Uchaguzi 2020 Napinga viongozi wa dini kukutana kwa lengo la kuelezea kinachoitwa mafanikio ya Rais Magufuli, hii ni kampeni na haikubaliki

Umaskini wa akili na vipato unatutesa sana, badala ya kufanya kazi ya MUNGU wamegeuza dini ni biashara
 
Wakisema akina Bagonza na Mwamakula mbakenua. Tulieni dawa iwaingie.
 
Mbona maaskofu wakikemea unakuwaga wa kwanza kuanzisha uzi humu kusifia.

Unataka mambo yanayokufurahisha tu ndo yatendeke. Tengeneza dunia yako!
Utaafiki hivyo hivyo kama viongozi wa dini watakusanyika Kwa lengo la kuelezea mabaya ya serikali ya awamu ya 5?

Viongozi wa dini kwa nafasi zao wanapaswa kuunga mkono au kukosoa serikali, napinga hili la kukusanyika kwa ajili ya hilo!
 
Waache Kujipendekeza,Mkuu hataki mambo ya kujipendekeza kwake.
 
Haya mapambio hadi yanachosha kusikiliza!
 
Umejua kunifurahisha,eti Bakwata ni taasis ya serikali na iliundwa na Nyerere na Mark Bomani
 
Mmesahau na nyie mlienda na askofu wenu asie na kanisa hospital kwa kina mdee akaanza kuongea siasa uchwara [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sijaona ulazima wakufanya yote hayo,kwani watu hawayaoni hayo mazuri mpaka wanatumia nguvu kubwa hivyo kuwaaminisha watu uongo.
"Chema chajiuza, kibaya chajitembeza" Shaaban Robert
 
Naona sifa ruksa Ila kukosoa marufuku siasa na dini kweli hii nchi chiboko
 
Mbona maaskofu wakikemea unakuwaga wa kwanza kuanzisha uzi humu kusifia.

Unataka mambo yanayokufurahisha tu ndo yatendeke. Tengeneza dunia yako!
kazi ya Askofu si kusifia wanadamu bali....

1. kukemea
2. kuombea baraka
3. kuombea uponyaji
4. kutoa sifa kwa Mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…