kama hata Samia hajui wanaoteka watu,basi hata yeye hayuko salama.ipo siku watamteka.
Wakati nafikiria kuandika uzi huu, niliogopa kidogo kwa hofu hiyo hiyo ya kutekwa, lakini nikajipa moyo kwamba tukinyamaza hapa JF ni nani mwingine atasema?
Kwa Rais kusema hadharani kwamba masuala ya kutekwa watu yanayoendelea kwenye nchi anayoiongoza ni Drama, si tu kwamba ni uongo lakini pia ni kejeli isiyokubalika, Yaani watu watekwe na kupelekwa polisi na baadaye kutupwa kusikofahamika halafu tuaminishwe kwamba hizo ni Drama! ili kuamini jambo hili Tunapaswa tusiwe na akili kabisa au tuwe tumenyofolewa ubongo.
Ni kweli kwamba Mkubwa hakosei, lakini kwenye hili Mama Kakosea na anapaswa kuomba radhi, Vinginevyo awe tayari kuhusishwa na utekaji unaoendelea na kwamba Yeye ndiye anayewatuma Watekaji na ameamua kufunika ili kuepuka lawama.
View attachment 3047088View attachment 3047092
Hivi mkuu mbona leo umeandika kama panya anayekula mguu wa mtu aliyelala, kuuma na kupuliza ili 'host' asiamke na kukasirika?
Nikawaza hivi, labda kuna mtu kaazima simu yako kuchezea ama hii michezo yao ya 'kuhaki' account za watu?
Iwe ni wewe kabisa og usijue namna taasisi za kiserikali zinavyofanya kazi, kwa hili siamini!
Kuna usalama ama Polisi gani anayefanya kazi bila kupewa 'order' na mkubwa wake?
Iko hivii, hawa watu wanaoikosoa Serikali na kisha kutekwa na kupotezwa, anayebariki hayo yote ni Rais mwenyewe, kwa kuagiza yeye ama kwa kushauriwa, lakini ni lazima taarifa awe nayo.
Na amri ya utekekezaji hushushwa kwa maandishi ya siri ambayo wasiohusika hawawezi kuelewa mpango huo.
Jambo lolote kubwa la kuchezea maisha ya mtu halafu eti vyombo vyote vya dola visiwe na habari ni utani wa matusi ya nguoni.
Kazi hiyo ingelifanywa na 'mafia' wa kujitegemea wasiopokea maagizo toka juu wangelidabuliwa kwa kasi ya mwanga na dunia nzima ikajua ndani ya muda mfupi ambao wewe hauwezi kuamini.
Mfumo wa kiutendaji wa majeshi yote ya kiulinzi na kiusalama hupokea amri zao na maagizo ya kila siku kutoka kwa amiri jeshi mkuu na pia wao kila siku huwasilisha 'SITREP' kuainisha utendaji na utekelezaji wa majukumu yao na maagizo ya boss wao.
Kwa maana hiyo sasa, tangu kina Tundu Lisu, Sanane na kina Gwanda ni mwendo wa kujiteka na kujipiga risasi wao kwa wao wenyewe tu bila ya gavamento kuhusika siyo!
Rais kama anafurahia matendo haya wanayofanyiwa raia wake, angelisherehekea kwa kunyamaza, ingelitosha sana kwa sababu hakuna anayeweza kuthubutu kuchongoroa domo lake kumuuliza pia ana kinga, hahojiwi.