Pre GE2025 Napinga Kauli ya Rais Samia kwamba Utekaji ni Drama, hii ni dharau kwa Wananchi

Pre GE2025 Napinga Kauli ya Rais Samia kwamba Utekaji ni Drama, hii ni dharau kwa Wananchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hawa watu kama ni Kodi kuwalevya basi imewalevya kwelikweli !!.

Imagine ni Rais wa Nchi, Rais ambaye Mara Kadhaa anashuhudia Taarifa Mara Kwa mara juu ya Kupotea, kutekwa n.k Kwa Watanzania .

Leo unasimamia mbele ya watu kusema Utekaji ni DRAMA?.

Ukiachilia mbali Urais, anayoyasema hayo ni MWANAMKE ambaye ana watoto, hivi kweli mtoto wake ndio angekua ametekwa angediriki kusema haya ??.

Huu utekaji na mauaji ya kishenzi, hata Bungeni Akina MPINA wanasema Kila kukicha, Inakuaje wanyama wawe na haki sawa na uhai wa binadam?.

Kuna Vijana Kila siku wanapotea Kariakoo , hatuelezi chochote?.

Hawa watu wanaopotea, hata kama ni Wahaini, Si wakamatwe Kisha wafikishwe kwenye vyombo vya Sheria?.


Mambo ya Ajabu sana , tukubali tu, sisi Gen Z wa Tanzania ni wapuuzi, haiwezekan Vijana wenzetu tunaozunguka nao Kariakoo, wanapotea, ila kwakua sisi tuko salama kesho tunawahi kazin, tunasahau kua kesho ni zamu yetu.!!
Mbaya zaidi wananchi wako kimya, wako bize na simba na yanga na siasa, such things kwa watu wanao jielewa wangesha firce serikal ifanye kitu
 
Vitu vingne viache vikupite mkuu utahangaika mpaka lini, au na ww hujielewi🤣
Masikini waliojaribu kutuloga kama unavyofanya wewe ni wengi sana lakini wamepotea wao sisi tupo
 
Akuloge Nani unajiloga ww mwenyewe kwa kutolea povu vitu visivyokuhusu, sku nyngne tulia tu yakupte kamanda
Ungetulia wewe,Hukuitwa huku kwa uzi wa jamaa.Kama unaungana na rais kusema kutekwa kwa Watu ni Drama,Yule wa Tanga alipotea 29 days ndugu zake wanamtafuta vituo vyote hayupo. Polisi wanakuja kujibu baada ya siku 29 kuwa tunae.

Vipi kuhusu Sativa ambae hata matibabu Rais kamlipia. Je alitokaje Dar mpaka Manyara? Alijiteka akajipiga ns kujiumiza vile?

Hebu acha utahira wako
 
Kiswahili inaweza ikawa ni lugha ngumu kueleweka licha ya kwamba ndio lugha ya Taifa. Kama ulisikiliza mwanzo mwisho utabaini Rais hakusema kwamba kila tukio mtu kajiteka na alianza kuzungumzia tatizo na baadae ndio akasema kwamba wengine wanajiteka na mfano wa mtu kujiteka upo pengine umesahau tu, ABDUL NONDO aliwahi kujiteka kipindi cha Hayati Magufuli
Ndugu,tukumbuke huu msemo wa mtu kujiteka mwenyewe,uliletwa na polisi,...kama walivyomzushia Hamza ugaidi baada ya kumuua pale salender, na matukio mengine yanayo fanana na hayo,tutambue kuwa polisi wanaweza kufanya/kuzusha chochote ilimradi wafiche uovu wao pamoja na kuwafurahisha mabwana zao.Hivyo tusishangae, hata hii dhana ya mtu kujiteka wenyewe,nayo ikawa ni uzushi pia.Hii taasisi haiamiki.
 
Nanyi kweli mnakosa kazi kiasi cha kuweza msikiliza samia akiongea? Mna uvumilivu sana.
 
Ungetulia wewe,Hukuitwa huku kwa uzi wa jamaa.Kama unaungana na rais kusema kutekwa kwa Watu ni Drama,Yule wa Tanga alipotea 29 days ndugu zake wanamtafuta vituo vyote hayupo. Polisi wanakuja kujibu baada ya siku 29 kuwa tunae.

Vipi kuhusu Sativa ambae hata matibabu Rais kamlipia. Je alitokaje Dar mpaka Manyara? Alijiteka akajipiga ns kujiumiza vile?

Hebu acha utahira wako
Sativa ndo nani
 
Wakati nafikiria kuandika uzi huu, niliogopa kidogo kwa hofu hiyo hiyo ya kutekwa, lakini nikajipa moyo kwamba tukinyamaza hapa JF ni nani mwingine atasema?

Kwa Rais kusema hadharani kwamba masuala ya kutekwa watu yanayoendelea kwenye nchi anayoiongoza ni Drama, si tu kwamba ni uongo lakini pia ni kejeli isiyokubalika, Yaani watu watekwe na kupelekwa polisi na baadaye kutupwa kusikofahamika halafu tuaminishwe kwamba hizo ni Drama! ili kuamini jambo hili Tunapaswa tusiwe na akili kabisa au tuwe tumenyofolewa ubongo.

Ni kweli kwamba Mkubwa hakosei, lakini kwenye hili Mama Kakosea na anapaswa kuomba radhi, Vinginevyo awe tayari kuhusishwa na utekaji unaoendelea na kwamba Yeye ndiye anayewatuma Watekaji na ameamua kufunika ili kuepuka lawama.


"Nchi yetu ina sifa kubwa sana ndani ya ukanda wetu na duniani, sasa zikitoka ripoti hizi huyu kauawa, huyu katekwa, huyu kafanywaje aahh, na yakitokea mbio serikalini"

"Tukizungumza haya ya kutekwa haya, unasema katekwa nani? unasikia mtoto alijiteka mwenyewe anapiga simu kwao zitoke pesa, huku mama kamtekesha mwanawe ili baba atoe pesa, yani vidude vya drama drama tu hivi lakini vinavyoandikwa kwenye vyombo vya habari ni kama serikali imelala watu wanatekwa tekwa tu hovyo, naomba sana tusiyafumbie macho" - Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Machifu Ikulu Dodoma

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Rais Samia: Machifu waambieni wanasiasa ukweli vyeo havipatikani kwa kuua watu
 

Attachments

  • Screenshot_2024-07-20-14-00-47-1.png
    Screenshot_2024-07-20-14-00-47-1.png
    552.5 KB · Views: 4
  • VID-20240723-WA0032.mp4
    20.1 MB
The weird and extreme abduction has been taking place throughout Tanzania,and meantime the President recently cited that, there's no such a thing other than Drama,well, take a look at this Drama.👇

Screenshot_20240723-225931.png
 
Huko kwa akina Chaula majambazi na majangili wanataka wapewe milioni 3....
 
Back
Top Bottom