Napinga kabisa dhana ya "Mume ni Provider" katika ndoa

Napinga kabisa dhana ya "Mume ni Provider" katika ndoa

1. Babu yangu was a real man, alikuwa na watoto 12 na alibeba majukumu ya kumtunza bibi na baba zangu na mashangazi. ndio maana na babangu kawa real man.

2. Babangu alikuwa real man, alikuwa na watoto 8, wote alitutunza na alibeba majukumu yote kama provider kwa mama na kwetu na akanisomesha pia.

3. Mimi ni real man, nina watoto 6, mke wangu namtunza na nafurahia ninavyokuwa provider, watoto pia. in reality, mke wangu akiwa na hela huwa sihesabu sana kama yetu, mimi ndiye provider hiyo ya kwake, najiona kidume zaidi anapotumia pesa zangu na mimi natafuta kwa bidii kwaajili yake na watoto.


4. wewe inawezekana sio real man, ndio maana unakwepa majukumu, unataka kulelewa na wanawake. Mwanaume halisi hayupo hivyo. badilika.
Umeandika mke wako akiwa na hela hauhesabu Sana Kama za familia,

Maana yake unazihesabu kidogo!
[emoji28][emoji28]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimi sinaga tabia ya kuomba, kwanza sipendi kabisaa na naichukia hiyo tabia..!!
Kuna namna najiona vipi sijui!! Mpaka naomba basi ujue nimejikanyaga mpk basi.
basi huna tofauti na ombaomba ila mbinu tofauti 😎😂😂😂
 
Ndio, napinga!,

Ni dhana ya uongo na inakiuka kabisa asili ya maisha ya ndoa!

Ndoa ni muunganiko wa mtu mume na mtu mke na kuzaa watoto kisha kuwatunza. Jumuia hii ya familia inahitaji mahitaji mbalimbali ya maisha kwa maendeleo yake.

Kuna watu wachache wanaibuka hapa bila hata chembe ya aibu na kutaka kuuaminisha umma kuwa mtu mume yampasa kutafuta mahitaji ya familia but mtu mke pamoja na watoto hawawajibiki.

Wanaume wanapolalamika kwamba wanawake kwenye ndoa wanapenda kuhudumiwa zaidi kuliko kuhudumia, wanaibuka watu hawa na vicomment vyao eti ni jukumu la mume kuprovide, na hiari ya mke kuprovide! Salaleee!

Najaribu kujiuliza hii dhana wanaitoa wapi? Ni taasisi gani imefundisha hivi? Au ni ubunifu katika fikra zao?

Katika Ukristo haipo sijui kule kwa wenzetu!

Kwa Wakristo ipo wazi;

"Zaeni mkaongezeke, mkaijaze dunia na kuimiliki"

Kauli ya Mungu kwa mume na mke ikiashiria ushirikiano wa pamoja katika kuijenga familia na dunia kwa ujumla.

"Si vema mwanaume awe pekeyake, nitamfanyia msaidizi wake"

Kauli ya Mungu ikiashiria matakwa yake ya mke kuwa msaidizi kwa mume. Then why mume awe provider bila kusaidiwa?

"Mume na mke watawaacha wazazi na kuungana na kuwa mwili mmoja"

Kauli ya Mwana wa Mungu ikiashiria ndoa ni mshikamano kwa raha na shida hadi kifo kiwatenganishe.

Then mshikamano gani huo wa mmoja kuprovide?

"Mwanamke amtii mumewe na mwanaume ampende mkewe"

Kauli ya mtume wa Mwana wa Mungu ikiashiria kuwa mwanamke awe tayari kutumika kwa hali na mali mbele ya mumewe.

Maisha halisi ya mwanadamu tangu kale yapo wazi. Mwanaume na mwanamke wamefanya kazi pamoja kwa ajili ya maisha yao.

Tangia enzi za Adam na Eva, enzi za manabii, enzi za Yesu Kristo, nyakati za mitume, nyakati za mwanzo za kanisa Katoliki, nyakati za mtume Mohammed hadi leo, mume na mke wameshirikiana katika kazi.

Wamelima pamoja, wamefuga pamoja.

Mume alivua samaki na mke aliwapika wakala,

Mume alitengeneza visu na mke alitengeneza vyungu na makapu wakauza na kupata riziki ya maisha yao.

Hayo yote yalifanyika kwa maelfu ya miaka iliyopita!

Vipi wewe leo kisa una kijikampuni chako unapata fedha, eti unaanza kuleta propaganda kuwa mahitaji ya familia ni jukumu la mume!

Ikumbukwe dunia imebadilika.

Kwa sasa uchumi hauna mwenyewe tena.

Mwanaume au mwanamke aweza kuhodhi uchumi mkubwa.

Leo hii mke aweza kuwa waziri au raisi na akapata mamilioni ya fedha.

Je, hayo mamilioni ya fedha apeleke wapi iwapo hapaswi kuprovide na kujenga familia yake?

Leo una mshahara mnono au kampuni inakupa fedha nyingi halafu unahisi unaweza kuhudumia familia kwa 100%, then unaanza kuwatukana waume wenzako kuwa hawatakiwi kushirikiana na mke katika kuhudumia familia.

What if mtu kama JPM anakufukuza kazi au anaifilisi kampuni yako, yule mke wako afisa maendeleo ya jamii pale Halmashauri asihudumie familia yenu?

Unajua wakati mwingine watu wakiwa na pesa, pesa zinawalevya na wanaongea vyovyote!

