Napinga vikali Uchunguzi wa Polisi na kumwita Hamza ‘gaidi’

Napinga vikali Uchunguzi wa Polisi na kumwita Hamza ‘gaidi’

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Hamza hakuwa gaidi kwa sababu zifuatazo:
1. Hamza baada ya kuwatwanga risasi aliendelea kutamba barabarani na bunduki zake zikiwa zimejaa risasi bila ya kudhuru raia ye yote.

2. Mahali ambapo Hamza aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi ilikuwa wazi sana kiasi kwamba polisi wenye ujuzi wangeweza kimkamata akiwa hai bila majeraha au kwa kujeruhiwa miguuni.

3. Kitendo cha askari kuendelea kumpiga risasi Hamza hata baada ya kuanguka chini na kuendelea kuipiga risasi maiti ya Hamza inaonyesha polisi wetu ama kukosa weledi wa kazi yao au kupoteza ushahidi kwa makusudi. Kwani polisi waligeuza maiti ya Hamza uwanja wa range wa kujifunzia shabaha.

4. Hamza angekuwa gaidi wa kidini kama DCI Wambura anavyodai angekuwa ameshambulia makanisa mengi na pia angekuwa ameua wakristu wengi sana. Aidha angekuwa ameshambulia misikiti na waislam wasio dhehebu lake.

5. Kwa muda wote ambao amekuwa kada wa CCM, wanachama wenzake na vyombo vya usalama vingekuwa vimeshamtambua. Kumbukeni uovu haujifichi kwa muda mrefu namna hii.

Ugaidi hauendeshwi na mtu mmoja hivyo kama Hamza angekuwa gaidi lazima angekuwa na wenzake ambao muda huu vyombo vya usalama vingekuwa vimewabaini na kuwatia mbaroni.

Nawashauri polisi wafanye kazi yao au waombe msaada wa uchunguzi kubaini ukweli. Katika suala hili polisi ni watuhumiwa hivyo hawana uhalali wa kujichunguza wenyewe na kutoa ukweli.
 
Hawajasema kuwa ni gaidi. Wamesema alikuwa na viashiria vya ugaidi.

Kabla ya tukio lile lililosababisha mauti yake na askari kadhaa.

Alijirekodi video akiwa ameshika bastola huku akiimba nyimbo za uhamasishaji hasa zinazotumiwa na vikundi vya ugaidi.

Ni kweli anaweza kuwa hakuwa gaidi lakini alikuwa na viashiria vya ugaidi.

Na mwisho ni namna alivyofanya tukio lenyewe ,linafanana na ugaidi.

Tusitetee tu kila kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namba 1: Gaidi huwinda na target ambayo inawika. Osama angeweza kushambulia jengo lolote Marekani lakini alichagua Trade Tower na Pentagon pekee. Anashambulia panapowika ila naye awike.

Namba 4: Gaidi husaka target yake, hapotezi lengo. Osama alishambulia ubalozi nchini Kenya na Tanzania lakini akilenga ubalozi wa Mareakani pekee. Angeweza kushambulia balozi nyingine lakini akamua kushughulika na Marekani pekee.

Namba 5: Paragraph ya pili inaonyesha wewe tayari ni mfuasi wa Hamza.

Hivyo vigezo vinamthibitisha Hamza alikuwa gaidi.
 
Mjumbe wa mkutano mkuu wilaya ccm ni GAIDI!
Naamini bado wengi sana ndani ya chama wamchunguze na ndu..guy ile video animcharaza mwanaccm mwezake bakora naona wazi kuna ugaidi mkubwa ataufanya badae.
We! Wewe! Unashangaa mjumbe wa kamati kuu kuwa Gaidi! Basi, hujui Tanzania! Ndani ya Tanzania - hata mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani, ni Gaidi!
 
Hawajasema kuwa ni gaidi. Wamesema alikuwa na viashiria vya ugaidi.

Kabla ya tukio lile lililosababisha mauti yake na askari kadhaa....
Ndiyo wakamfanya uwanja wa range kujifunzia shabaha?
 
