Napinga kutumbuliwa kwa Mrisho Gambo

Cheo Ni dhamana aisee kwa hiyo Hana chaie Tena ? Ndio maana nasema mi nitabaki mkulima siogopi kupinduliwa au kukatwa au kupugwa au kutumbuliwa
 
bila shaka ww uliyeandika ndiye mwenyewe uliyetumbuliwa
 
Unapingana na Mh.Rais?.

yashatokea ni kukubali tu
 
Acha ushabiki wa kidini, eneo sio la waislam, ni open space ambayo tangu utawala wa mwinyi, mkapa, kikwete wote walikataa kulitoa kwa msikiti, tatizo nyinyi wenzetu (baadhi, ila wengi) you have a very poor understanding ,
 
Uchaguzi una mambo mengii...watu wanachorwaa tu apo na mipangoo yao ya kujidai wanafukuzana...usishangae ata makonda aka pigwa chini alafu baadae akawa waziri...wanachora watu tu
 
Gambo aombe msamaha, uzaifu wa Magu ni kumuomba msamaha
 
Alitemteua ndiye aliyemtengua...naye alishasema hapangiwi na mtu!

Wahenga walisema mpanda ngazi hushuka!

Everyday is Saturday........................... 😎
 
Wananchi wengi waliokwenda kumwona kutaka msaada watakuwa wamefurahi sana kutumbuliwa kwa kuwa hakuwa na msaada wowote Kama walivyo wateule wengi huko Mikoani na Wilayani. Alipanga kuwasikiliza wenye shida kila Jumanne na Alhamisi lakini zikawa ni siku za mateso na kujionyesha yeye ni nani huku watu wakirudi walikotoka na shida zao bila msaada wowote. Wengi, Mimi mmoja wao, wamefurahi sana kutenguliwa kwao ingawa hatua hiyo imechelewa sana na kuleta madhara makubwa. Yaliyokuwa yanatokea Arusha ndo yanatokea sehemu kubwa ya nchi yetu na siyo rahisi Rais kuyaona yote kwa muda mfupi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…