Hii dhana ya wanawake kupenda kuhudumiwa tu bila kuwajibika hata kama uwezo wanao ni dhana mpya! Na imejengwa na waume wenye fedha pale wanapowarubuni kwa kuwaambia, "We mtoto mzuri hautakiwi kupata shida, wakati mwanaume nipo kwa ajili yako, nitakuhudumia chochote utakacho!"

Kauli hizi zimewaharibu wanawake wengi sana.

Mabibi na mabibi zao tangu kale hawakujua huu ujinga. Wao walijua kuolewa ni kazi! Kuamka, kufanya usafi, kwenda kushirikiana na mume shambani, au malisho ya ng'ombe! Leo mwanamke anamshahara wake hataki utumike nyumbani!

Kwani kuna tofauti gani na bibi yetu aliyesuka kapu akauza na pesa ikatumika nyumbani?

Hivi nyie wanaume muliyewapotosha wanawake kwa dhana potofu ya mume ni provider, mumetumia msingi gani wa elimu?

Hapana, mume na mke wawajibike pamoja kuijenga familia. Mume ukiamua kuwa provider, na iwe kwa maamuzi yako, na usishinikize kuwa principle ya ndoa. Kwani maisha hayo si asili ya mwanadamu tangu kale. Labda kama unakusudia kuleta mapinduzi ya mfumo wa uwajibikaji katika ndoa!

Kuna sehemu nilisoma andiko la mwanamke akiwahoji wanaume kwanini awajibike kumtii mume wakati anasaidia kuprovide mahitaji ya ndani?

Swali hili ni sawa na kumhoji mkurugenzi kwanini umtii wakati unachangia maendeleo ya taasisi? Swali hili alitakiwa aliulize Eva kwa Mungu wake.

Bahati mbaya cheo hiki alishapewa mwanamume tayari. Ukimtii Mungu utatii na neno lake. Familia ni taasisi ambayo lazima awepo kiongozi wakuweka direction za maisha. Hata hivyo haulazimiki kutii chochote. Unapaswa kumtii mume kwa yote yaliyomema. Mungu alishafanya uteuzi, labda tusubiri utenguzi na ateuliwe mwanamke siku za usoni!

Mke wajibika kuprovide kwa familia yako pale inapowezekana. Usikwepe wajibu ilihali mukiachana unadai mgao hamsini kwa hamsini.

Mume akifa unadai urithi wa mali zote!

Hata hivyo, hapa, nikiri kwamba asilimia kubwa ya wanawake wanajitoa na kuprovide kwa familia zao. Asanteni sana!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Naomba nikushauri kijana; ni vyema ukajiunga na kundi la kataa ndoa. You are too dumb and soft to be somebody's husband and a responsible head of the family.
 
Kuna 50/50 ya aina mbili.

Traditional 50/50

Mama anafanya kazi (akipenda, na hela ni ya matumizi anayotaka) na mara nyingi si kazi nzito, akili yake inakuwa kwenye kutunza mume na watoto watakaojaliwa huku mwanaume akihudumia familia kila kitu.

50/50 modern imbalanced (napenda kuiita 70/30)

Hii wote mnafanya kazi na kuleta hela nyumbani.
Ila mwanamke bado anafanya kazi ya kubeba mimba, kuzaa kwa uchungu, kulea, kupika na kulipia watoto Ada, kodi n.k (70%)

Mwanaume akichangia mbegu na pesa kwa jinsi awezavyo pekee (30%)

Wewe unataka 50/50 ipi?

Kwa mwanamke kubeba mimba na kuzaa, kisha kulea , tayari anaanza na 50% ya mchango wake kwa familia, hivyo ungependa aongeze ngapi kusaidia zaidi?
Leo ndio nasikia kutoka kwako kuwa kuzaa ni 50% ya majukumu ya familia, inashangaza!!

Kwanza picha inaanza kwa mume kumpiga miti mke,

Uja uzito tangu umeanza hadi miezi sita ni hakuna uchungu

Uchungu wa uja uzito unaanza labda miezi Saba Hadi tisa na siku yenyewe ya labour!
Hio ni miezi mitatu ya uchungu wa kuzaa

Mtoto akizaliwa Kuna jukumu la kulea mtoto, hapa baba anashiriki. Kubeba mtoto, kumuogesha, kumvisha, kucheza nae kwenye kochi, kumpeleka hospitali n.k

Uchungu wa miezi mitatu wa kuzaa haiwezi kuthaminishwa na uchungu wa kutunza maisha ya watu wa familia kwa miaka 30

Mwanamke mwenyewe ukimwambia achague kukaa pekeyake miaka 30 bila kupewa uchungu wa kuzaa, au kukaa na mume ampe uchungu wa kuzaa atachagua Nini?

Kumbuka Eva alizaa kwa uchungu Kisha akaendelea na kazi za shamba ili kutunza familia yao

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Najaribu kujiuliza hii dhana wanaitoa wapi? Ni taasisi gani imefundisha hivi? Au ni ubunifu katika fikra zao?

wewe hii dhana umetoa wapi mkuu?

maandiko yanatuambia mwanamke atazaa kwa uchugu na mwanaume atakula kwa jasho lake.
maana yake mwanaume kazi yako ni kupambana na kuhakikisha familia ina kula vzr na kuishi vizuri.

maandiko yanatumbia mwaanaume ni kichwa cha familia{mke wake}
 
Back
Top Bottom