Eti alikuwa anaishi kwa siri!!! 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 mtu anaishi kwa siri inakuwaje anafikia hadi kuwa mjumbe wa Mkutano wa wilaya ya Ilala maccm?
Hamza hakuwa gaidi kwa sababu zifuatazo:
1. Hamza baada ya kuwatwanga risasi aliendelea kutamba barabarani na bunduki zake zikiwa zimejaa risasi bila ya kudhuru raia ye yote...
 
Police wetu kwa bahati mbaya sana hawajui maana ya neno GAIDI - Ama kwa kimombo terrorist.

Wikipedia wasaide police wetu.

Ugaidi ni mfumo wa kulenga mabadiliko ya kisiasa kwa kutisha watu kwa njia ya vurugu au mauaji. Matendo ya kigaidi yanatisha kwa sababu watu wanajeruhiwa au kuuawa. Watendaji wa ugaidi kwa kawaida ni vikundi au watu wasio na cheo au nafasi rasmi.

Mara nyingi si rahisi kutofautisha kati ya magaidi, wapinzani wa uhuru au watu wanaoendesha vita ya msituni. Hata jeshi rasmi za serikali zinaweza kutumia mbinu za kigaidi lakini kwa kawaida hawahesabiwi kati ya magaidi.

A person who uses unlawful violence and intimidation, especially against CIVILIANS, in the pursuit of political aims.

Hitimisho: Kwa sababu Ndugu Hamza hakushughulika na Raia kabisaaa - hakuwa Gaidi.
 
Eti alikuwa anaishi kwa siri!!! 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 mtu anaishi kwa siri inakuwaje anafikia hadi kuwa mjumbe wa Mkutano wa wilaya ya Ilala maccm?
Polisi wakizidiwa wanakuwa kama kuku aliyefyekwa kichwa na kuanza kuruka ruka hovyo! 🤣🤣🤣Sasa wajibu hiyo hoja alipataje ujumbe wa chama chao CCM kama alikuwa anaishi kwa siri?
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 ni wahuni hao waliopoteza heshima kwenye jamii ya Watanzania na ndiyo sababu wanachukiwa sana nchini kote kuliko hata ukoma.
Polisi wakizidiwa wanakuwa kama kuku aliyefyekwa kichwa na kuanza kuruka ruka hovyo! 🤣🤣🤣Sasa wajibu hiyo hoja alipataje ujumbe wa chama chao CCM kama alikuwa anaishi kwa siri?
 
Uwaue polisi baada ya hapo uende kutamba mbele ya geti la ubalozi wa Ufaransa, eneo ambalo miaka 23 iliyopita mwezi kama huu huu watukio la Hamza lilikuwa ni muhanga pacha wa shambulio la kigaidi kwenye ubalozi wa Marekani. Hili linatosha kuhusisha tukio la Hamza na ugaidi.

Kuna jambo la Hamza kupenda kutumia bodaboda kubwa kama magaidi wa talibani kule kandrahaa Afghanistan. Bahati mbaya majirani hawakuulizwa kama marehemu Hamza kuna wakati alipendalea kuvaa paddle pusher au la? Kitendo Hamza alichofanya mazishi yake pamoja na kwamba yalifanyika usiku lakini alizikwa kama shujaa flani.

Kama wako ambao hawaridhiki yaani wale wenye macho na wamejivika upofu na masikio wakaamua kujivika ukiziwi basi waiombe serikali iunde tume huru kuliko kuanzisha hii midahalo itakayoongeza chuki kwenye jamii. Ni ulize kwenye wale Polisi walio uwawa na Hamza yuko mwisilamu yeyote pale?
 
Nchi hii Mbovu sana Gaidi gani linaua Polisi tu yani Gaidi la kuwaambia watu wapishe kweli hii Nchi Mbovu yani kuna siku moja tunaamua tunawatoa wote Watawala yani yanaudhi kuliko hata Mtoto mdogo anaeuliza maswali bila kuchoka
 
Nchi hii Mbovu sana Gaidi gani linaua Polisi tu yani Gaidi la kuwaambia watu wapishe kweli hii Nchi Mbovu yani kuna siku moja tunaamua tunawatoa wote Watawala yani yanaudhi kuliko hata Mtoto mdogo anaeuliza maswali bila kuchoka
Duuh 😁😁😁
 
Back
Top Bottom