Napinga Mikel Arteta kupewa mikoba ya Wenger sababu hana uwezo

Napinga Mikel Arteta kupewa mikoba ya Wenger sababu hana uwezo

FB_IMG_1637449146741.jpg

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Kumpa kijana huyu mikoba ya kufundisha Arsenal itakuwa kamari ya kijinga sana kuicheza na nachukua nafasi hii kupinga kabisa njama hizo .

Arteta aliyezaliwa 26/3/1982 hana uzoefu wa maana wala ujasiri wowote wa kuipa Arsenal mataji , katika kipindi alichoitumikia Arsenal pamoja na kupewa Arm band hakuwahi kutoa mchango wowote wa kusaidia timu yake , hata kwa kuhamasisha kwa maneno tu kama wafanyavyo Ma Captain wa vilabu vingine , aliitwa Man City kuwa kocha msaidizi July 3 2016 , mpaka sasa ni chini ya miaka miwili , huyu si wa kupewa timu tajiri kama Arsenal

Arsenal inahitaji kocha mzoefu mwenye mafanikio yasiyotiliwa mashaka , Au la kama viongozi wanapenda kumpa kazi hiyo yule aliyechezea klabu yao basi nafasi hiyo wapewe wachezaji wenye uchungu mkubwa waliotoa jasho na damu kuipa timu mataji , wachezaji hao wapo na majina yao yanafahamika , lakini si Arteta .

Nakala imfikie Arsene Wenger .
Watakulaani wenzio
 
Huu uzi ufutwe sasa hauna maana tena ..
unafunga Leeds halafu unachapwa na Man city , chelsea , liverpool , man United , everton , tena goli tano tano halafu wategemea ubingwa ? utakuwa bwege sana kuamini timu hii
 
unafunga Leeds halafu unachapwa na Man city , chelsea , liverpool , man United , everton , tena goli tano tano halafu wategemea ubingwa ? utakuwa bwege sana kuamini timu hii
Hizo ni strategic management
Sawa anafungwa na Liverpool na kina city sasa ubora wa wachezaji wa liver, City utafananisha na wa kina saka arsenal?
Lakini bado mikel kabuni mbinu nyingine anapata points kwengine,sio lazima uchukulie points kwa hao wengine.

Mbona West Ham kapiga wakubwa wote ila kafungwa na arsenal? Na anafungwa na team unazoita ndogo mkuu?

Arteta anajitahidi atakuja kuwa kocha mkubwa.
 
WestHam aliwahi kuchukua ubingwa wa EPL mwaka gani ?
 
Back
Top Bottom