Uchaguzi 2020 Napinga viongozi wa dini kukutana kwa lengo la kuelezea kinachoitwa mafanikio ya Rais Magufuli, hii ni kampeni na haikubaliki

Uchaguzi 2020 Napinga viongozi wa dini kukutana kwa lengo la kuelezea kinachoitwa mafanikio ya Rais Magufuli, hii ni kampeni na haikubaliki

Naona zinatumika nguvu nyingi sana kupamba hii awamu,yaani utadhani nchi inapaa angani kwa mafanikio kumbe kawaida tu.Nchi bado ina changamoto kibao wanakosa muda na akili zakuisaidia serikali hili iendelee kupambana nazo wao wamekali kusifu nakupamba.
Umaskini wa akili na vipato unatutesa sana, badala ya kufanya kazi ya MUNGU wamegeuza dini ni biashara
 
Wakisema akina Bagonza na Mwamakula mbakenua. Tulieni dawa iwaingie.
 
Mbona maaskofu wakikemea unakuwaga wa kwanza kuanzisha uzi humu kusifia.

Unataka mambo yanayokufurahisha tu ndo yatendeke. Tengeneza dunia yako!
Utaafiki hivyo hivyo kama viongozi wa dini watakusanyika Kwa lengo la kuelezea mabaya ya serikali ya awamu ya 5?

Viongozi wa dini kwa nafasi zao wanapaswa kuunga mkono au kukosoa serikali, napinga hili la kukusanyika kwa ajili ya hilo!
 
Waache Kujipendekeza,Mkuu hataki mambo ya kujipendekeza kwake.
 
Tafadhalini sana nyie ndugu zetu wakikristo, mara nyingi tumemijuza kuwa Bakwata sio taasisi ya waislamu, hiyo ni taasis ya serekali, na iliundwa na Nyerere na Mark Bomani, na hao munaowaita Mashehe hawana tofauti na Gwajima.

Anayeunga mkono juhudi aunge kama mwanachama wa chama, hai ni wanachama wenzetu ndani ya ccm.
Umejua kunifurahisha,eti Bakwata ni taasis ya serikali na iliundwa na Nyerere na Mark Bomani
 
Mmesahau na nyie mlienda na askofu wenu asie na kanisa hospital kwa kina mdee akaanza kuongea siasa uchwara [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sijaona ulazima wakufanya yote hayo,kwani watu hawayaoni hayo mazuri mpaka wanatumia nguvu kubwa hivyo kuwaaminisha watu uongo.
"Chema chajiuza, kibaya chajitembeza" Shaaban Robert
 
Naona sifa ruksa Ila kukosoa marufuku siasa na dini kweli hii nchi chiboko
 
Wavae na mashati ya kijani kabisaaa. Wavue kanzu zao
Wavae kanzu ya kijani kama ya Nabii Tito
JamiiForums-795763129.jpg
 
Mbona maaskofu wakikemea unakuwaga wa kwanza kuanzisha uzi humu kusifia.

Unataka mambo yanayokufurahisha tu ndo yatendeke. Tengeneza dunia yako!
kazi ya Askofu si kusifia wanadamu bali....

1. kukemea
2. kuombea baraka
3. kuombea uponyaji
4. kutoa sifa kwa Mungu
 
Back
Top Bottom