taxi. Sote tunajua uwezo mdogo uliopo kuondoa matatizo yanayowakabili wananchi, siyo wasafiri pekee. Kuwepo kwa kituo cha mabasi ni hatua moja, tuendelee kutafuta njia za kufanikisha kitupo hicho kifanye kazi kwa ufanisi. Yote hayawezi kuja kwa wakati mmoja.
Hii kali sana.
 
Lazima niseme, hii ni ngumu mkuu Erythro.

Pamoja na pendekezo lako la mabasi hayo lazima yapitie Stendi kuu, bado naona Makalla yumo ndani ya mstari, hata kama yeye atakuwa na msukumo wa maslahi tofauti na matakwa ya mabasi hayo kuanzia na kuishia stendi kuu.

Stendi kuwa mbali na mjini siyo hoja, kwa sababu stendi kuu ni lazima ihudumiwe na usafiri toka sehemu zote za mji, kwa hiyo hiyo ni fursa kwa wenye biashara zao za usafirishaji mjini.

Ni sawa na uwanja wa ndege, ambako ukitaka kusafiri, kama unatokea Kawe, ni lazima utafute usafiri wa kukufikisha JKNIA, na hivyo hivyo, kama unaingia, utapata usafiri toka hapo kukupeleka Kawe.

Mimi naona la msingi zaidi ni Makala kuhakikisha sehemu zote za mji wake zipo huduma za kuwafikisha wananchi Stendi kuu ya mabasi, Mbezi Luis.

Lakini pia inabidi niulize swali hapa: kuna ubaya wowote kwa mfano kuwepo kwa vituo kadhaa vya mabasi mjini Dar, kwa mfano kituo cha mabasi yanayoelekea kusini mwa nchi kikawepo Mbagala; kituo cha mabasi yaendayo Nyanda za juu yakaanzia, tuseme Gongo La Mboto, n'k.?

Vipi, mbona hujachangamkia fursa ya Hotel/Guest maeneo hayo mkuu Erythrocyte!
Wajenge stendi zaidi ya moja... UKIZINGATIA kutoka nje ya Dar kuna kuna njia kubwa 3 tu..!! Kila road, Morogoro road na Bagamoyo road...
 
Huu utaratibu upo mikoa yote, Ila Dar ilikuwa haijaguswa, Sasa mmeguswa full matusi, mbona mnajiona special Sana, waliotembea kidogo duniani wanasema utaratibu huu upo miji mingi mikubwa duniani, nyie mnataka kila mtu Basi limshushe nyumbani kwake.

Mbona wenzenu wa mkoa tunavumilia, tukiingia saa nane usiku, tunakodi bajaji hadi home!!!
Usisahau huko wanakokubali Luna mashoga pia..!! Si kila kifanywacho huko kwingine lazima kifanywe huku kwetu
 
Wajenge stendi zaidi ya moja... UKIZINGATIA kutoka nje ya Dar kuna kuna njia kubwa 3 tu..!! Kila road, Morogoro road na Bagamoyo road...
kwa Hatua ya sasa hatukuwa na shida sana na stendi mpya kila mahali , ombi letu lilikuwa ni kuacha Magari yatumie yard zake hata kama ni lazima yapite kwenye stendi ya Mbezi , tusiseme wapakie na kushusha mbezi tu
 
Amos Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mfadhili wa zamani wa bendi ya FM ACADEMIA ya Kinondoni, bila kufanya utafiti wowote ule leo ametoa amri ya kulazimisha mabasi yote ya mikoani kuanzia safari zao kwenye kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Mbezi Luis, kinachoitwa kituo cha mabasi cha Magufuli na kushushia abiria wake hapohapo.

Lengo kuu la kauli yake hii ni kujaribu kukusanya watu ili kuneemesha wafanyabiashara waliojazana kwenye stendi hiyo bila mpangilio wowote, Makalla anaamini kwamba abiria wote wakishushwa ama kuanzia safari zao hapo basi watanunua bidhaa za wamachinga waliojazana hapo, hivi ndivyo akili yake ilivyomtuma, kwamba abiria wakomeshwe ili kufurahisha wafanyabiashara, amesahau kwamba abiria ni bora kuliko wamachinga kwenye mustakabhali wa Safari, hata hivyo sikubaliani naye.

Mbezi Luis eneo ilikojengwa Stendi ya Mabasi ya Mikoani ni nje kabisa ya jiji la DSM , kulazimisha Mabasi yaliyokuwa yanaanzia safari zake Mbagala, Tandika au Kigamboni kuacha kazi hiyo na kulazimisha sasa lazima yote yaanzie Nje ya jiji ni sawa na unyama , kwamba sasa aliyekuwa anapandia basi Mbagala akodi teksi kwa zaidi ya gharama ya tsh elfu 30 ili kulifuata basi Mbezi Luis, kwa vile tu Amos Makalla kajisikia hivyo haikubaliki na ni lazima ipingwe kwa nguvu zote.

