Napinga Ramadhani Kailima kuteuliwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, ni Kada wa CCM

Napinga Ramadhani Kailima kuteuliwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi, ni Kada wa CCM

Duh hiyo picha inanikumbusha statement ya Zitto kuwa tunaongozwa na Washamba.
 
Kurejeshwa kwa Kailima kuwa Mkurugenzi wa NEC akichukua nafasi ya Dr. Mahera, ni sawa na kejeli na dharau kubwa sana kwa Watanzania, Jambo hili ni sawa na matusi ya nguoni kwa Watanzania.

Huyu ni miongoni mwa Makada wakubwa kabisa wa CCM wa tangu enzi na enzi.

Ushahidi huu hapa akiwa na Mwigulu enzi zao UVCCM.

View attachment 2530740

Wakati Kagulumujuli akihujumu uchaguzi wa Kinondoni na kusababisha mauaji ya Akwilina , Kailima alikuwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi na akanyamaza , Kailima alihusika na kukamatwa kwa Salum Mwalimu aliyekuwa Mgombea wa Chadema kwenye vituo vya kupigia kura Magomeni akishirikiana na RC wa DSM wakati huo Paulo Makonda , Mtu kama huyu awezaje kuaminiwa na kurejeshwa tena Tume ya uchaguzi , kwa uteuzi huu Rais Samia ana malengo gani na Demokrasia ya Tanzania ?

Hata kama Watanzania ni Wajinga lakini si wajinga kwa kiwango ambacho mamlaka ya uteuzi inawaona , ni nani aliyesahau madudu ya Kailima hapo Tume ya Uchaguzi ?

Hakika kwa Uteuzi huu ninaamini Mungu hawezi kukubali na ATATENDA JAMBO , haliwezi kwisha hivi hivi tu .
Umenikumbusha wimbo nimepata kuusikia .... Teeeenda muujiza.....usiache siku ipite bila kutenda muujiza
 
Ulitarajia ateuliwe kada wa chadema?
Dai katiba wewe sio viposheni vyakazi
 
Lema si alisema huwa anaongea na Rais sasa si umwambie Lema amoigie Mama ili ambadilishe 😂😂😂😂😂
 
Huu uzi uingizwe kwenye maoni ya muswada wa sheria za uchaguzi kama sehemu ya maoni ya wadau
 
Kurejeshwa kwa Kailima kuwa Mkurugenzi wa NEC akichukua nafasi ya Dr. Mahera, ni sawa na kejeli na dharau kubwa sana kwa Watanzania, Jambo hili ni sawa na matusi ya nguoni kwa Watanzania.

Mtu kama huyu awezaje kuaminiwa na kurejeshwa tena Tume ya uchaguzi , kwa uteuzi huu Rais Samia ana malengo gani na Demokrasia ya Tanzania ?

Hata kama Watanzania ni Wajinga lakini si wajinga kwa kiwango ambacho mamlaka ya uteuzi inawaona , ni nani aliyesahau madudu ya Kailima hapo Tume ya Uchaguzi ?

Hakika kwa Uteuzi huu ninaamini Mungu hawezi kukubali na ATATENDA JAMBO , haliwezi kwisha hivi hivi tu .
Kwa taarifa yako, Watanzania wote waliopita JKT mpaka mwaka 1992, wote walikuwa CCM!.
Ramadhani Kailima ndie the best Mkurugenzi wa uchaguzi wapinzani zaidi ya 100 waliingia bungeni!. Hebu mshuhudie hapa
View: https://youtu.be/IY40h1ylhGg?si=J4iQfZI7hFMej6Gw

View: https://youtu.be/UuKX3zBuTsc?si=Sn2rPSq2QV7K5D4m

View: https://youtu.be/qo7NpVePtCg?si=P2x6PisHrEBTWzmk
P
 
Hakuna atakae kusikiliza
Nitawalazimisha kunisikiliza , nguvu ya JF si ya Mchezo , kwa yanayoendelea sasa kwenye maoni ya Wadau , Kailima atakuwa kiongozi wa kwanza wa Tume ya Uchaguzi kujiuzulu
 
Back
Top Bottom