Napinga kutumbuliwa kwa Mrisho Gambo

Napinga kutumbuliwa kwa Mrisho Gambo

Cheo Ni dhamana aisee kwa hiyo Hana chaie Tena ? Ndio maana nasema mi nitabaki mkulima siogopi kupinduliwa au kukatwa au kupugwa au kutumbuliwa
 
Unapingana na Mh.Rais?.

yashatokea ni kukubali tu
 
Uongozi Wa Arusha ulikuwa na mgogoro mkubwa sana na waislam wa arusha, baada ya kumega eneo la msikiti mkuu wa arusha, waislam walitaka kuleta fujo siku ya idd wakatulizwa na viongoz wao, huu mgogoro ndio umewaondoa mkurugexzi na mkuuwake, wala sio maugomz yao
Acha ushabiki wa kidini, eneo sio la waislam, ni open space ambayo tangu utawala wa mwinyi, mkapa, kikwete wote walikataa kulitoa kwa msikiti, tatizo nyinyi wenzetu (baadhi, ila wengi) you have a very poor understanding ,
 
Uchaguzi una mambo mengii...watu wanachorwaa tu apo na mipangoo yao ya kujidai wanafukuzana...usishangae ata makonda aka pigwa chini alafu baadae akawa waziri...wanachora watu tu
 
Gambo aombe msamaha, uzaifu wa Magu ni kumuomba msamaha
 
Alitemteua ndiye aliyemtengua...naye alishasema hapangiwi na mtu!

Wahenga walisema mpanda ngazi hushuka!

Everyday is Saturday........................... 😎
 
Mheshiwa mkuu wa Nchi, umemtumbua Mrisho Gambo kimakosa sana.
Na hapa ninaona kama ameonewa sana.

Gambo alikuwa mkuu wa mkoa. Mkuu wa mkoa ndio top say ya mkoa wa Arusha, iweje Mkurugenzi na DC wasimheshimu?

Tofauti zao kubwa ni za kimadaraka. CED na DC ndio walistahili kumsikiliza Mkuu wao wa mkoa na kuheshimu yale wanayokubaliana.

Iweje mkuu wa Mkoa asimamie nafasi yake then hawa wa chini yake wasimheshimu?? Wamdharau??
Tunajua Mrisho ni mchapa kazi mzuri.

Haya maamuzi sio sahihi.

Gambo alikuwa anasimamia uongozi wake tu na kuheshimiwa.
Wananchi wengi waliokwenda kumwona kutaka msaada watakuwa wamefurahi sana kutumbuliwa kwa kuwa hakuwa na msaada wowote Kama walivyo wateule wengi huko Mikoani na Wilayani. Alipanga kuwasikiliza wenye shida kila Jumanne na Alhamisi lakini zikawa ni siku za mateso na kujionyesha yeye ni nani huku watu wakirudi walikotoka na shida zao bila msaada wowote. Wengi, Mimi mmoja wao, wamefurahi sana kutenguliwa kwao ingawa hatua hiyo imechelewa sana na kuleta madhara makubwa. Yaliyokuwa yanatokea Arusha ndo yanatokea sehemu kubwa ya nchi yetu na siyo rahisi Rais kuyaona yote kwa muda mfupi.
 
Back
Top Bottom