Alichotakiwa kufanya Mh RC ni kuhakikisha kwamba basi lolote kutoka kwenye yard yoyote ile binafsi linakoanzia safari lisiondoke DSM bila ya kupita Stendi kuu ama lishushe litakako ila ni lazima lije stendi kuu, Vinginevyo Mh Makalla atamke hadharami Maslahi yake binafsi atakayopata kwa kuwatesa abiria wa Kigamboni, Vikindu , Chamanzi, Mbagala, Tandika na kwingineko waliokuwa wanapata ahueni ya kuanzia safari kwenye maeneo yao ya karibu.

Naomba kuwasilisha.
Mkuu umepiga kwenye mshono Mimi bado nasimama na PR Asad alisema viongozi wengi nchi hii ni wajinga sana
 
Naunga mkono hoja. Baadhi ta wenye mabasi wenye stendi zao pale Sinza Shekilango kama Kilimanjaro, Dar Lux, Marangu Coach na mengine, wenye mabasi zaidi ya moja kwa route ya Moshi Arusha, njia rahisi kwao ni route ya Bagamoyo Msata, na sio njia ya Chalinze, kuwalazimisha lazima waanzie Stendi mpya ni kuwatesa tuu bure abiria, after all, wengi wa abiria wa mabasi hayo, haswa wale abiria wa 1st Class, sio wa type ya kununua vitu kwa machinga au kula kwa Mama Ntilie! Hivyo kama nia ni kuwasaidia Machinga na mama ntilie, then, hizo ni sababu alizotoa Mkuu wa Mkoa ni sababu za kijinga sana!.

Hatuwezi kuendelea kuendesha nchi kijinga jinga hivi halafu utegemee tutapata mafanikio. Il tuendelee , la kupata maendeleo ya kweli de must stop such nonsense!.

p
Mkuu umemaliza kazi siongezi neno hata moja
 
Naafikiana nawe 100% ila napingana nawe 100% kumwita mtu mwenye akili za Makala mheshimiwa, Makala hastahili kuheshimiwa kwa lolote, kwa mtazamo huo ipo siku hata vibaka watapewa heshima, kitendo alichofanya Makala ni economic rapping, na hii huenda ina agenda ya siri nyuma yake kwa manufaa yake binafsi. He is stupid!!
Mia mia
 
Daudi Mchambuzi said:
CAG alivyosema kuwa hiyo stand kuwepo eneo hilo ni hasara tupu, mataga pori walimshambulia kwa maneno ya kejeli sasa leo kibuyu kimeitika

Na bado mengi yaja kuumbuka hakutaisha
 
Hatua nyingi za viongozi wa umma si kufanya maisha ya watu kuwa marahisi, ila ni kuongeza ugumu tu.
 
Hiyo yote ni kutaka kustawisha miradi yao kupitia watu masikini, na mbaya zaidi makosa hayo watayarekebisha 2025 ili waonekane wametatua tatizo ambalo walilitengeneza wao wenyewe kwa makusudi
 
Very sad aisee!
 
Amos Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mfadhili wa zamani wa bendi ya FM ACADEMIA ya Kinondoni, bila kufanya utafiti wowote ule leo ametoa amri ya kulazimisha mabasi yote ya mikoani kuanzia safari zao kwenye kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Mbezi Luis, kinachoitwa kituo cha mabasi cha Magufuli na kushushia abiria wake hapohapo.

Lengo kuu la kauli yake hii ni kujaribu kukusanya watu ili kuneemesha wafanyabiashara waliojazana kwenye stendi hiyo bila mpangilio wowote, Makalla anaamini kwamba abiria wote wakishushwa ama kuanzia safari zao hapo basi watanunua bidhaa za wamachinga waliojazana hapo, hivi ndivyo akili yake ilivyomtuma, kwamba abiria wakomeshwe ili kufurahisha wafanyabiashara, amesahau kwamba abiria ni bora kuliko wamachinga kwenye mustakabhali wa Safari, hata hivyo sikubaliani naye.

Mbezi Luis eneo ilikojengwa Stendi ya Mabasi ya Mikoani ni nje kabisa ya jiji la DSM , kulazimisha Mabasi yaliyokuwa yanaanzia safari zake Mbagala, Tandika au Kigamboni kuacha kazi hiyo na kulazimisha sasa lazima yote yaanzie Nje ya jiji ni sawa na unyama , kwamba sasa aliyekuwa anapandia basi Mbagala akodi teksi kwa zaidi ya gharama ya tsh elfu 30 ili kulifuata basi Mbezi Luis, kwa vile tu Amos Makalla kajisikia hivyo haikubaliki na ni lazima ipingwe kwa nguvu zote.

Alichotakiwa kufanya Mh RC ni kuhakikisha kwamba basi lolote kutoka kwenye yard yoyote ile binafsi linakoanzia safari lisiondoke DSM bila ya kupita Stendi kuu ama lishushe litakako ila ni lazima lije stendi kuu, Vinginevyo Mh Makalla atamke hadharami Maslahi yake binafsi atakayopata kwa kuwatesa abiria wa Kigamboni, Vikindu , Chamanzi, Mbagala, Tandika na kwingineko waliokuwa wanapata ahueni ya kuanzia safari kwenye maeneo yao ya karibu.

Naomba kuwasilisha.
ah
 
Wajenge stendi zaidi ya moja... UKIZINGATIA kutoka nje ya Dar kuna kuna njia kubwa 3 tu..!! Kila road, Morogoro road na Bagamoyo road...
Hilo nipendekezo moja; lakini bado watakuwepo wasafiri toka mbali na vituo hivyo watakavyovitumia, hata kama watakuwa ni wachache.

Kituo kimoja kiwe Tandika, kuna wasafiri watakaokitumia wakitokea Bunju; hali ni hivyo hivyo na vituo vingine vitakavyojengwa kwingine.
 
Amos Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mfadhili wa zamani wa bendi ya FM ACADEMIA ya Kinondoni, bila kufanya utafiti wowote ule leo ametoa amri ya kulazimisha mabasi yote ya mikoani kuanzia safari zao kwenye kituo kikuu cha mabasi ya mikoani cha Mbezi Luis, kinachoitwa kituo cha mabasi cha Magufuli na kushushia abiria wake hapohapo.

Lengo kuu la kauli yake hii ni kujaribu kukusanya watu ili kuneemesha wafanyabiashara waliojazana kwenye stendi hiyo bila mpangilio wowote, Makalla anaamini kwamba abiria wote wakishushwa ama kuanzia safari zao hapo basi watanunua bidhaa za wamachinga waliojazana hapo, hivi ndivyo akili yake ilivyomtuma, kwamba abiria wakomeshwe ili kufurahisha wafanyabiashara, amesahau kwamba abiria ni bora kuliko wamachinga kwenye mustakabhali wa Safari, hata hivyo sikubaliani naye.

Mbezi Luis eneo ilikojengwa Stendi ya Mabasi ya Mikoani ni nje kabisa ya jiji la DSM , kulazimisha Mabasi yaliyokuwa yanaanzia safari zake Mbagala, Tandika au Kigamboni kuacha kazi hiyo na kulazimisha sasa lazima yote yaanzie Nje ya jiji ni sawa na unyama , kwamba sasa aliyekuwa anapandia basi Mbagala akodi teksi kwa zaidi ya gharama ya tsh elfu 30 ili kulifuata basi Mbezi Luis, kwa vile tu Amos Makalla kajisikia hivyo haikubaliki na ni lazima ipingwe kwa nguvu zote.

Alichotakiwa kufanya Mh RC ni kuhakikisha kwamba basi lolote kutoka kwenye yard yoyote ile binafsi linakoanzia safari lisiondoke DSM bila ya kupita Stendi kuu ama lishushe litakako ila ni lazima lije stendi kuu, Vinginevyo Mh Makalla atamke hadharami Maslahi yake binafsi atakayopata kwa kuwatesa abiria wa Kigamboni, Vikindu , Chamanzi, Mbagala, Tandika na kwingineko waliokuwa wanapata ahueni ya kuanzia safari kwenye maeneo yao ya karibu.

Naomba kuwasilisha.
Umenena ukweli wa zaidi ya asilimia [emoji817] Congratulations! Yaani mtu anaenda Dar es Salaam anashushwa Mbezi Majanga. Mifumo ya kizamani sana! Halafu hapo Mbezi aanze tena safari nyingine! Ya mambo ya mapato yanatuharibia mambo.
 
Iwe kali iwe poa, ukweli unabaki pale pale.

Ni wapi duniani matatizo ya kuhudumia matabaka yote ya watu yanakamilishwa kwa wakati mmoja?

Kituo kimejengwa, hiyo ni hatua moja, hatua nyingine zitafuata kadri mipango itakavyoweza kuyatimiza, hatua kwa hatua.
Inaendelea kuwa kali zaidi
 
Back
Top Bottom